Pakua App Yetu Playstore Bofya Hapa!

XKILIMO

UTUNZAJI KUMBUKUMBU Na. Mshindo Media


UNAWEKAJI  KUMBUKUMBU ZA SHAMBA LAKO

     Uwekaji wa kumbukumbu utakuwezesha kutambua ufanisi wa shughuli mbalimbali zinazofanyika shambani kwako. Mathalani, kuweza kutambua faida kiasi gani imepatikana kutokana na uzalishaji wa maziwa, au kutokana na uzalishaji wa mahindi? Uwekezaji upi una tija au upi husababisha hasara?,

Ni dhahiri unahitaji kujua taarifa fulani iwapo utahitaji kubadili zao unalolizalisha au pale unapoamua kununua au kutonunua ng’ombe mwingine. Vilevile wakati unapoamua kuchukua mkopo kutoka mabenki au taasisi zozote nyinginezo zinazokopesha pesa inapasa kuwasilisha kumbukumbu za shamba lako ili kuweza kuonyesha jinsi shamba lako linavyojiendesha kwa ufanisi. Ni dhahiri inakuwa vigumu kupatiwa mkopo bila ya kuwa na ushahidi wa kumbukumbu za namna shamba lako unavyoliendesha.

 

ORODHESHA MALI ZOTE ZILIZOPO KWENYE SHAMBA:

Hii ni hatua ya awali inayopasa kufanywa. Orodha sahihi ya mali zilizopo shambani inapasa kuzingatiwa ili kumwezesha mkulima au mfugaji kuweza kutambua mali zitakazomsaidia katika uzalishaji wake, mathalani majengo yaliyopo ukubwa na ujazo na matumizi yake: pembejeo za mifugo, mashine na mali nyinginezo zilizopo. Zote hizi zinapasa kuorodheshwa na tathimini ya kipesa ya kila moja ifanyike kwa ufasaha. Pia kupanga mipango ya hatua zinazofuata, kuchora ramani ya shamba lako ikionyesha mipangilio na sura ya maumbile ya sehemu zote pia ni muhimu, kadhalika kufahamu lina heka au hekta ngapi na kati ya hizo ngapi zinatumika kwa uzalishaji mazao, mabanda, nyumba na kiasi gani ni ardhi isiyofaa?,Vilevile ni muhimu kuzingatia mambo yafuatayo:

UWEKAJI KUMBUKUMBU NI MUHIMU
UWEKAJI KUMBUKUMBU NI MUHIMU

UPATIKANAJI WA MAJI:

Namna gani utapata maji ya kumwagia mazao yako, je kuna mto unapita karibu na shamba? Au utahitajika kupata maji kutoka mbali? Upatikanaji maji kutoka maeneo ya mbali na shamba kutahitaji kuwepo wafanyakazi wa kutosha na muda wa ziada na kuwa na mikakati thabiti ya kuanzisha na mfumo wa umwagiliaji.

 

HALI YA HEWA:

Kuwa na kumbukumbu ya misimu ya mvua ya mahali husika: Siku ngapi mvua hunyesha kwa mwaka? Je kiasi cha mvua hubadilika kila baada ya miaka fulani? Na kama jibu ni ndiyo, mabadikiko haya hutokea kwa namna gani? Kiwango cha mvua ndiyo humwezesha mkulima kuamua aina ipi ya mazao anaweza kuyapanda kwa vile maji ya kutosha yatahitajika kwa ajili ya umwagiliaji. Je unapendelea kuwa na msimu mmoja au miwili ya uzalishaji kwa mwaka? Vilevile yapasa kutambua aina ya udongo na uoto wa asili kwenye shamba lako na mabadiliko ya muda mrefu kwa vile yatakusaidia kubadilisha shughuli za kilimo za mahali husika. Kadhalika kumbukumbu za magonjwa ni muhimu kuzingatiwa.

 

Baadhi ya mifano ya kumbukumbu ni kama zinavyooneshwa hapo chini:

 

KUMBUKUMBU ZA UTENDAJI:

Kila shughuli inayofanyika lazima iingizwe kwenye kumbukumbu, kama inavyopendekeza kitaalamu ni vyema kuwa na ufahamu wa bei ya pembejeo, tarehe, mahali ziliponunuliwa na gharama ya kila moja.

 

REKODI ZA UZALISHAJI WA MAZAO:

Weka kumbukumbu sahihi ya kiasi gani cha mbegu au miche ulipanda shambani, vitalu vingapi, ukubwa na siku zipi ulivitayarisha? Weka alama kwenye kila kitalu, weka jina la miche uliyootesha kitaluni. Vilevile weka kumbukumbu ya muda na siku ambazo utahitaji kuzalisha mazao yako. Weka taarifa ya samadi au mbolea uliyotumia. Kama ulitayarisha wewe mwenyewe? basi weka kumbukumbu ya pembejeo ulizochanganya na gharama zake. Vilevile weka kumbukumbu ya idadi ya magunia au kilo ya zao husika ulizoweza kuvuna. Pia weka taarifa kuhusu kiasi gani cha mavuno ulichotumia wewe mwenyewe na idadi gani uliuza pia kumbukumbu ya tarehe, bei na sehemu husika ni muhimu kuwekwa.

 

KUMBUKUMBU ZA UZALISHAJI WA MIFUGO:

Idadi ya ngombe, mbuzi au kuku wako na kadhalika, kumbukumbu ya mifugo mipya iliyozaliwa, uzito na wazazi wao. Weka kumbukumbu ya kiasi cha fedha ulichotumia kwa malisho, maji, kutayarisha mabanda na tiba kwa mifugo na nyinginezo kipindi chote cha uhai wa mifugo husika. Weka hesabu ya kiasi cha nyama, maziwa, mayai na mazao mengine yaliyopatikana, uliyotumia wewe mwenyewe, kiasi ulichouza tarehe na mahali husika.

 

KUMBUKUMBU ZA GHALA:

Kumbukumbu kama vile ukubwa wa ghala na kiasi cha fedha zilizotumika kujenga maghala husika.

 

KUMBUKUMBU ZA WAFANYAKAZI:

Idadi ya wafanyakazi waliofanya kazi shambani kwako: kwa masaa na siku ngapi? Zingatia kuweka rekodi ya namna na kiasi gani cha pesa ulichowalipa? (hapa lazima ujumuishe hata malipo uliyowalipa ndugu wa karibu).

Kila mwisho wa mwezi fanya tathmini ya mapato (mazao na tathmini ya kipesa ya mazao yako, mauzo ya mifugo na mengineyo) yatokanayo na shughuli uzifanyazo shambani kwako na utoe kiasi cha pesa ulichotumia kughalamia pembejeo (gharama za mbolea, malipo ya vibarua/wafanyakazi, mbolea na mengineyo) kutoka kwenye mapato. Kiasi kitakachosalia ndiyo itakuwa faida uliyopata..

 

BAADHI YA MIFANO YA KUMBUKUMBU MBALIMBALI ZA MASHAMBANI

 

KADI NA 1. KUMBUKUMBU ZA AFYA ZA NG’OMBE

KUMBUKUMBU ZA AFYA YA NG'OMBE

 

KADI NA 2. KUMBUKUMBU ZA NG’OMBE ANAYEKAMULIWA

KUMBUKUMBU ZA NG’OMBE ANAYEKAMULIWA

 

KADI NA 3. KUMBUKUMBU ZA IDADI YA NG’OMBE KWA MAKUNDI

KUMBUKUMBU ZA IDADI YA NG’OMBE KWA MAKUNDI

 

KADI NA 4. KUMBUKUMBU ZA KIASI CHA CHAKULA CHA ZIADA

KUMBUKUMBU ZA KIASI CHA CHAKULA CHA ZIADA

 

KADI NA 5. KUMBUKUMBU ZA KUZALIWA NDAMA NA JINSIA YA NDAMA

KUMBUKUMBU ZA KUZALIWA NDAMA NA JINSIA YA NDAMA

 

KADI NA 6. KUMBUKUMBU ZA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA

KUMBUKUMBU ZA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA

About Veterinary Centre&Animal Care

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.