Pakua App Yetu Playstore Bofya Hapa!

XBUSTANI

MJASIRIAMALI:MBINU MBALIMBALI ZA KILIMO NA UFUGAJI I Mshindo media

 1. KILIMO BORA CHA NJEGERE

  KILIMO BORA CHA PILIPILI MANGA
  KILIMO BORA CHA PILIPILI MANGA
  KILIMO BORA CHA PILIPILI MANGA: Pilipili mtama au kwa jina lingine pilipili manga ni kiungo muhimu sana katika mapishi. Radha yake ya muwasho ndio kitu hasa kinachotafutwa katika vipunje vidogo vidogo vya zao hili. Pilipili manga husagwa ili kupata ungaunga kabla ya kutumika ingawa pia inaweza kutumika bila kusagwa.
  Jina la kitalaam ni Piper nigram na kwa kiingereza ni black pepper. Zao hili asili yake ni Mashariki ya Mbali, na linalimwa zaidi katika mkoa wa Tanga na Zanzibar. Ingawa pia inaweza kukubali katika maeneo ya Kagera
  Pilipili nyeusi na nyeupe zote hutumika kwa mapishi ya nyama, samaki na kwa mapishi mengine mbalimbali. Nchi za magharibi zina matumizi makubwa ya viungo hivi. Aidha pilipili mtama nyeusi ndiyo huzalishwa zaidi hapa nchini.

  Namna ya uzalishaji wa pilipili manga.

  1. Hali ya hewa na udongo
  Viungo vingi humea katika maeneo yenye joto la wastani kati ya nyuzi joto 24-26 na huzalishwa maeneo ya mwambao. Udongo wenye rutuba na unaopitisha maji na wenye uchachu wa kiasi cha pH 6.5. Mahitaji ya mvua ni mililita 1500-2000 kwa mwaka.
  1. Uchaguzi wa mbegu
  Uchaguzi huzingatia mambo yafuatayo:-
  1. a) Urefu wa pingili na ukubwa wa majani
  2. b) Ufupi wa pingili unaoambatana na majani madogo.
  Tofauti iko hadi kwenye umbile la matunda. Majani ya mche mama sehemu kinapokatwa kipando huondolewa wiki mbili kabla ya kukata. Vipando vyenye macho (nodes) 3-4 humika. Macho mawili huzikwa kwenye udongo na kipando kiwekewe kivuli. Inashauriwa kuweka mbolea ya samadi wakati wa kupanda.  PILIPILI MANGA

  1. Nafasi ya upandaji
  Nafasi ya kupanda ni mita 2-3 kati ya mmea na mmea endapo miche imepandwa na miti inayotakiwa kupogolewa mara kwa mara.
  1. Mahitaji ya mbolea
  Matumizi ya mbolea hapa Tanzania si makubwa katika kilimo cha viungo. Ingawa kiasi cha kilo 0.4 cha Urea, kilo 0.3 cha Superphosphate na kilo 0.3 cha Potash ya Muriate kinaweza kutumika kwa miche mikubwa.
  1. Miti ya kusimikia miche
  Miche hupandwa kwa kusimikiwa nguzo ili ikue kwa kujizungusha kwenye miti kama mijenga ua, n.k. Mti huo wa kusimikia nao pia hupaswa kupunguziwa majani ili kupunguza giza. Kila kabla ya msimu miti hiyo hupaswa kupunguziwa matawi (pruning).
  Kupogolea miche ya pilipili mtama
  Mche ukifikia miezi 18 inapaswa kupogolea kwa kukata sehemu ya juu ya mche ili kufanya matawi mengine yachipue chini ya mche. Inashauriwa mche kuwa na urefu wa mita 3-3.5.

  Uvunaji
  Maua ya kwanza hutoka baada ya miaka miwili. Matunda hukomaa miezi tisa (9) hadi kumi (10). Uvunaji ni mizunguko 5 hadi 6 kwa mwaka. Pilipili mtama inaweza kuvunwa kwa misimu miwili. Mavuno ni kati ya tani 0.35 – 3.75 kwa hekta. Wakati wa uvunaji kishina cha matunda ya kijani hukatwa kutoka kwenye mti kisha mbegu za huchambuliwa kutoka kwenye vishina na kisha huanikwa juani kwa siku 3 hadi 4 ili kuhakikisha zinakauka vizuri kabisa. Kiasi cha unyevu kiwe angalau 13 – 14%.
  PILIPILI MTAMA
  PILIPILI MTAMA
  Kuhifadhi
  Pilipili mtama iliyokaushwa vizuri inaweza ikawekwa kwenye chombo kisichopitisha hewa na kudumu kwa miaka hadi 20 bila kuharibika.
  Masoko ya pipili mtama
  Soko la pilipili matama linapatikana ndani ya nchi na nje pia. Bei ya ndani ni kati ya Sh1,000-1,500. Zao hili huuzwa katika nchi za Uganda, Kenya, Uingereza, Ujerumani, Mashariki ya Kati, n.k. Bei ya Nje ni wastani wa dola za kimarekani 1,985 kwa tani. (Tafadhali fanyia utafiti soko, data hizi ni za siku  nyingi)


  KILIMO BORA CHA VITUNGUU
  KILIMO BORA CHA VITUNGUU
  KILIMO BORA CHA VITUNGUU: 
  Hapo awali kitungu kilikuwa ni zao lililokuwa linapatikana porini katika ukanda wa bahari ya Mediterania. Zao hili hulimwa katika nchi nyingi za magharibi, nchi za milima zilipo kaskazini mwa dunia, likwemo bara la Afrika. Vitunguu hustawi katika hali ya hewa ya jotoridi 13°C – 24°C, hali ya hewa inayofaa kwa kuotesha na kukuzia miche kwenye kitalu ni jotoridi 20°C – 25°C. Kwa kawaida vitunguu huhitaji kiasi cha joto nyuzi 20°C-25°C ili kuweza kustawi na kukua vizuri. Joto zaidi ya hapo hufanya vitunguu kudumaa na kutoweza kutengeneza viazi (bulbs).


  KILIMO CHA VITUNGUU
  KILIMO CHA VITUNGUU
  Matumizi
  Kitunguu hutumika kama kiungo cha kuongeza ladha kwenye chakula, na pia hutumika kama dawa ya kansa ya tumbo, vidonda na majipu.
  Ustawi
  Zao la vitunguu hustawi katika udongo wa tifu tifu wenye mbolea ya kutosha, ukiwa na uchachu wa udongo (PH) kiasi cha 6 – 6.8.  Udongo wa mfinyanzi haufai kwa zao la vitunguu kwa kuwa hauruhusu viazi vya vitunguu (bulbs) kutanuka.  Hivyo uwezekano wa kupata mazao ni mdogo. Pia udongo wa kichanga haufai kwa zao la kitunguu kwa kuwa hauna mbolea na hivyo vitunguu huwa vidogo sana, jambo ambalo ni vigumu kupata mazao yanayofaa kwa soko.
  Zao la kitunguu huhitaji unyevu muda wote wa ukuaji wake. Zao hili lina mizizi mifupi hivyo linahitaji kumwagiliwa maji mara kwa mara.
  AINA ZA VITUNGUU
  AINA ZA VITUNGUU
  AINA ZA VITUNGUU

  Kuna aina mbili za vitunguu ambazo zimezoeleka
  :
  • Vitunguu vya asili kama vile Singida, na Rujewa (aina hii ina rangi ya kahawia iliyopauka).
  • Chotara: Hii ni aina ya vitunguu inayojulikana kama vitunguu vya kisasa. Katika kundi hili kuna vitunguu kama Texas grano, Red creole, Bombay red, White granex, na Super rex.
  Mgawanyiko
  Zao la vitunguu limegawanyika katika makundi mawili. Hii inatokana na uhitaji wa mwanga na ukuaji wake.  Aina ya kwanza inahitaji mwanga kwa saa 8-13 ili kuweza kuchanua na kutoa mbegu.
  Aina ya pili inahitaji mwanga kwa saa 13-15 kuweza kuchanua na kutoa mbegu.
  UPANDAJI WA VITUNGUU
  Kupanda
  Vitunguu hupandwa kwa kutumia mbegu ambazo husiwa kwenye vitalu.  Kitalu kinaweza kuwa na upana wa mita 1, urefu unategemeana na ukubwa wa eneo ulilo nalo.
  Unaweza kupanda vitunguu kwenye matuta mbonyeo (Sunken bed). Aina hii ya upandaji hutumika kwenye eneo lenye shida ya maji. Upana wa tuta uwe mita moja.
  Kupanda kwenye matuta mwinuko (Raised bed) upandaji wa iana hii hutu mika sehemu yenye maji mengi au yanayotuama.
  Tahadhari: Maji yakituama kwenye vitunguu hufanya vitunguu kuoza, hivyo kuathiri mavuno.
  Nafasi
  Vitunguu vipandwe kwa nafasi ya sentimita 7.5 kutoka mche hadi mche, sentimita 12.5 kutoka mstari mmoja hadi mwingine kwenye matuta.
  UDONGO MZURI KWA VITUNGUU
  UDONGO MZURI KWA VITUNGUU
  Mbole ya kupandia
  Unaweza kutumia mboji, au samadi iliyo oza vizuri kupandia. Baada ya hapo unaweza kuongeza mboji baada ya miezi miwili. Endapo unafanya kilimo kisichozingatia misingi ya kilimo hai, unaweza kupanda kwa kutumia mbolea aina ya NPK (20:10:10) baada ya mwezi na nusu, unaweka mbolea ya Urea.
  Palizi
  Vitunguu ni zao lenye uwezo mdogo sana wa kushinda na magugu. Hivyo, inabidi shamba liwe safi muda wote wa ukuaji hadi kuvuna.
  UVUNAJI VITUNGUU
  UVUNAJI VITUNGUU
  Uvunaji
  Kwa kawaida, vitunguu huchukua muda wa miezi 5-6 tangu kupandwa hadi kuvunwa. Unaweza kuanza kuvuna vitunguu baada ya asilimia 75 ya shingo za vitunguu kuvunjika.  Baada ya kuvuna, unaweza kuweka kwenye madaraja (grades) kwa kufuata ukubwa, rangi na unene wa shingo ya kitunguu. Vitunguu vyenye shingo nyembamba hudumu zaidi, vyenye shingo nene huoza haraka.
  Ukataji
  Hakikisha kuwa shingo ya kitunguu inabaki kiasi cha sentimita 2. Hii husaidia kuzuia kuoza haraka.
  Namna ya kuhifadhi vitunguu
  Baada ya kuvuna, hifadhi vitunguu kwenye kichanja chini ya kivuli na uvitandaze vizuri.  Unaweza kuhifadhi vitunguu kwa kufunga kwenye mafungu na kuvitundika.  Vitunguu vikihifadhiwa vizuri vinaweza kukaa hadi miezi minne bila kuharibika, hii hutegemeana na aina ya uhifadhi.

  Wadudu wanaoshambulia vitunguu

  Kuna aina nyingi za wadudu wanaoweza kushambulia vitunguu.  Hawa wafuatao ni baadhi ya wadudu waliozoeleka kwenye zao la vitunguu.
  WADUDU WABAYA
  WADUDU WABAYA
  Thiripi (Thrips): Wadudu hawa hukaa kwenye jani sehemu inayokutana na shina. Wadudu hawa hufyonza maji kwenye majani ya vitunguu na kusababisha majani kuwa na doti nyeupe.
  Madhara: Husababisha vitunguu kudumaa hivyo kuathiri ukuaji wake jambo ambalo huathiri mavuno pia


  KITUNGUU
  KITUNGUU
  Kimamba: Wadudu hawa hufyonza maji kwenye vitunguu, na kusambaza ugonjwa wa virusi. Husababisha kudumaa kwa vitunguu. Wadudu hawa ni hatari zaidi kwa kuwa husambaza virusi vinavyoingia hadi kwenye mbegu.
  Minyoo fundo (Nematodes): Aina hii ya minyoo hushambulia mizizi ya vitunguu. Hali hii husababisha kudumaa kwa vitunguu kwa kuwa hushindwa kufyonza maji na chakula kutoka ardhini.
  Vidomozi (Leaf minor): Hushambulia majani kwa kujipenyeza kwenye ngozi ya jani na kusababisha michoro ambayo huathiri utendaji wa majani.
  Utitiri mwekundu (Red spider mites): Wadudu hawa hufyonza maji kwenye majani na kusababisha vitunguu kunyauka.
  Funza wakatao miche: Funza hawa hutokana na wadudu wajulikanao kama Nondo, na hushambulia shina na kulikata kabisa.
  Namna ya kukabiliana na wadudu hawa
  Unaweza kukabiliana na wadudu hawa kwa kufanya kilimo cha mzunguko.  Usioteshe vitunguu sehemu moja kwa muda mrefu, au kufuatanisha mazao jamii ya vitunguu kama vile leaks.
  Tumia mbegu bora zilizothibitishwa kutoka kwenye kampuni zinatambuliwa kisheria na kibiashara.  Kupanda kwa wakati unaotakiwa; vitunguu visipandwe wakati wa kiangazi. Vipandwe wakati wa majira ya baridi na kuvunwa wakati wa joto. Tumia dawa za asili za kuulia wadudu, au dawa nyinginezo zinazopendekezwa na wataalamu wa kilimo.
  UGONJWA KWA VITUNGUU
  UGONJWA KWA VITUNGUU
  1. Purple blotch: Ugonjwa huu husababishwa na ukungu (fungus). Ugonjwa huu husababisha mabaka ya zambarau na meusi katika majani ya vitunguu.  Ugonjwa huu hutokea wakati wa unyevu unyevu mwingi.
  Madhara: Ugonjwa huu hupunguza mavuno mpaka asilimia hamsini (50%).
  2. Stemphylium leaf blight: Hukausha majani kuanzia kwenye ncha hadio kwenye shina.; Ugonjwa huu hutokea wakati wa unyevu na ukungu mwingi.
  Madhara: Hupunguza mavuno hadi kwa asilimia sabini na tano (75%).

  VITUNGUU
  VITUNGUU

  1.  Magonjwa ya virusi (Onion yellow draft virus): Ugonjwa huu husababisha vitunguu kuwa na rangi iliyochanganyika, kijani na michirizi myeupe au njano.  Vitunguu hudumaa kwa kiasi kikubwa;Ugonjwa huu husababishwa na kimamba. Madhara: Huathiri mavuno kwa asilimia 80 mpaka asilimia 100%.
   4. Kuoza kwa kiazi (Bulb rot): Husababishwa na fangasi. Ugonjwa huu hutokea vitunguu vikishakomaa, huku udongo ukiwa na maji maji.  Vitunguu vikishakomaa visimwagiliwe tena.
   Uharibifu wa vitunguu usiotokana na magonjwa
   1. Kuchipua baada ya kuvunwa: Hali hii hutokea endapo vitunguu vitavunwa kabla ya muda wake.  Endapo vitunguu havitakaushwa vizuri baada ya kuvunwa. Hali hii husababisha uharibifu mpaka asilimia themanini (80%).  Sehemu ya kukaushia vitunguu iwe na hewa inayozunguka na mwanga wa kutosha. Vitunguu vikiwekwa gizani huchipua kwa urahisi.
   2. Muozo laini (Soft rot): Ugonjwa huu hushambulia vitunguu baada ya kukomaa; husababishwa na vimelea (bacteria). Vitunguu hutoa harufu mbaya ya uozo.  Kuepuka hilo vuna kwa wakati unaofaa, hifadhi sehemu yenye mwanga na hewa inayozunguka.
  MAGONJWA MABAYA KWA VITUNGUU
  MAGONJWA MABAYA KWA VITUNGUU
  Virusi
  Unaweza kuzuia vimamba ambao ndio wanaoeneza virusi kwa kutumia dawa za kuulia wadudu.
  Vitunguu vinalipa
  “Vitunguu vinatofauti kidogo na mazao mengine ya mboga mboga kwa kuwa si rahisi kukosa soko, na endapo bei si nzuri unaweza kuhifadhi kwa muda ili kusubiri bei iwe nzuri.” Ni maneno ya mkulima Peniel Rodrick (pichani) ambaye amejikita zaidi katika kilimo cha vitunguu kibiashara.
  Mkulima huyu kutoka kijiji cha Oloigeruno anasema pamoja na kwamba anazalisha pia mazao mengine, lakini ameamua kujikita zaidi kwenye vitunguu baada ya kugundua siri na namna ya kupata faida zaidi.
  Toka aanze kilimo cha vitunguu miaka 12 iliyopita, ameweza kuendesha maisha yake vizuri, ikiwa ni pamoja na kuanzisha miradi mingine kama ufugaji wa ng’ombe, kujenga nyumba ya kisasa na kuitunza familia yake ya watoto watatu ipasavyo. Pamoja na hayo anasema tatizo kubwa la vitunguu ni magonjwa na wadudu. Anasema si rahisi sana kugundua mara moja kuwa kuna ugonjwa unaoshambulia vitunguu, na mara unapogundua unakuwa umefikia kwenye hali mbaya

  Add a comment 2. KILIMO BORA CHA KABICHI
  KILIMO BORA CHA KABICHI
  KILIMO BORA CHA KABICHI : 
  Unaweza kulima kabichi msimu wote wa mwaka. Soko lake ni la uhakika katika kipindi chote na ni muhimu kwa afya. Pia, linaweza kutumika kama malisho ya mifugo
  Kabichi ni moja ya mazao yaliyomo katika jamii ya mimea inayojumuisha mimea ya kaulifulawa (cauliflower ), kabichi ya kichina na kale. Kwa kawaida kabichi hupandwa kwa msimu mmoja, lakini iwapo itakuzwa kwa ajili ya kutoa mbegu hukuzwa zaidi ya msimu mmoja. Endapo inalimwa sehemu yenye maji ya kutosha, inaweza kulimwa msimu wote wa mwaka. Kichwa cha kabichi kinapofunga vizuri, hutumika kama chakula na huvunwa baada ya kufunga na kukomaa vizuri.
  Mizizi: Mizizi ya kabichi hutawanyika ardhini vizuri. Kwa kawaida, huenda chini kiasi cha sentimita ishirini (20 sm), na hujitawanya kwa kiasi cha sentimita sabini na tano (75sm).
  Shina: Shina la mmea wa kabichi huwa na rangi ya kijani au zambarau. Hii hutegemeana na aina ya kabichi, na kwa kawaida ni fupi.
  Hali ya hewa: Kabichi hustawi vyema katika sehemu yenye hali ya baridi, hali ya joto jingi haifai kwa kabichi kwa kuwa huathiri uotaji na ukuaji wake. Joto jingi pia husababisha kulegea kwa vichwa vilivyofunga. Zao hili hustawi vema katika maeneo yenye mwinuko wa zaidi ya mita 100 toka usawa wa bahari.
  Udongo: Zao hili linaweza kustawishwa kwenye udongo wa aina yoyote mradi tu udongo huo usiwe na chumvichumvi nyingi na usiotuhamisha maji. Udongo wa kichanga na ule usio na rutuba ya kutosha husababisha kabichi kukomaa upesi na kuzaa kabichi hafifu zenye vichwa vidogo.
  Kitalu: Kitalu ni muhimu katika uzalishji wa zao hili. Ni vema kutengeneza matuta yenye upana wa mita moja, na urefu wowote kulingana na matakwa ya mkulima.
  Mbolea za samadi na zenye asili ya chokaa zichanganywe vizuri kwenye udongo. Kiasi cha gramu 500 za mbegu huhitajika kwa hekta moja.  Katika upandaji kwenye kitalu ni vizuri kutengeneza mistari katika tuta, umbali toka mstari hadi mstari uwe sentimita ishirini (20). Udongo kiasi kidogo utumike katika kufunika mbegu.
  Baada ya mbegu kuota ni vizuri kupunguza baadhi ya miche na uwe katika kipimo cha sentimita 2-3 toka mche hadi mche.
  Hii itasaidia kuwa na miche mifupi na yenye nguvu. Inafaa kunyeshea kitalu mara moja au mbili kwa siku na katika sehemu za joto ni vizuri kuweka kivuli katika matuta. Katika wiki ya tatu, hadi wiki ya nne, ni vyema kuondoa kivuli kidogo kidogo huku ukipunguza unyeshaji. Hali hii itasaidia miche isipate mshtuko wa uhamishaji shambani.
  Kuhamisha na kupanda
  Hamisha na kupandikiza miche shambani ikiwa na umri wa wiki nne, wakati huo miche ikiwa na majani manne ya mwanzoni na urefu wa kiasi cha sentimita kumi na mbili (12). Wakati wa upandaji, ni vizuri udongo ukashindiliwa kwenye kila mche. Inafaa upandaji ufanyike mara moja, na ni vizuri ukafanyika nyakati za jioni au asubuhi sana, na udongo uwe na unyevu wakati wote.
  Nafasi kati ya mmea
  Katika mstari hadi mstari inatakiwa iwe sentimita 60-75. Kutoka mmea hadi mmea ni sentimita 30-60. Pia sentimita 75-90 inaweza kutumika kati ya mstari na mstari.
  Mbolea: Ni vizuri kuweka kiasi cha viganja 2-3 vya mbolea ya samadi iliyooza vizuri katika kila shimo.
  Palizi: Wakati wa palizi ni vizuri mkulima akawa mwangalifu ili asiharibu mizizi. Wakati kabichi inapoanza kufunga hufunika ardhi, hivyo, husaidia kuzuia magugu yasiote, kwa wakati huu hakuna haja ya kupalilia.
  Kuvuna: Kabichi hukomaa katika kipindi cha siku 60-100 tangu kupandwa. Kwa ajili ya kuuza ni vizuri kuvuna wakati vichwa vinapofunga vizuri na huwa na uzito wa kutosha kabichi iangaliwe na kutunzwa baada ya kuvunwa ili isikwaruzwe na kuoza kabla ya kutumiwa. Kwa kawaida hekta moja hutoa mavuno kiasi cha tani 50-80.
  Aina za kabichi
  Kuna aina nyingi za kabichi na zifuatazo ni miongoni mwa aina hizo:
   Early Jersey wakefield – Aina hii hukomaa katika kipindi cha miezi 3.5
  Early Jersey wakefield – Aina hii hukomaa katika kipindi cha miezi 3.5

   Sugar loaf – Aina hii hukomaa mapema sana, kiasi cha miezi 2.5
  Sugar loaf – Aina hii hukomaa mapema sana, kiasi cha miezi 2.5

  Glory of enkhuizen – Aina hii hukomaa katika kipindi cha miezi 3.5
  Glory of enkhuizen – Aina hii hukomaa katika kipindi cha miezi 3.5

  Prize drumhead – Aina hii hukomaa katika kipindi cha miezi 3.5
  Prize drumhead – Aina hii hukomaa katika kipindi cha miezi 3.5

   F1-High Breed – Aina hii hukomaa katika kipindi cha miezi 2-4
  F1-High Breed – Aina hii hukomaa katika kipindi cha miezi 2-4

  Duncan – Aina hii hukomaa katika kipindi cha miezi 3
  Duncan – Aina hii hukomaa katika kipindi cha miezi 3


 3. KILIMO BORA CHA NYANYA
  KILIMO BORA CHA NYANYA : Nyanya ni zao la mboga ambalo hulimwa sehemu nyingi duniani kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na pia kama zao la biashara. Inahisiwa kuwa asili ya nyanya ni nchi ya Peru/Equador huko Amerika ya Kusini. Mmea huu ulianza kuzalishwa kama zao katika nchi ya Mexico na baadaye kusambaa katika nchi nyingine za ulimwengu.
  matandazo kwa ajili ya nyanya
  matandazo kwa ajili ya nyanya
  Uzalishaji wa nyanya duniani na hapa Tanzania
  Nchi zinazolima nyanya kwa wingi duniani ni pamoja na USA, Italia na Mexico. Kwa upande wa Africa nchi zinazo lima ni kama; Malawi, Zambia na Botswana. Zao hili hulimwa pia katika nchi za Africa Mashariki, ikiwemo Kenya, uganda na Tanzania.
  Zao la nyanya linalimwa karibu maeneo yote ya Tanzania. Uzalishaji wa nyanya ni mkubwa kuliko mazao mengine ya mbogamboga yanayolimwa hapa Tanzania, uzalishaji wa nyanya kwa mwaka ni jumla ya tani 129,578 ikiwakilisha asalimia 51 ya mazao yote ya mboga. Kwa mujibu wa Wizara ya kilimo ya Tanzania maeneo yanalolima sana nyanya ni pamoja na Mkoa wa Kilimanjaro (Hai, Moshi na Rombo), Arusha (Arumeru), Morogoro (Mgeta), Tanga (Lushoto), Mbeya (Mbeya vijijini) na Singida.
  Morogoro ndiyo inayoongoza kwa kilimo hichi ikiwa na wazalishaji wenye zaidi ya hekta 6,159 (ekari 15,398). Pamoja na kwamba eneo la uzalishaji linaongezeka kwenye maeneo mengi lakini uzalishaji wa nyanya bado ni mdogo sana.
  Uzalishaji mdogo unasababishwa na kupungua kwa rutuba ya ardhi, upepo, joto, ukame. Sababu nyingine ni pamoja na ukosefu wa aina za nyanya zenye mavuno mengi amabazo zinahimili mazingira ya kwetu, wadudu, magonjwa na magugu.
  UDONGO KWA AJILI YA NYANYA
  UDONGO KWA AJILI YA NYANYA
  Mazingira
  • Hali ya Hewa:
   Nyanya hustawi vizuri zaidi kwenye mazingira ya joto la wastani kuanzia nyuzi joto 18-27 sentigreti. Mvua nyingi husababisha mlipuko wa magonjwa ya ukungu kama vile Baka jani chelewa n.k.) • Udongo:
   Nyanya hustawi kwenye aina zote za udongo kuanzia udongo wa kichanga, mweupe wa tifutifu hadi udongo wa mfinyanzi, ili mradi uwe na mboji ya kutosha na usiosimamisha/tuamisha maji. Pia uwe na uchachu wa wastani yaani pH 6.0 – 7.0.
  AINA ZA NYANYA

  Aina za Nyanya
  Kutokana na tabia ya ukuaji, nyanya zinagawanyika katika makundi mawili:
  1. Aina ndefu ( intermediate) kwa mfano ANNA F1, Tebgeru 97. Aina hizi hufanya vizuri zaidi zinapopandwa ndani ya greenhouse. Uvunaji wake ni wa muda mrefu, zipo ambazo zinavunwa hata zaidi ya miezi 6, yaani hiyo miezi 6 ni ya uvunaji.
  2. Aina fupi (determinate) kwa mfano Tanya, Cal J, Mwanga, Onyx, Roma VF (nyanya mshumaa)
  Kotokana na uchavushaji, nyanya zinagawanyika makundi mawaili:
  1. OPV (Open Pollinated Variety) – Aina za kawaida
  2. Hybrid – Chotara: Hizi ni aina zenye mavuno mengi, kati ya hizo zipo aina fupi na ndefu.
  Katika karne hii ya 21, nyanya zinazopendelewa kulimwa zaidi na wakulima, ni zile zinazoweza kuvumilia magonjwa, zinazo zaa sana, na zenye ganda gumu ili kufanikisha usafirishaji, na kuhifadhika kwa siku nyingi bila kuharibika mapema.

  Kuandaa Kitalu cha Nyanya

  Mambo muhimu ya kuzingatia:
  • Kitalu kiwe karibu na maji ya kutosha na ya kudumu
  • Kiwe sehemu iliyowazi na yenye udongo ulio na rutuba ya kutosha
  • Eneo la kitalu kama ni kubwa liwe tambarare au na mwiinuko kidogo ili kuepuka maji yasituame kwenye kitalu, mtelemko ukiwa mkali sana nao sio mzuri kwani husababisha mmomonyoko wa udongo.
  • Kitalu kiwe sehemu ambayo haikuwa na zao la nyanya au viazi mviringo (au mazao ya jamii ya nyanya k.m. mnavu, biringanya n.k.)
  • Kiwe sehemu ambayo ni rahisi kupata huduma zote muhimu kwa urahisi, ikiwa ni pamoja na uhamishaji wa miche kwenda sehemu nyingine. Pia kurahisisha usambazaji wa miche kwenda sehemu nyingine.
  Kuandaa Matuta ya Kusia Mbegu za Nyanya
  Kuandaa Matuta ya Kusia Mbegu za Nyanya
  Kuandaa Matuta ya Kusia Mbegu za Nyanya

  Aina ya matuta:

  • matuta ya makingo (sunken seed bed)
  • matuta ya kunyanyulia udongo (raised seed bed)
  • matuta ya kawaida (flat seed beds)
  Mambo Muhimu ya Kuzingatia wakati wa Kuandaa Matuta
  • Tuta liwe na upana kati ya sentimita 90-120, na urefu wowote, [ili mradi muhudumu anaweza kutoa huduma nyingine zote kitaluni bila kukanyaga miche].
  • Kwatua/lima kina kirefu cha kutosha kiasi cha sentimita 15-20 ili mizizi iweze kusambaa vizuri ardhini.
  • Choma takataka juu ya kitalu, au funika tuta kwa nailoni, majuma 4-8 ili kuua vimelea vya magonjwa na wadudu.
  • Wakati wa kuandaa, kitalu, ongeza mbolea aina ya samadi/vunde au mboji kwenye udongo kisha kwatua ili ichanganyike vizuri na udongo.
  • Changanya kiasi cha debe 1 hadi 2 kila baada ya mita moja (hatua moja) mraba.
  • Tuta lisiwe na mabonde mabonde au mawe mawe ambayo yanaweza kuzuia usambaaji mzuri wa mbegu kwenye tuta, lisawazishwe vizuri ili kuhakikisha usambazaji mzuri wa mbegu na kuepuka mbegu kufukiwa chini mno kiasi ambacho hazitaota.

  Faida na Hasara za Matuta yaliyotajwa hapo juu


  1. Matuta ya kunyanyulia udongo (raised seed beds);

  • matuta ya namna hii huruhusu maji, hewa na mizizi kupenya kwenye udongo kwa urahisi zaidi.
  • Mazao ya mizizi hupata nafasi ya kutosha kutanuka haraka zaidi
  • Matuta haya hayatuamishi maji kama mengine, hivyo hutumika zaidi kwenye maeneo yanayokuwa na mvua mara kwa mara.

  Hasara:

  o Matuta ya namna hii yana sababisha sana mmomonyoko wa udongo kama hayakutengenezwa vizuri.

  2. Matuta ya makingo (sunken seed beds):

  Faida:
  • matuta haya ni rahisi kutengeneza
  • hutumika wakati wa kiangazi ili kuhifadhi maji na unyevu
  • nyevu mdogo unaopatikana ardhini
  • ni rahisi kumwagilia kwa kutumia maji ya mfereji au bomba
  • huhifadhi unyevu nyevu kwenye ardhi kwa muda mrefu
  • huzuia mmomonyoka wa ardhi

  Hasara:

  • Matuta ya aina hii hayawezi kutumika kwenye maeneo yenye
  • mvua nyingi.
  1. Matuta ya kawaida (flat seed beds):

   Faida:
  • ni rahisi sana kutengeneza kwani udongo ukisha kwatuliwa
  • na kusambazwa mbegu huoteshwa
  • ni rahisi kutumia eneo kubwa kuotesha mbegu

  Hasara:
  Matuta ya aina hii hayawezi kutumika kwenye maeneo yenye mvua nyingi.
  Kusia Mbegu
  • Hakikisha ubora na uotaji wa mbegu kabla ya kuzipanda kitaluni (germination test)
  • Weka mistari kwenye tuta kulingana na ukubwa wa tuta, lakini mistari isiwe chini au zaidi ya sentimita 15-20 toka mstari hadi mstari
  • Kina cha mistari kisiwe cha kutisha bali kiwe kati ya sentimita 1-2
  • Matuta yapate maji ya kutosha siku moja kabla ya kusia mbegu. Ni vizuri kutumia chombo cha kumwagilia (watering can).
  • Mbegu ziatikwe kwenye mistari na zisambazwe vizuri ili kufanikisha usambaaji mzuri wa mbegu kwenye tuta. Changanya mchanga laini na mbegu kisha sambaza kwenye mistari iliyoandaliwa kwenye tuta.
  Mbegu zinaweza pia kuatikwa kwenye tuta bila mistari, lakini zisambazwe kwa uwiano mzuri kwenye tuta ili kupunguza msongamano. Msongamano husabisha magonjwa ya fangasi kama vile kinyausi (damping off) au ukungu (blight).
  • Weka matandazo kiasi cha kutosha ambacho hakitazuia kuota kwa mbegu.
  • Mara baada ya kuatika mbegu, mwagilia maji kiasi cha kutosha kulingana na unyevu nyevu ulioko ardhini

  Mambo ya Kuzingatia baada ya kusia mbegu pamoja na Matunzo Kitaluni

  • Mwagilia maji kwenye kitalu baada ya kuotesha kulingana na unyevu nyevu uliopo kwenye udongo.
  • Miche yote ikisha ota, ondoa matandazo, kisha weka chanja ili kupunguza mionzi ya jua ambayo inaweza kuunguza miche michanga. (kipindi cha baridi si muhimu sana)
  • Punguzia miche (thinning) ili ibakie kwenye nafasi ya kutosha. Hivyo miche ibakie kwenye umbali wa sentimita 2.5 – 4. Hii itapunguza magonjwa ya ulemavu na mnyauko, pia itasaidia kupata miche bora na yenye nguvu.
  • Endelea kumwagilia hadi miche ifikie kimo kinachofaa kuhamishia shambani.
  • Punguza kiwango cha umwagiliaji maji, siku chache kabla ya kuhamishia miche shambani, yaani siku 7-10.
  Kanuni na Mbinu za kuhamisha miche toka Kitaluni kwenda shambani (Transplanting
  Rules)
  • Mwagilia miche masaa machache kabla ya kuhamishia miche shambani ili wakati wa kung’oa miche mizizi ishikamane vizuri na udongo.
  • Kabla ya kuhamisha miche, mashimo yawe yamekwisha andaliwa katika nafasi zinazo stahili huko shambani.
  • Miche ihamishwe wakati wa jioni ili kuepuka madhara yanayoweza kusababishwa na jua.
  • Kwa ujumla karibu mazao yote ya mboga mboga huwa tayari kuhamishiwa shambani yakiwa na majani kamili kati ya 2-6 pamoja na mizizi mingi iliyostawi vizuri.
  • Mche lazima uwe na afya nzuri, uwe umenyooka vizuri, hivyo miche yote iliyonyongea au myembamba kupita kiasi isichukuliwe wakati wa kupeleka shambani.
  • Ng’oa miche kwa uangalifu hasa pamoja na udongo wake kwa kutumia vifaa husika ili mizizi isidhurike.
  • Miche ihamishiwe shambani mapema mara baada ya kung’olewa toka kitaluni.
  • Wakati wa kuhamisha miche, uangalifu mkubwa utumike ili kutoharibu miche/mizizi.
  Maandalizi ya Shamba la Nyanya
  • Shamba la nyanya liandaliwe mwezi 1-2 kabla ya kupanda miche.
  • Mara baada ya kulima choma nyasi juu ya udongo au ondoa magugu yote yanayoweza kuhifadhi wadudu na magonjwa ya nyanya.
  • Siku moja au mbili kabla ya kuhamishia nyanya shambani, mwagilia sehemu iliyoandaliwa kwa ajili ya kuhamishia nyanya.
  • Nafasi kati ya mche hadi mche ni wastani wa sentimita (50-60) x (50-75) kutegemeana na aina au hali ya hewa. Kama ni kipindi cha baridi ni vyema nyanya zikapandwa mbalimbali ili kuruhusu mzungungo wa hewa na kuzuia magonjwa ya fangasi.
  Jinsi ya kupanda miche:
  • Hamisha miche toka kitaluni pamoja na udongo wake
  • Sambaza mizizi vizuri kwenye shimo bila kukunja.
  • Fukia miche kina kile kile ambacho shina lilikuwa limefukiwa bustanini.
  • Mwagilia maji ya kutosha kulingana na unyevunyevu uliopo kwenye udongo kasha weka matandazo na kivuli ili kupunguza uharibifu unaosababishwa na mionzi ya jua.

  Mambo muhimu ya kuzingatia baada ya kuhamishia Miche Shambani

  • Kagua shamba mara kwa mara ili kujua maendeleo au matatizo yaliyoko shambani mapema
  • Hakikisha shamba ni safi wakati wote, palilia shamba na hakikisha magugu yote hasa yale ya jamii ya nyanya yamelimiwa chini.
  • Ondoa mimea iliyoshambuliwa na magonjwa au ondoa sehemu zilizoshambuliwa, kisha zifukiwe chini au kuunguza moto.
  • Punguza matawi na vikonyo ili kuongeza mwanga wa kutosha kwenye nyanya pamoja na kuruhusu mzunguko wa kutosha wa upepo na kusababisha mazingira magumu ya wadudu maadui kwenye nyanya, hasa wale wanaopenda kiza na magonjwa yanayopendelea unyevunyevu.
  Asante sana:


 4. TEKNOLOJIA YA KILIMO CHA GREENHOUSE
  TEKNOLOJIA YA KILIMO CHA GREENHOUSE: Kwanza tuanze kwa kupata tafsiri ya neno lenyewe, Greenhouse imekua ikipatiwa majina tofauti tofauti, wapo watu wanaiita Nyumba ya Kijani, wengine wanaiita Banda Kitalu n.k Vyovyote utakavyopenda kuiita teknolojia hii, cha muhimu ni kuelewa nini hasa maana yake.
  Greenhouse (Banda Kitalu):  ni teknolojia ya kuipatia mimea mazingira mazuri ambayo yataisaidia mimea/mazao kumea vizuri na kua na uzao mkubwa, mimea hii inapandwa kwenye banda, au nyumba maalumu. Teknolojia hii inatumika hasa kuikinga mimea usiathiriwe na mazingira haribifu ya hali ya hewa.
  Mazingira haribifu ni kama upepo mkali, baridi kali, mvua kubwa, au mvua za mawe, mionzi mikali ya jua, joto kali , wadudu pamoja na magonjwa. Hayo ndio mazingira ambayo teknolojia hii inaleta suluhisho, kuhakikisha mimea inastawi vizuri bila ya kuathiriwa na moja ya matatizo hayo yaliyotajwa.
  Teknolojia hii ilivumbuliwa huko kwenye nchi baridi, zaidi ya karne moja na nusu (miaka 150) iliyopita. Nchi zilizopo ukanda wa baridi, mazao ya kitropiki (mazao yanayo pendelea joto) ilikua haiwezekani kabisa kulimwa maeneo hayo ya ukanda wa baridi. Ndipo hapo wazo la kuvumbua Greenhouse lilipoibuka.
  Nchi hizi walianza kutumia teknolojia hii maana nyumba hii ya kijani ilikua ina uwezo wa kutunza joto, na hivyo wakaanza kulima mazao ya ukanda wa joto kama mbogamboga (nyanya, hoho) na matunda. Pamoja na teknolojia hii kuanza kitambo kidogo katika nchi zilizoendelea, lakini kwa upande wa nchi zinazoendelea bado teknolojia hii ni mpya kwa watu wengi.  Teknolojia hii pia inatumika katika nchi za joto, japo kuna utofauti  kati yake na  zile za nchi za ukanda wa baridi
  Nchi hizi walianza kutumia teknolojia hii maana nyumba hii ya kijani ilikua ina uwezo wa kutunza joto, na hivyo wakaanza kulima mazao ya ukanda wa joto kama mbogamboga (nyanya, hoho) na matunda. Pamoja na teknolojia hii kuanza kitambo kidogo katika nchi zilizoendelea, lakini kwa upande wa nchi zinazoendelea bado teknolojia hii ni mpya kwa watu wengi.  Teknolojia hii pia inatumika katika nchi za joto, japo kuna utofauti  kati yake na  zile za nchi za ukanda wa baridi.
  GREENHOUSE
  Faida za Greenhouse
  • Mavuno yanakua mara 10 hadi 12 zaidi ya kilimo cha eneo la wazi, ikitegemea aina ya mazao yanayolimwa humo, aina greenhouse pamoja na vifaa vya kudhibiti mazingira ya ndani ya greenhouse.
  • Uhakika wa kuvuna mazao unaongezeka. Maana Greenhouse inaweza kuzuia visababishi vya  uharibifu wa mazao.
  • Uzalishaji wa mazao katika kipindi chote cha  mwaka, maana huhitaji kusubiri mpaka msimu wa zao ufike ndio ulime.
  • Uwezo wa kupata soko zuri la mazao. Greenhouse itakuwezesha kuzalisha kipindi ambacho sio cha msimu (off- season) kwa vile kipindi hiki watu wengi hawazalishi kutokana na mazingira kutoruhusu,  ukiwa na greenhouse una uwezo wa kuzalisha kipindi hicho na ukapata bei nzuri
  • Ufanisi katika utumaji wa dawa, viwatilifu katika kudhibiti.
  • Matumizi ya maji ni madogo sana na udhibiti  wake  ni rahisi. Miundombinu ya umwagiliaji inayotumika hapa ni umwagiliaji wa matone (drip irrigation) ambapo maji yanakwenda pale penye mmea pekee.
  • Uwezo wa kutunza mimea inayozalishwa maabara kutokana na teknolojia ya tishu (tissue culture technology) mimea inapotoka maabara kabla haijapelekwa shambani inatunzwa kwanza kwenye greenhouse maalumu kwa ajili  ya kuzoea mazingira ya nje kwanza.
  • Uwezo wa kupanda mimea bila kutumia udongo (soilless culture).  Kutokana na changamoto ya magonjwa na vijidudu vya kwenye udongo kama Nematodes, ndipo uvumbuzi  wa teknolojia ya kupanda mimea kwa kutokutumia udongo ulipotokea
  KILIMO NDANI YA GREENHOUSE
  Baadhi ya Nchi zinazofanya vizuri kilimo cha  Greenhouse.
  Kuna nchi zaidi ya 50 katika dunia ambapo kilimo kinalimwa kwenye greenhouse. Tutaangalia baadhi ya nchi ambazo zimekua zikifanya vizuri kupitia teknolojia hii. Tuanze na Marekani, Marekani ina eneo takribani 4000 hekta ambazo zina greenhouse kwa ajili ya kilimo cha maua,
  Marekani kupitia kilimo hicho wanapata pato la zaidi ya Dola bilioni 2.8 (zaidi ya trilioni 5 hela za Tz) kwa mwaka. Nchini Hispania inakadiriwa zaidi 25,000hekta na Italia ni hekta 18,500, zimefungwa  greenhouse kwa kilimo cha pilipili hoho, strawberry, matango, maharagwe machanga,  pamoja na nyanya.
  Canada greenhouse ni kwa kilimo cha maua na mboga mboga wakati ambapo hazilimwi kwingine. Mazao maarufu  yanayolimwa kwenye Greenhouse za Canada kama nyanya, matango na hoho.
  Uholanzi ni zaidi ya hecta 89,600 zipo nchini ya greenhouse.
  Uholanzi sekta ya greenhouse ndio iliyo bora zaidi duniani. Uholanzi ndio nchi inayoongoza kwa teknolojia hii na wamepiga hatua mbali sana. Yapo makampuni makubwa ya Kiholanzi yanayotumia teknolojia hii baadhi yao yapo hapa Tanzania katika kilimo cha maua, matunda, mbogamboga, pamoja na mbegu. Mfano : Kili Hortex, Multi flower, Mount Meru Flower, Enza Zaden, RJK ZWAAN (Q-SEM na AFRISEM)
  Israel: 15000 hekta. Israel ndiyo nchi inayoongoza kwa kuuza maua (cut flowers) nje ya nchi. Japokuwa nchi ya Israel eneo lake kubwa ni jangwa. Pia Nchi ya Israel imekua moja ya nchi zilizopo mstari wa mbele katika teknolojia ya umwagiliaji na Greenhouse.
  Balton Tanzania yenye makao yake makuu mjini Arusha, ni moja ya kampuni toka Israel zinazofanya vizuri katika sekta hii.
  Uturuki: hekta 10,000 zinalimwa maua na mbogamboga kwa kutumia teknolojia hii ya Green house. Saudi Arabia: 90% ya mazao ya yanya na tango yanalimwa kwenye green house.
  Misri 10,000 hekta nyanya, matango na pilipili hoho. Teknolojia ya Greenhouse nchini China inakua kwa kasi sana kuliko nchi yeyote   Japokuwa teknolojia hii haijaanza muda mrefu kivile huko China lakini mpaka sasa zaidi ya hekta 48,000 tayari zimefungwa Greenhouse.  Nchi nyingine zinzofanya vizuri barani Asia ni kama  Japan (40,000hekta) na Korea kusini (21,000 hekta).
  MUUNDO WA GREENHOUSE
  Aina za Greenhouse.
  Greenhouse zinagawanyika makundi mbalimbali kutegemeana na vigezo vifuatavyo:
  Aina za Greenhouse kwa  kigezo cha sura/umbile (shape)
  Zipo aina aina 8 za greenhouse, hapa nitataja chache tu kwa majina yake ya kitaalamu
  • Quonset Greenhouse
  • Saw tooth type
  • Even span type greenhouse
  • Uneven span type greenhouse
  MFANO WA GREENHOUSE
  Aina za Greenhouse kwa kigezo cha Matumizi
  • Green house zinazoongeza joto (Hizi ni kwa maeneo ya baridi)
  • Greenhouse zinazopunguza joto (hizi ni kwa maeneo ya joto)
  Aina za greenhouse kwa kigezo cha matengenezo yake (construction)
  • Greenhouse za miti (Wooden framed structure)
  • Pipe framed structure (Greenhouse zinazotumia mabomba)
  • Truss/Aluminium framed structure ( Geenhouse zinazojengwa kwa vyuma)
  Aina za Greenhouse kwa kigezo  cha aina ya zana za ufunikaji (covering types)
  • Greenhouse zinazofunikwa kwa zana za Vioo (Glass Greenhouse or Screenhouse) )- hizi zinatumika sana maeneo ya baridi kali, ili kutunza joto kwa muda mrefu ndani   greenhouse
  • Greenhouse zinazofunikwa kwa mifuko ya plaski (plastic film)
  KILIMO NDANI YA GREENHOUSE
  Aina ya Greenhouse kwa kigezo cha uwekezaji unaofanywa:
  • Greenhouse za gharama kubwa (High cost greenhouse) ( Zaidi ya milioni 50)
  • Greenhouse za gharama za kati (medium cost greenhouse) (milioni 20 hadi 50)
  • Greenhouse za gharama ndogo (Low cost greenhouse) (chini ya milioni 20)
  • Greenhouse za gharama ndogo ndio watu wengi wanazitumia sana katika nchi zinazoendelea.
  0

  Add a comment

 5. YAFAHAMU MAKUNDI MAWILI YA MBEGU ZA MPUGA
  YAFAHAMU MAKUNDI MAWILI YA MBEGU ZA MPUNGA
  YAFAHAMU MAKUNDI MAWILI YA MBEGU ZA MPUGA: Je umekuwa ukijihoji ni vipi utapata mbegu bora za mpunga? Kama jibu ni ndiyo basi makala haya yanakuhusu sana wewe kwani lengo letu ni kuona wewe unafanikiwa sana kataika kilimo.
  Watu wengi wemekuwa hawafahamu ni mbegu ipi ambayo inafaa katika upandaji, na kosa hilo ambalo wanalifanya limekuwa likisababisha mazao nkupatikana kwa uchache zaidi, ila mukweli ni kwamba Matumizi ya mbegu bora ni muhimu katika upatikanaji wa mavuno mengi na bora. Hivo ili kuhakikisha unapata mazao mengi Kuna makundi mawili makuu ya mbegu ambayo ni:
  1. Mbegu za asili za mpunga
  Ni zile ambazo zimetumika miaka mingi katika historia ya kilimo. Kuna aina nyingi za mipunga ya asili inayolimwa sehemu mbalimbali hapa nchini kama Supa, Kahogo, Kula na Bwana, Shingo ya mwali, n.k. Wakulima wanazipenda mbegu hizi kutokana na kuwa na sifa kama vile ladha nzuri, uvumilivu wa matatizo mbalimbali ya kimazingira na kwa sababu ya uwezo wa mbegu hizi kustahimili katika hali mbaya ya hewa na hazihitaji uangalizi wa hali ya juu.
  Sifa hizi ni matokeo ya mbegu hizi kumudu mazingira na uchaguzi wa mbegu uliofanywa na wakulima kwa miaka mingi. Hata hivyo, nyingi ya mbegu hizi zina uwezo mdogo wa kuzaa, zinachelewa kukomaa, ni ndefu na rahisi kuanguka.
  2. Mbegu zilizoboreshwa:
  Hizi ni zile zilizoboreshwa kutokana na mbegu za asili. Mfano wa mbegu zilizoboreshwa ni kama vile Katrin, IR54, na IR64. Zinazaa sana hasa kwa kilimo cha umwagiliaji. Hata hivyo, hazikidhi ladha ya walaji na ukobolekaji wake si mzuri na baadhi hazistahimili kwenye mazingira mengi ya kawaida. Hii imezifanya mbegu hizi kukubalika na wakulima kwa kiwango kidogo sana.
  Mbegu bora nyingine zilizozalishwa kutoka utafiti na kuonekana kupendwa kwa ajili ya mavuno mengi na ladha nzuri kama TXD88 na TXD85. Hivi karibuni imetolewa mbegu nyingine iitwayo TXD306 (SARO5), mbegu hii hupendwa na wakulima, wafanyabiashara na walaji kutokana na sifa yake ya mavuno mengi, punje ndefu kiasi na nzito, ladha nzuri na yenye kunukia pindi ipikwapo na kuliwa.
  Hayo ndiyo makundi ya mbegu bora ya mpunga ambayo yatakusaidia kuweza kukua katika kilimo.
  0

  Add a comment

 6. UFUGAJI BORA WA NG’OMBE
  UFUGAJI BORA WA NG’OMBE
  UFUGAJI BORA WA NG’OMBE : Ng’ombe wanafugwa kwa ajili ya nyama na maziwa lakini pia hutoa mazao mengine kama ngozi,mbolea na hutumika kama wangyama kazi.  Zaidi ya asilimia95 ya ng,ombe na hutumika kama wanyama kazi.  Zaidi ya asilimia 95 ya ng’ombe wanaofugwa hapa nchini ni wa asili ambao huzalisha nyama na maziwa kwa kiwango kidogo ikilinganishwa na wale wachache walioboreshwa.  Ng’ombe walioboreshwa wamegawanyika katika makundi mawili, wale wanaofugwa kwa ajili ya nyama na wanaofugwa kwa ajili ya maziwa.
  Ili kuwawezesha ng’ombe kuzalisha mazao bora ya nyama, maziwa na ngozi mfugaji anapaswa kufuata kanuni za ufugaji bora ambazo ni pamoja na:-
  1. Kufuga ng’ombe katika eneo kwa kuzingatia uwianao wa idadi ya ng’ombe na malisho katika mfumo wa ufugaji huria.
  2. Kujenga banda au zizi bora.
  3. Kuchagua koo/aina ya ng’ombe kulingana na uzalishaji (nyama au maziwa).
  4. Kutunza makundi  mbalimbali ya ng’ombe kulinga na umri na hatua ya uzalishaji.
  5. Kumpa ng’ombe lishe sahihi kulingana na umri na mahitaji ya mwili.
  6. Kudhibiti magonjwa ya ng’ombe kama inavyoshauriwa na mtaalamu wa mifguo.
  7. Kuvuna mifugo katika umri na uzito muafaka kulingana na mahitaji ya soko.
  8. Kuzalisha maziwa, nyama na ngozi zinazokidhi viwango vya ubora na usalama.
  9. Kutunza kumbukumbu za uzalishaji na matukio muhimu ya ufugaji.
  MIFUMO YA UFUGAJI
  Ng’ombe wanaweza kufugwa katika mfumo wa ufugaji huria au kulishwa katika banda (ufugaji shadidi).  Ufugaji huria huhitaji eneo kubwa la ardhi yenye malisho mazuri na vyanzo vya maji.  Pamoja na kuwa na ufugaji huu, ni muhimu ardhi hiyo itunzwe kwa kuzingatia uwiano wa idadi ya ng’ombe na malisho.  Ufugaji wa shadidi uzingatie uwepo wa banda bora na lishe sahihi.
  UFUGAJI KATIKA MFUMO HURIA
  Ili mfugaji aweze kupata mazao mengi na bora katika ufugaji huria anapaswa kuzingatia yafuatayo:-
  • Atenge eneo la kutosha la kufugia kulingana na idadi ya ng’ombe alionao.
  • Atunze malisho ili yawe endelevu na yapatikana wakati wote.
  • Awe na eneo lenye maji ya kutosha na
  • Atenganishe madume na majike ili kuzuia ng’ombe kuzaa bila mpangilio.
  Matunzo mengine ya ng’ombe yazingatie vigezo vingine muhimu kama umri hatua ya uzalishaji na matumizi ya ng’ombe husika.
  BANDA/ZIZI BORA LA NG’OMBE BANDA BORA.
  Band alijengwe sehemu ya mwinuko mbali kidogo na makazi ya watu na liwe na sifa zifuatazo:-
  • Uwezo wa kumkinga ng’ombe dhidi ya mvua, upepo, jua kali na baridi.
  • Kuta imara zenye matunda au madirisha kwa ajili ya kuingiza hewa na mwanga wa kutosha,
  • Sakafu yenye mwinuko upande mmoja ili isiruhusu maji na uchafu kutuama.
  • Lijengwe katika hali ya kuruhusu kufanyiwa usafi kwa urahisi kila siku, na sakafu ngumu ya zege au udongo ulioshindiliwa na kuweka malalo.
  • Paa lisilovuja na
  • Aidha kwa wafugaji wanaofuga katika ufugaji huria ambako mazizi hutumika, inashauriwa  kuzingatia yafuatayo:-
  • Zizi likae mahali pa mwinuko pasiporuhusu maji kutuama.
  • Zizi liweze kukinga mifugo dhidi ya wezi na wanyama hatari.
  • Ukubwa wa zizi uzingatie idadi na umri wa mifugo ng’ombe watengwe kulingana na umri wao.
  • Zizi lifanyiwe usafi  mara kwa mara na
  • Liwe na sehemu ya kukamulia (kwa ng’ombe wa maziwa), stoo ya vyakula, sehemu ya kutolea huduma za kinga na tiba, eneo la kulishia na maji ya kunywa.
  ZIZI BORA
  Zizi lijengwe sehemu ya mwinuko isiyoruhusu maji kutuama mbali kidogo na makazi ya watu na liwe na sifa zifuatazo:-
  • Liweze kuhakikisha usalama wa ng’ombe.
  • Ukubwa wa zizi uzingatie idadi ya mifugo.
  • Liwe na sakafu ya udongo ulioshindiliwa vizuri na kufanyiwa usafi  mara kwa mara
  • Zizi la ndama liwe na paa ma
  • Lijengwe kwa vifaa madhubuti na visivyoharibu ngozi.
  UCHAGUZI WA KOO NA AINA YA NG’OMBE WA KUFUGA
  Kwa ufugaji wenye tija, mfugaji anashauriwa kuchagua koo na aina ya ng’ombe kwa kuzingatia malengo ya ufugaji (nyama au maziwa).
  NG’OMBE WA NYAMA
  Ng’ombe wanaofaa kufugwa kwa ajili ya uzalishaji nyama ni wale wanaokua kwa haraka na kuweka misuli mikubwa iliyojengeka vizuri.  Baadhi ya koo zenye sifa hizo ni pamoja na Boran, Mpwapwa (nyama na maziwa), Charolais, Aberdeen Angus, pamoja na chotara wao.  Hata hivyo, nchini Tanzania ng’ombe aina ya Zebu (mfano Ufipa,Gofo, Masai, Sukuma, Tarime, Iringa red), Sanga (Ankole) na chotara wao ndio hutumika kama ng’ombe.
  NG’OMBE WA MAZIWA.
  Sifa za ng’ombe wa maziwa zifuatazo:-
  • Umbo lililopanuka kwa nyuma na kupungua kuelekea kichwani.
  • Mgongo ulionyooka kuanzia mabegani kuelekea mkiani
  • Miguu ya nyuma mirefu iliyonyooka, minene yenye kuacha nafasi kwa ajili ya kiwele na kwato imara.
  • Kiwele kiwe kikubwa chenye chuchu nne, ndefu na unene wa wastani
  • Nafasi kati ya chuchu na chuchu iwe ya kutosha na
  • Endapo ng’ombe anakamuliwa awe na kiwele kikubwa kilichoshikamana vizuri mwilini, na mishipa mikubwa kwenye kiwele iliyosambaa.
  Aina ya ng’ombe wa maziwa wanaofugwa kwa wingi nchini ni pamoja na Friesian, Ayrshire, jersey, Mpwapwa, Simmental na chotara watokanao na mchangoayiko wa aina hizo na Zebu.
  UTUNZAJI WA MAKUNDI MABALIMBALI YA NG’OMBE WA MAZIWA KULINGANA NA UMRI NA HATUA YA UZALISHAJI

  UTUNZAJI WA NDAMA

  Mfugaji anapaswa kutunza ndama vizuri kwa lengo la kupata ng’ombe wengi na bora kwa ajili ya maziwa.  Mambo muhimu ya kuzingatia katika utunzaji wa ndama tangu kuzaliwa hadi kuachishwa maziwa ni pamoja na Kuhakikisha kuwa ndama anapakwa dawa ya kuzuia maambukizi ya viini ya magonjwa kupitia kwenye kitovu, kwa mfano dawa joto (Tincute of Iodine) mara baada ya kuzaliwa na
  Ndama apatiwe maziwa ya awali yaani dang’a (colostrums) mara baada ya kuzaliwa kwa lengo la kupata kinga ya mwili dhidi ya magonjwa.  Aidha, aendelee kunyonya maziwa hayo kwa muda wa siku 3-4.
  Endapo jike aliyezaa amekufa au hatoi maziwa, apewe dang’a toka kwa ng’ombe mwingine kama yupo au dang’a mbadala, ambayo inaweza kutengenezwa kwa kuchanganya vitu vifuatavyo:-
  Lita moja ya maziwa yaliyokamuliwa wakati huohuo.
  • Lita moja ya maji yaliyochemshwa na kupozwa hadi kufikia joto la mwili.
  • Kijiko kimoja cha chai cha mafuta ya samaki (cod liver oili).
  • Mafuta ya nyonyo vijiko vya chai 3 na
  • Yai moja bichi
  Koroga mchanganyiko huo, weka katika chupa safi na ndama anyweshwe kabla haujaopoa.  Ndama anyweshwe mchanganyiko huo mara 2 kwa siku kwa muda wa siku 3 mfululizo na kila mara mchanganyiko uwe mpya.  Wakati wa kunywesha chupa iwekwe juu ya  kidogo ili asipaliwe.
  Endapo ndama hawezi kunyonya ng’o mbe akamuliwe na ndama anyweshwe maziwa kwa njia ya chupa kwa kuzingatia usafi wa maziwa na chupa.
  Ndama aendelee kunyweshwa maziwa kwa kiasi kama ilivyoonyeshwa kwenye Jedwali Na. 1
  Ndama aanze kuzoeshwa kula nyasi laini, pumba kidogo na maji safi wakti wote kuanzia wiki ya 2 baada ya kuzaliwa na Ndama aachishwe kunyonya au kupewa maziwa akiwa na umri wa miezi 3.  Mfugaji ahakikishe kwamba ndama anayeachishwa kunyonya ana afya nzuri.
  JEDWALI NA. 1 KIASI CHA MAZIWA NA CHAKULA MAALUMU KWA NDAMA
  UMRI (WIKI) KIASI CHA MAZIWA KWA SIKU (LITA) KIASI CHA CHAKULA MAALUM CHA NDAMA KWA SIKU (KILO)
  1 3.0 0.0
  2 3.5 0.0
  3 4.0 0.0
  4 4.5 0.0
  5 5.0 0.1
  6 5.0 0.2
  7 5.0 0.3
  8 4.0 0.4
  9 3.0 0.7
  10 2.0 1.0
  11 1.5 1.25
  12 – 16 0.75 1.5

  Vyombo vinavyotumika kulishia ndama visafishwe vizuri kwa maji yaliyochemshwa, sabuni na kukaushwa.

  Matunzo mengine ya ndani ni pamoja na:-
  • Kuondoa pembe kati ya siku 3 hadi 14 mara zinapojitokeza ili kuzuia wanyama kuumizana na kuharibu ngozi,
  • Kukata chuchu za ziada kwa ndama jike
  • Kuhasi ndama dume wasiozidi umri wa miezi 3 ambao hawatahitajika kwa ajili kuendeleza kizazi ili wakue hawatajika kwa ajili ya kuendelea kizazi ili wakue haraka na kuwa na nyama nzuri.
  • Kuweka alama au namba za utambulisho kati ya siku ya kwanza na ya tano, mfano kuvalishwa hereni kwenye masikio kwa ajili ya urahisi wa udhiti wa umiliki na utunzaji kumkukumbu na,
  • Kuwapatia kinga dhidi ya maabukizi na tiba ya magonjwa wanapougua.
  Huduma hizi zifanyike chini ya maelekezo ya mtaalam wa mifugo.
  UTUNZAJI WA NDAMA BAADA YA KUACHISHWA MAZIWA HADI KUPEVUKA (MIEZI – 18)
  Ndama baada ya kuachishwa maziwa apate malisho bora na chakula mchanganyiko kuanzia kilo 2 4 kwa siku kutegemea umri wake na Ndama wanapofikia umri wa miezi 18 wachaguliwe wanaofaa kuendeleza kizazi, wasio na sifa nzuri waondolewe katika kundi.

  UTUNZAJI WA MTAMBA
  Mtamba ni ng’ombe jike aliyefisha umri wa kupandwa (wastani wa miezi 18) hadi anapozaa kwa mara ya kwanza.  Ni muhimu kutunza vizuri mtamba ili kupata kundi bora la ng’ombe.  Miezi 3 kabla ya kupandishwa mtamba apatiwe:-
  • Malisho bora
  • Maji ya kutosha
  • Madini  mchanganyiko na
  Chakula cha ziada kiasi cha kilo 2 – 3 kwa siku, ili kuchochea upevukaji na kuongeza uzito wa mwili.

  UTUNZAJI WA NG’OMBE WAKUBWA
  Kundi hili linajumuisha ng’ombe wenye mimba, wanaokamuliwa na madume.  Mfugaji anapaswa kutunza vizuri ng’ombe wake wakubwa kwa lengo la kumpatia malisho bora na maji safi ya kutosha kila siku.  Mambo muhimu ya kuzingatia katika utunzaji wa ng’ombe wakubwa ni pamoja na:-
  • Ng’ombe apatiwe majani makavu (hei) wastani wa kilo 10 au majani mabichi kilo 40 kwa siku kutegemeana na uzito.  Iwapo malisho hayatoshi hususan wakati wa kiangazi apewe masalia ya mazao (viwandani na mashambani) kama molasisi, mabua, maharage, mpunga n.k
  • Ng’ombe apewe vyakula vya ziada (pumba, mashudu, madini mchanganyiko, unga wa mifupa na chokaa) kulingana na hatua na kiwango cha uzalishaji na
  • Ng’ombe apatiwe kinga na tiba ya magonjwa kulingana na ushauri wa mtaalam wa mifugo.

  UPANDISHAJI
  Mfugaji anapaswa kumpandisha ng’ombe kwa umri na wakati muafaka ili kuepuka matatizo ya uzazi na pia kuhakikisha anapata ndama bora na maziwa mengi.  Mambo muhimu ya kuzingatia ni pamoja na
  • Mtamba apandishwe akiwa na umri wa miezi 17 -24 na uzito wa kilo 230 – 300 kwa ng’ombe wa kigeni na umri wa miezi 30 – 36 na uzito wa kilo 200 kwa ng’ombe wa asili.  (Rejea jedwali Na 2)
  • Ng’ombe aliyekwisha zaa apandishwe siku 60 baada ya kuzaa na
  • Siku 18 – 23 baada ya kupandishwa, ng’ombe achunguzwe kama ana dalili za joto ili apandishwe tena.  Iwapo ng’ombe ataendelea kuonyesha dalili za joto baada ya kupandishwa mara tatu mfugaji apate ushauri wa mtaalam wa mifugo.

  JEDWALI NA.2.  UMRI NA UZITO UNAOSHAURIWA KUPANDISHA MTAMBA
  AINA YA NG’OMBE UZITO (KG) UMRI (MIEZI)
  Friesian 240 – 300 18 – 24
  Ayrshire 230 – 300 17 – 24
  Jersey 200- 250 18 – 20
  Mpwapwa 200 – 250 18 – 20
  Chotara 230 – 250 18 – 24
  Boran 200 – 250 24 – 36
  Zebu 200 30 -36


  DALILI ZA NG’OMBE ANAYEHITAJI KUPANDWA
  Ni muhimu mfugaji akazitambua dalili za ng’ombe anayehitaji kupandwa ili aweze kumpandisha kwa wakati.  Dalili hizo ni pamoja na
  •  Kupiga kelele mara kwa mara
  •  Kutotulia/kuhangaika
  •  Kutokwa na ute mweupe usiokatika ukeni
  •  Kupenda kupanda wenzake na husimama akipandwa na wenzake na
  •  Kunusanusa ng’ombe wengine
  Ng’ombe akionyesha dalili za joto apandishwe baada ya masaa 12, kwa kuhimilisha au kwa kutumia dume bora (kwa mfano, akionyesha dalili asubuhi apandishwe jioni na akionyesha dalili jioni apandishwe asubuhi).

  UHIMILISHAJI
  Uhimilishaji ni njia ya kupandikiza mbegu kwa ng’ombe jike kwa kutumia mrija.  Faida za uhimilishaji ni pamoja na kusambaza mbegu bora kwa haraka na kwa gharama nafuu, kupunguza gharama za kutunza dume na kudhibiti magonjwa ya uzazi.

  ILI MFUGAJI ANUFAIKE NA HUDUMA HII ANAPASWA KUFANYA YAFUATAYO:-
  Kuchunguza kwa makini ng’ombe mwenye dalili za joto
  Kumjulisha mtaalam wa uhimilishaji mapema ili kuwezesha zoezi hili kufanyika kwa wakati.
  Kuchunguza kama ng’ombe atarudi kwenye joto siku ya 18 – 23 baada ya kupandishwa na
  Ng’ombe aliyepandishwa apimwe mimba siku 60 hadi 90 baada ya kupandishwa.

  MATUNZO YA NG’OMBE MWENYE MIMBA
  Ng’ombe mwenye mimba huchukua miezi 9 hadi kuzaa.  Katika kipindi hicho chote anastahili kupatiwa lishe bora na maji ya kutosha ili akidhi mahitaji ya ndani aliye tumboni na kutoa maziwa mengi baada ya kuzaa.

  Mambo ya kuzingatia ni pamoja na
  • Ng’ombe apewe lishe bora na maji ya kutosha kipindi chote cha mimba
  • Miezi 2 kabla ya kuzaa apewe kilo 2 za chakula cha ziada kwa siku
  • Apewe kinga dhidi ya maambukizi na tiba ya magonjwa
  • Ng’ombe anayekaribia kuzaa, hususani mtamba, azoeshwe kuingia kwenye sehemu ya kukamulia.

  DALILI ZA NG’OMBE ANAYEKARIBIA KUZAA
  Mfugaji anapaswa kufahamu dalili za ng’ombe anayekaribia kuzaa ili aweze kufanya maandalizi muhimu.

  Dalili hizo ni pamoja na
  Kujitenga kutoka kwa wenzake
  • Kiwele kuongezeka 
  • Chuchu kutoa maziwa zikikamuliwa
  • Kutokwa na ute mwekundu na sehemu za uke kuvimba na kulegea
  • Kuhangaika kulala chini na kusimama na
  • Kati ya saa moja hadi mbili kabla ya kuzaa sehemu ya uke hutokwa na maji mengi ambayo husaidia kulainisha njia ya ndama kupita.

  HUDUMA KWA NG’OMBE ANAYEZAA
  Ng’ombe anayezaa anahitaji uangalizi wa karibu ili kuhakikisha usalama wa ng’ombe na ndama anaezaliwa.  Mambo ya kuzingatia ni pamoja na yafuatayo:-
  • Sehemu ya kuzalia ng’ombe iandaliwe kwa kuwekwa nyasi kavu na laini na iwe safi.
  • Ng’ombe ahamishwe sehemu iliyoandaliwa kwa ajili ya kuzaa mara baada ya dalili za kuzaa kuonekana na
  • Ng’ombe aachwe azae mwenyewe bifa usumbufu

  MFUGAJI APATE USHAURI/HUDUMA KUTOKA KWA MTAALAM IWAPO MATATIZO YAFUATAYO YATAJITOKEZA:-
  • Ng’ombe kushindwa kuzaa kwa masaa mawili hadi matatu baada ya chupa kupasuka
  • Kondo la nyuma kushindwa kutoka masaa sita baada ya kuzaa
  • Kizazi kutoka nje na
  • Ng’ombe kushindwa kusimama baada ya kuzaa

  MATUNZO YA NG’OMBE ANAYEKAMULIWA
  Ng’ombe anayekamuliwa anahitaji kupata chakula kwa ajili ya kujikimu na cha ziada kwa ajili ya uzalishaji wa maziwa.  Ili kukidhi mahitaji ya uzalishaji wa maziwa ng’ombe
  • Apewe chakula cha ziada kwa kiwango cha kilo 1 kwa kila lita 2 – 3 za maziwa anayotoa.
  • Apewe madini na virutubisho vingine kulingan ana mahitaji
  • Apewe maji mengi kwa vile ni ya muhimu katika kutengeneza maziwa.
  • Aachwe kukamuliwa siku 60 kabla ya kuzaa.  Uachishwaji huu ufanywe taratibu ili ifikapo siku ya 60 kabla ya kuzaa ukamuaji usitishwe.
  • Baada ya kusitisha kukamuliwa apewe kilo 2 za chakula cha ziada kwa siku hadi atakapozaa na
  • Apatiwe kinga dhidi ya maambukizi ya magonjwa na tiba kulingana na ushauri wa mtaalam wa mifugo.

  UZALISHAJI WA MAZIWA
  Lengo la ufugaji wa ng’ombe wa maziwa ni kupata maziwa mengi, safi na salama pamoja na mazao yatokanayo na maziwa .

  Mambo muhimu ya kuzingatia ni:-
  • Sehemu ya kukkamulia iwe safi na yenye utulivu
  • Ng’ombe awe na afya nzuri msafi na kiwele kioshwe kwa maji safi ya uvuguvugu.
  • Mkamuaji  awe msafi kucha fupi na asiwe na magonjwa ya kuambukiza
  • Inashauriwa mkamuaji asibadilishwebadilishwe
  • Vyombo vya kukamulia viwe safi
  • Muda wa kukamua usibadilishwe na
  • Maziwa ya mwanzo kutoka kila chuchu yakamuliwe kwenye chombo maalum (strip cup) ili kuchunguza ugonjwa wa kiwele.

  UCHAGUZI WA UTUNZAJI WA DUME BORA LA MBEGU
  Dume ndilo linalojenga ubora wa kundi  la ng’ombe katika masuala ya uzalishaji kutokana na uwezo wake wa kupanda majike 20 – 25 wakati wa msimu wa uzalianaji (breeding season).
  Ili kundi la ng’ombe liwe bora, mambo yafuatayo yazingatiwe
  • Chagua dume kutoka kwenye ukoo ulio bora kwa kuzingatia kumbukubu za uzalishaji wa maziwa au nyama za wazazi wake
  • Mfugaji apate ushauri wa mtaalam wa mifugo katika kuchagua dume bora
  • Lisha dume malisho bora na maji safi ya kutosha.  Pia apatiwe chakula cha ziada.
  • Katika ufugaji shadidi dume la ng’ombe  lifugwe kwenye banda imara lenye sehemu za kuwekea chakula maji na kufanyia mazoezi.
  • Katika ufugaji huria dume atengewe sehemu na kupatiwa chakula cha ziada.
  • Dume livalishwe pete puani kwa ajili ya kupunguza ukali na kuwezesha urahisi wa kumshika.
  • Dume apatiwe kinga na tiba ya magonjwa kulingan ana ushauri wa mtaalam wa mifugo na
  • Mfugaji apate ushauri wa mtaalam wa mifugo katika kuchagua dume bora.

  UTUNZAJI  WA NG’OMBE WA NYAMA
  Ng’ombe wengi wanaofugwa hapa nchini Tanzania ni wa asili ambao kwa kiwango kikubwa hutumika kwa ajili ya uzalishaji wa nyama.  Hata hivyo uzalishaji wake wa nyama ni mdogo kutokana na kasi ndogo ya kukua na kuwa na uzito mdogo wakati wanapopevuka.  Hali hii husababishwa na matunzo duni, kwa kuwa huchungwa/hulishwa kwa kutegemea malisho peke yake ambayo hayawezi kukidhi mahitaji ya viinilishe vinavyohitajika kwa ng’ombe.

  Ili kuongeza kasi ya ukuaji na kuongeza uzalishaji wa nyama, mfugaji anapaswa kufanya mambo yafuatayo:-

  UTUNZAJI WA NDAMA
  • Wajengewe banda/boma imara safi na lisilo na unyevunyevu ili kuepukana na magonjwa kama kichomi na kuhara
  • Waruhusiwe kunyonya kwa muda usiopungua miezi sita, pia wapatiwe majani laini kuanzia wanapofikia umri wa wiki mbili ili waanze kula mapema.
  • Wapatiwe maji safi na yakutosha
  • Ndama dume ambao hawatahitajika kwa ajili ya kuendeleza kizazi wahasiwe wakiwa na umri wa wiki mbili ili waanze kula mapema.
  • Wapatiwe maji safi na yakutosha
  • Ndama dume ambao hawatahitajika kwa ajili ya kuendeleza kizazi wahasiwe wakiwa na umri usiozidi miezi 3 ili wakue haraka na kuwa na nyama nzuri.
  • Wawekwe alama au namba za utambulisho kati ya siku ya kwanza na ya tano kwa ndama wote, mfano kuvalishwa hereni kwenye masikio, kwa ajili ya urahisi wa udhibiti wa umiliki na utunzaji kumbukumbu.
  • Ndama wachungwe eneo tofauti na ng’ombe wakubwa kuepuka maambukizi ya minyoo na magonjwa na

  UTUNZAJI WA NDAMA BAADA YA KUACHISHWA KUNYONYA HADI KUPEVUKA (MIEZI 6 – 24).
  Ndama wa umri huu anatakiwa apatiwe
  • Malisho bora na maji safi ya kutosha wakati wote
  • Vyakula vya ziada ili kukidhi mahitaji ya mwili (mifano ya vyakula mchanganyiko imeonyeshwa kwenye jedwali Na. 3 ) na
  • Tiba na kinga dhidi ya magonjwa hususan kinga ya kutupa mimba (S19) kwa ndama jike watakaotumika kuendeleza kundi.
  Katika kipindi cha miezi 6 hadi 24 mfugaji anashauriwa kuchagua ndama watakaoingizwa katika kundi la wazazi na wanaobaki wawe katika kunenepesha kwa ajili ya nyama.

  UTUNZAJI WA NG’OMBE WA NYAMA
  • Apatiwe malisho bora na maji safi ya kutosha wakati wote
  • Vyakula vya ziada (mifano ya vyakula mchanganyiko iliyooneshwa kwenye jedwali Na.3), ili kukidhi mahitaji ya mwili.
  • Vyakula vya ziada kiasi kisichopungua kilo 2 kila siku miezi 2 kabla ya kuzaa.
  • Nafasi ya kunyonyesha ndama kwa miezi 6 mfululizo,
  • Tiba na kinga dhidi ya magonjwa na
  • Apandishwe kwa kutumia dume bora au kwa kutumia njia ya uhimilishaji siku 60 baada ya kuaa.

  UNENEPESHAJI WA NG’OMBE WA NYAMA
  Ng’ombe kwa ajili ya nyama anaweza kuchinjwa akiwa na umri wa kuanzia miezi 3 kulingana na mahitaji ya soko.  Kwa kawaida hapa Tanzania ng’ombe huchinjwa wakiwa na umri wa kuanzia miezi 18 kwa ng’ombe wa kigeni na zaidi ya miezi 36 kwa ng’ombe wa kigeni na zaidi ya miezi 36 kwa ng’ombe wa asili.

  Ili mfugaji aweze kupata faida kutokana na ufugaji wa ng’ombe wa nyama anapaswa afanye yafuatayo:-
  • Afuge aina ya ng’ombe wanaokua na kukomaa haraka
  • Anenepeshe ng’ombe kwa muda wa miezi 3 – 6 kabla ya kuchinjwa.  Unenepeshaji huongeza ubora wa nyama na kipato kwa mfugaji.
  • Awapatie chakula chenye mchanganyiko wenye viinilishe vya kutosha viinilishe vya kutia nguvu na joto mwilini viwe na uwiano mkubwa kuliko vingine (Jedwali Na.3), na
  • Auze ng’ombe mara wanapofikisha umri na uzito unaohitajika katika soko ili kuepuka gharama za ziada.
  JEDWALI NA.3. MFANO WA MCHANGANYIKO WA CHAKULA KWA AJILI YA UNENEPESHAJI
  AINA YA CHAKULA KIASI KWA KILO
  Majani makavu ya mpunga/NganoHey 23.3
  Molasis 44.72
  Mahindi yaliyorazwa 18.94
  Mashudu ya Alizeti/pamba 11.4
  Madini mchanganyiko 0.7
  Chumvi 0.47
  Urea 0.47
  Jumla 100

  UZALISHAJI NA UHIFADHI WA MALISHO BORA NA VYAKULA VYA ZIADA
  Chakula kikuu cha ng’ombe ni nyasi, vyakula vingine ni pamoja na miti malisho, mikunde na mabaki ya mazao.  Ili kupata malisho misimu yote ya mwaka ni muhimu kuvuna na kuhifadhi malisho kipindi yanapopatikana kwa wingi.  Inawezekana kupanda malisho mengi kuliko kiasi kinachohitajika msimu mmoja/wakati wa mvua, kuyavuna yanapofikia hatua ya kutoa maua na kuyahifadhi (mfano wa malisho yanayoweza kupandwa ni mabingobingo, Guatemala, African fox-tail, desmodium, centrosema, lukina n.k).  Malisho yakupandwa ni vizuri yawe na mchanganyiko wa jamii ya nyasi, mikunde na miti malisho.

  MASALIA YA MAZAO SHAMBANI
  Masalia ya mazao shambani kama vile mabua, magunzi, majani ya mikunde, viazi, ndizi, mpunga, na mengineyo yanaweza kukusanywa na kuhifadhiwa vizuri kama chakula cha ng’ombe.

  MALISHO YA MITI NA MATUNDA YAKE
  Malisho yatokanayo na miti ya malisho na matunda yake yanaweza kutumika kama malisho ya ng’ombe.  Majani na matunda ya miti ya lukina, sesibania, migunga na mbaazi yanaweza kukaushwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya kulisha ng’ombe.

  VYAKULA VYA ZIADA
  Ili kukidhi mahitaji ya viinilishwe kulingana na kiwango cha uzalishaji, ng’ombe anatakiwa kupewa vyakula vya ziada.  Vyakula hivyo vinatokana na mchanganyiko wa vyakula mbalimbali.  Michanganyiko hii  inategemeana na upatikanaji wa malighafi katika maeneo husika.

  Mifano ya mchanganyiko huo ni kama ifuatavyo:-

  EDWALI NA. 4 MFANO WA KWANZA WA CHAKULA CHA ZIADA
  AINA YA CHAKULA KIASI (KILO)
  Pumba za mahindi 47
  Mahindi yaliyoparazwa 20
  Mashudu ya alizeti/pamba 20
  Unga wa lukina 10
  Chokaa ya mifugo 2
  Chumvi 1
  Jumla 00

  Mfano wa pili wa chakula cha ziada ni tofali la kulamba lenye urea ambalo mchanganyiko wake ni:-

  Unga wa mahindi                  kilo 1  
  Pumba za mahindi                               kilo 3
  Urea                                                       kilo 1
  Mashudu ya alizeti                               kilo 2
  Chumvi  ya kawaida                            gramu 200
  Unga wa mifupa                                   gramu 200
  Chokaa ya mifugo                                  kilo 1.5
  saruji                                                        kilo 1

  mfugaji anatakiwa kuzingatia yafuatayo ili kupata tija katika ufugaji:-
  • kulisha mchanganyiko wa nyasi, mikunde na mchanganyiko wa madini na vitamin
  • kutenga maeneo kwa ajili ya kulisha ng’ombe kwa mzunguko pamoja na kupanda malisho katika mfumo huria na nusu huria na
  • kuvuna nyasi na mikunde inapofikia hatua ya kutoa maua na kuyahifadhi kwa matumizi wakati wa uhaba wa malisho hususan wakati wa kiangazi.
  NJIA ZA KUHIFADHI MALISHO
  Malisho yanaweza kuhifadhiwa kwa kuyakausha (Hei) au kuyavundika (Sileji).

  HEI
  Hei ni majani yaliyohifadhiwa kwa kukaushwa baada ya kukatwa au kuachwa kukauka yakiwa shambani kwa matumizi ya baadaye.  Katika kutengeneza hei yafuatayo yazingatiwe:-
  • vuana malisho yanapoanza  kutoa maua
  • aanikwe kwa siku 3 hadi 6 kutegemea aina ya malisho na hali ya hewa na yageuze mara 1 au 2 kwa siku ili yakauke vizuri.
  • Yafungwe katika marobota baada ya kukauka inawezekana kutumia kasha la mbao lenye vipimo vifuatavyo:-  Urefu sentimeta 75, upana sentimeta 45 na kina sentimeta 35 au mashine na zana za kufunga marobota ya hei na
  • Hifadhi marobota juu ya kichanja ili kuzuia maji yasiingie unyevu na kuharibiwa na wadudu.
  SILEJI
  Sileji ni majani yaliyokatwakatwa na kuvundikwa.  Madhumuni ya kuyavundika ni kuyawezesha kubaki na ubora wake hadi wakati yatakapotumika katika kutengeneza sileji yafuatayo yazingatiwe:-
  • Tengeneza sileji kwa kutumia majani yenye sukari nyingi kama mahindi au mabingobingo na mikunde, mabaki ya viwandani kama molasis,
  • Andaa shimo au mfuko wa plastiki kulingana na kiasi cha majani yaliyovunwa.
  • Vuna majani ya kuvundika katika umri wa kuanza kutoa maua.  Endapo majani yaliyovunwa ni teketeke yaachwe kwa siku moja yanyauke kupunguza kiwango cha maji.
  • Katakata majani uliyovuna katika vipande vidogovidogo,
  • Tandaza majani uliyokatakata ndani ya shimo au mfuko katika tabaka nyembamba na kushindilia ili kuondoa hewa yote.
  • Funika shimo ulilojaza majani kwa plastiki ikifuatiwa na udongo.
  • Sileji itakuwa tayari kutumika kuanzia siku 21 na
  • Sileji iliyofunguliwa kwa ajili ya matumizi ifunikwe haraka iwezekanavyo ili kuzuia kuharibika.
  Sileji inaweza kubaki na ubora katika shimo kwa muda mrefu kama haitafunguliwa na kuachwa wazi kwa muda mrefu.

  UDHIBITI WA MAGONJWA YA NG’OMBE
  Magonjwa huweza kusababishwa na matunzo hafifu lishe duni na visababishi vya magonjwa kama vile protozoa bacteria.
  Virusi, riketsia na minyoo.  Aidha wadudu kama kupe na mbung’o wanasambaza visababishi vya magonjwa.

  Afya bora ya ng’ombe inatokana na kuzingatia mambo yafuatayo:-
  • Ndama apate maziwa ya awali (dang’a) ya kutosha kwa siku 3 – 4 baada ya kuzaliwa ili kuongeza kinga ya magonjwa mwilini.
  • Chovya kitovu cha ndama ndani ya madini joto (Tincture of Iodine) mara baada ya kuzaliwa kuzuia kuvimba kitovu kutokauka au kutohudumiwa ipasavyo mara baada ya ndama kuzaliwa.  Kitovu huvimba na kutoa usaha hukojoakwa shida na wakati mwingine huvimba viungo.
  • Ndama apewe dawa ya kuzuia minyoo kila baada ya miezi 3 kama atakavyoshauri mtaalam wa mifugo.  Minyoo huwashambulia ndama zaidi hasa wale walioana kula majani.
  • Zingatia usafi wa vyombo na band a epuka kumpa ndama maziwa yaliyopoa na machafu ili kuzuia kuharisha.
  • Zingatia ujenzi wa mabanda kuruhusu mzunguko wa hewa ili kuzuia ndama kupata ugonjwa wa vichomi.  Vichomi huwapata ndama wa umri wa miezi 5 au zaidi wanaofugwa ndani katika mabanda machafu yasiyo na mzunguko wa hewa ya kutosha.
  • Ogesha ng’ombe kulingana na ushauri wa mtaalam wa mifugo ili kuua kupe wote wanaoleta magonjwa yatokana yo na kupe (ndigana kali na baridi, kukojoa damu na maji moyo) na mbung’o (ndorobo) na
  • Ng’ombe wapatiwe chanjo dhidi ya magonjwa mbalimbali chanjo muhimu ni za ugonjwa wa kutupa mimba, kimeta, ugonjwa wa miguu na midomo na chambavu.

  Mfugaji anashauriwa kutoa taarifa kwa mtaalam wa mifugo anapoona ng’ombe wake ana baadhi ya dalili zifuatazo:-
  • Joto kali la mwili na manyonya kusimama
  • Amepunguza hamu ya kula
  • Amezubaa na kutoa machozi
  • Anasimama kwa shind ana kusinzia
  • Anapumua kwa shida na pua kukauka
  • Anatokwa na kamasi nyingi
  • Anajitenga na kundi
  • Anaconda na
  • Anapunguza utoaji wa maziwa ghafla

  KUMBUKUMBU NA TAKWIMU MUHIMU
  Kumbukumbu ni taarifa au maelezo sahihi yaliyoandikwa kuhusu matukio muhimu ya kila ng’ombe na shughuli zote zinazohusiana na ufugaji.  Mfugaji anashauriwa kuweka kumbukumbu na takwimu muhimu katika shughuli zake za ufugaji wa ng’ombe.  Kumbukumbu zinamsaidia mfugaji kujua mapato na matumizi na kufanya maamuzi sahihi kuhusu mifugo husika na mifugo husika na mazao yake.  Aidha humwezesha kuweka mipango ya shughuli zake.

  Mfugaji anapaswa kuweka kumbukumbu muhimu zifuatazo:-
  • Uzazi (uhimilishaji na matumizi ya dume, tarehe ya kupandwa, kuzaa kuachisha kunyonya)
  • Kinga na tiba
  • Utoaji wa maziwa
  • Ukuaji
  0

  Add a comment

 7. AINA BORA YA NG'OMBE WA MAZIWA
  AINA BORA YA NG’OMBE WA MAZIWA
  AINA BORA YA NG’OMBE WA MAZIWA : Ndugu msomaji leo nitakuletea kitu kipya na chenya manufaa sana ukikizingatia,hizi ni aina ya ng’ombe wa maziwa waliopo duniani.

  MAMBO YA KUZINGATIA KWENYE UCHAGUZI WA NG’OMBE MZURI WA MAZIWA
  Umbo : siku zote ngo’mbe wa maziwa anatakiwa awe na umbola pembe tatu, humpless pia awe na miguu imara pamoja na tumbo kubwa kwa sababu ng’ombe mwenye tumbo kubwa anaweza kula sana na kutunza chakula kingi.na chakula kingine kinabadilishwa na kua maziwa.hivyo ng’ombe mwenye tumbo kubwa anauwezo wa kutoa maziwa mengi sana.
  Kiwele na chuchu: siku zote ng’ombe mzuri wa maziwa anakiwele kizuri kimeshika vizuri kwenye mwili na kiwele kizuri hua kinabonyea kama spongy.na pia kiwele na chuchu vinatakiwa kua kubwa.
  Rangi ya mwili : sikuzote ng’ombe mzuri wa maziwa anarangi moja au mbili tu kwenye mwili wake e.g brown, red white and black.
  Asili : siku zote ng’ombe mzuri wa maziwa anatokea katika maeneo yenye hali ya hewa ya kati  e.g Holland, Switzerland, Scotland and other part of Europe and Asia.
  AINA BORA YA NG'OMBE WA MAZIWA
  AINA BORA YA NG’OMBE WA MAZIWA
  AINA ZA NG’OMBE WA MAZIWA
  Kuna makundi mawili ya ng’ombe kuna wa nyama pamoja na wamaziwa. na kuna aina nyingine pia ni wazuri kwa nyama pamoja na wamaziwa mfano mpwapwa na sahiwal.

   Hizi hapa na aina za ng’ombe wa maziwa

  • Holstein Friesian
  • Brown swiss
  • Ayrshire
  • Guernsey
  • Jersey
  • Mpwapwa
  • Sahiwal
  • Red poll

   AINA ZA NG’OMBE WA MAZIWA NA SIFA ZAKE
  HOLSTEIN FRIESIAN
  HOLSTEIN FRIESIAN
  HOLSTEIN FRIESIAN

  1. HOLSTEIN FRIESIAN
   Hii  ni aina ya ng’ombe wa maziwa ambayo ni kubwa kuliko aina zote

    SIFA
  • Asili yake ni Holland
  • Wanamabaka meupe na meusi
  • Maziwa yao yana mafuta kiasi cha 3.5%
  • Wanatoa maziwa mengi  6000 liters kwa kila msimu wa kukamua
  • Watoto wake wanazaliwa wakiwa na 40 kg na zaidi.
  • Jike anauzito wa 400-600kg na dume 600-1000kgs

  BROWN SWISS
  BROWN SWISS
  BROWN SWISS

  1. BROWN SWISS
   Hii ni kati ya aina za zaman sana, ili gunduliwa katika milima ya Switzerland?

   SIFA
  • Wame gunduliwa Switzerland
  • Hii ni aina nzito inayo fuata baada Friesian
  • Wanalangi ya brown inayo koza niwapole
  • Uzito wa jike 450-550kg na dume 600-900kgs

  AYSHIRE
  AYSHIRE
  AYSHIRE

  1. AYSHIRE
   Hii ni aina kubwa inayo fata baada yaFriesian na brown Swiss SIFA
  • Niwakubwa zaidi ya jersey na Guernsey
  • Wanarangi nyekundu  kuelekea mahogany mchanganyiko na nyeupe
  • Asili yao ni South west Scotland
  • Maziwa yao yanamafuta 4%
  • Wanachuchu na kiwele kizuri sana

  GUERNSEY
  GUERNSEY
  GUERNSEY

  1. GUERNSEY

   SIFA
  • Wanatoa maziwa yenye langi kama ya dhahabu
  • Wanarangi nyeupe na nyekundu
  • Maziwa yao yanamafuta 4.5%
  • Wanatoa maziwa 4200litres kwa msimu mmoja wa kukamua
  • Uzito wa jike 450-500kgs na dume 600-700kgs

  JERSEY
  JERSEY
  JERSEY

  1. JERSEY
   hii ndo aina ndogo kuzudi zote

   SIFA
  • Asili yao ni visiwani kati ya UK na France
  • Maziwa yao yanamafuta kuzidi wote 5%
  • Wanarangi ya blackish brown
  • Uzito wa jike 400-450kg  dumeto 500-600kgs. 
  Ahsante mpenzi msomaji endelea kua na mimi upate kujifunza mengi kwa tasinia ya kilimo pamoja na ufugaji na pia usisahau kuifollow blog hii hili kipata kile ninacho kiandika moja kwa moja kwenye email yako
  0

  Add a comment


 8. FAIDA NYINGI ZITOKANAZO NA UFUGAJI WA NYUKI
  FAIDA NYINGI ZITOKANAZO NA UFUGAJI WA NYUKI
  FAIDA NYINGI ZITOKANAZO NA UFUGAJI WA NYUKI : Kufuga nyuki na kuzalisha asali kwa mtindo wa kisasa kwa kujenga nyumba ya nyuki inamwezesha mfugaji kuongeza uzalishaji pamoja na kipato.
  Ufugaji wa nyuki ni kazi ambayo imekuwepo na kudumu kwa karne nyingi sana. Shughuli ya ufugaji wa nyuki nchini Tanzania hasa katika mkoa wa Tabora ambao ni maarufu kwa uzalishaji wa asali, ilianza kutambulika rasmi tangu mwaka 1884, wakoloni kama vile Rebman na Craft walipofika katika eneo hilo.
  Katika kipindi hicho, jamii ya eneo hilo walikuwa wanafuga nyuki kwenye magome ya miti, vibuyu, vyungu, mapango, vichuguu na kwenye miamba. Baada ya muda ufugaji ulipiga hatua kidogo na watu wengi wakawa wanafuga kwa kutumia mizinga iliyochongwa kutoka kwenye magogo ya miti. Ufugaji wa aina hii umedumu kwa karne nyingi kote nchini Tanzania.
  Kutokana na uhitaji na ongezeko la matumizi ya bidhaa za nyuki, kulifanyika tafiti mbalimbali ambazo ziliweza kuboresha ufugaji wa nyuki kwa kuwa na mizinga ya kisasa ambayo imewezesha uzalishaji wa asali kuwa mkubwa na kuongeza pato la wafugaji tofauti na ilivyokuwa hapo awali. Tafiti hazikuishia kwenye kuboresha mizinga tu, ila siku hadi siku kunavumbuliwa namna bora zaidi za kuimarisha uzalishaji wa nyuki. Katika makala hii, tutazungumzia namna ambavyo unaweza kuwajengea nyuki nyumba ili kuboresha mazingira yao ya uzalishaji, na hatimae kupata ufanisi zaidi.
  NYUMBA YA NYUKI
  Hii ni aina mpya ya ufugaji wa nyuki ambapo unaweza kujenga kibanda au nyumba kisha kuweka mizinga idadi unayohitaji.
  NI KWA NINI KUJENGA NYUMBA AU KIBANDA?
  • Ni muhimu kufuga nyuki kwenye kibanda au kwenye nyumba kwa sababu inasaidia kudhibiti wizi wa mizinga, pamoja na wanyama wanaokula asali na kudhuru nyuki.
  • Inarahisisha utunzaji wa mizinga na kuwafanya nyuki wasihame kwenda sehemu nyingine.
  • Inasaidia watu wengi kujifunza namna nzuri ya ufugaji wa nyuki, ikiwa ni pamoja na watoto, jambo ambalo linafanya shughuli hii kuwa endelevu.
  • Ufugaji wa aina hii unasaidia kuwak inga nyuki dhidi ya majanga kama vile moto, na mafuriko.
  • Inawaepusha nyuki na usumbufu unaoweza kuwafanya wasizalishe kwa kiwango kinachotakiwa.
  • Uzalishaji unaongezeka. Hii ni kwa sababu mizinga inayotumika ni ile ya kibiashara. Mzinga 1 unapata asali kilo 30 sawa na lita 20.
  AINA TATU ZA NYUKI
  AINA TATU ZA NYUKI
  CHUMBA CHA NYUKI AINA YA NYUMBA
  Unaweza kujenga nyumba yenye upana wa futi 3 na urefu wa futi 9. Nyumba hii inaweza kuchukua mizinga hamsini. Halikadhalika, unaweza kujenga kibanda chenye ukubwa sawa na huo.
  ENEO LINALOFAA
  • Ili kuwa na ufanisi mzuri, nyumba hii inafaa kujengwa nje kidogo ya makazi ya watu.
  • Kusiwe na mifugo karibu.
  • Iwe sehemu ambayo watoto hawawezi kufika.
  • Isiwe karibu na njia ambayo watu wanapita mara kwa mara.
  • Kusiwe na aina ya mimea ambayo nyuki hawapendi.
  • Kuwe na maji karibu.
  NYUKI KAZINI
  NYUKI KAZINI
  MAVUNO
  Baada ya kujenga nyumba, kuweka mizinga na nyuki kuingia, unaweza kuvuna kwa mara ya kwanza baada ya miezi mitatu. Utaweza kupata mavuno mazuri endapo utavuna kabla nyuki na wadudu wengine hawajaanza kula asali.
  Ni muhimu kuhakikisha kuwa wadudu waharibifu kama vile sisimizi, mende na wengineo wanadhibitiwa ili kutokuathiri uzalishaji wa asali. Hakikisha unavuna kitaalamu ili kuepuka upotevu wa asali. Endapo nyuki wametunzwa vizuri na kwenye mazingira mazuri, unaweza kuvuna asali mara tatu kwa mwaka. Katika mzinga mpya nyuki wana uwezo wa kutengeneza masega kwa siku tatu na kuanza uzalishaji wa asali.
  NI NINI UMUHIMU WA ASALI
  • Asali inatumika kama chakula
  • Inatumika kama tiba ya magonjwa mbalimbali
  • Hutumika kutibu majeraha
  • Ni chanzo kizuri cha kipato
  • Hutumika katika kutengeneza dawa za binadamu
  • Asali inaweza kuhifadhiwa kwa miaka mingi sana bila kuharibika. Hii inatokana na wingi wa dawa maalum iliyo nayo inayofanya isiharibike.
  MATUMIZI YA ASALI
  MATUMIZI YA ASALI
  BIDHAA ZINAZOTOKANA NA ASALI
  Chumba cha nyuki 2Kuna aina nyingi ya bidhaa zinatokana na asali, kwa kutengenezwa na nyuki wenyewe na nyingine zikitengenezwa na binadamu kutokana na tafiti mbalimbali.
  MIONGONI MWA BIDHAA HIZO NI:
  • Asali yenyewe
  • Royal jelly : Hii ni aina ya maziwa yanayotengenezwa na nyuki, ambayo hutumika kama tiba.
  • Gundi: Hii hutumika kutengeneza bidhaa za aina mbalimbali kulingana na mahitaji ya mtumiaji.
  • Nta: hutumika kutengenezea mishu maa, kulainisha nyuzi, kutengeneza dawa ya viatu, mafuta ya kupaka, pamoja na dawa ya ngozi.
  0

  Add a comment

 9. NJIA RAHISI ZA UPATIKANAJI WA VIFARANGA WENGI
  NJIA RAHISI ZA UPATIKANAJI WA VIFARANGA WENGI
  NJIA RAHISI ZA UPATIKANAJI WA VIFARANGA WENGI: Kuna njia tofauti za kuanza au kuongeza mtaji kwa mfugaji wa kuku kama vile, kununua kuku wakubwa, vifaranga kutoka kwa wafugaji wengine au kuzalisha vifaranga wako wewe mwenyewe.
  Kwa wafugaji wengi ambao wana lengo la kufuga kuku wengi wa umri mmoja na kupata mayai mengi au aweze kuuza kuku wengi kwa wakati mmoja wenye umri unaolingana inabidi uwe na vifaranga wengi wa umri mmoja.
  KWA NINI KUWA NA VIFARANGA WENGI WA UMRI MMOJA?
  • Kupunguza gharama za ufugaji kwa mfano chanjo na tiba;
  • Kutunza kuku kitaalam kwa urahisi
  • Kupata mayai mengi kwa wakati mmoja
  • Kuuza kuku wengi kwa waakti mmoja
  • Kuwapa uhakika wateja wako
  NJIA RAHISI ZA UPATIKANAJI WA VIFARANGA WENGI
  NJIA RAHISI ZA UPATIKANAJI WA VIFARANGA WENGI

  HIVYO KUNA NJIA KUU MBILI ZA UPATIKANAJI WA VIFARANGA WENGI KWA WAKATI MMOJA NAZO NI;
  1. Kwa kuhatamiza kuku wengi kwa wakati mmoja
  2. Kwa njia ya mashine ya kuangulia incubator)
  Njia zote mbili huweza kutoa vifaranga bora bali uchaguzi wa njia ipi itumike utatokana na mtaji wa mfugaji na mahali alipo.

  KWA KUHATAMIZA KUKU WENYEWE
  Njia hii hutumika kuhatamisha tetea wengi kwa wakati mmoja hivyo mfugaji anatakiwa achague mitetea, mayai, aandae viota, maji na chakula bora.
  SIFA ZA TETEA WA KUHATAMIA
  • Kuku mwenye umbo kubwa
  • Mwenye uwezo na historia nzuri ya kuhatamia na hatimaye kutotoa vifaranga
  SIFA ZA MAYAI YA KUHATAMISHA
  • Mayai ya siku ya mwisho kutagwa ndio yawe ya kwanza kuwekwa yafuatiwe na ya siku zinazofuata yasizidi wiki mbili tangu kutagwa
  • Lisiwe kubwa sana au la duara, lisiwe na uvimbe
  • Yasiwe machafu wala yasiwe na nyufa
  SIFA ZA KIOTA NA CHUMBA CHA KUHATAMIA
  • Kuku wanaohatamia watengwe katika chumba ili kuondoa tatizo la kutagiana.
  • Mlango na dirisha viwekwe wavu ili muda wa mchana mwanga na hewa uweze kuingia ndani.
  • Chumba kiwe na nafasi ya kutosha kuweka viota, chakula na maji.
  • Ili kutumia eneo vizuri viota vinaweza kutengenezwa ukutani kama mashelfu.
  • Viota viundwe vizuri kwa nyasi, maranda makavu ya mbao, au nguo ya pamba lakini isiyo tetroni.
  • Viota visiwe sehemu yenye unyevunyevu.
  • Idadi ya viota vilingane na idadi ya matetea walio chaguliwa kuatamia
  • Vinyunyiziwe dawa ya kuuwa wadudu kama utitiri kwani hawa ni wadudu wasumbufu ambao husababaisha kuku kutokatoka nje, hivyo kupunguza uwezekano wa mayai kuanguliwa yote.

  CHAKULA, VITAMINI NA MAJI
  Kuku wanaohatamia wapewe chakula cha kuku wakubwa wanaotaga (layers mash) cha kutosha muda wote kiwemo kwa kua kuku hawa hutoka wakati tofauti pia majani, mboga-mboga na maji ya kunywa ni muhimu sana. Vyote hivi viwekwe kwenye chumba ambacho kuku wanahatamia ili kumfanya kuku asiende umbali mrefu kutafuta chakula pia kuyaacha mayai kwa muda mrefu.

  HATUA ZA KUHATAMISHA KUKU
  1. Kuandaa viota, uchaguzi wa matetea bora na kuandaa mayai.
  2. Tetea wa kwanza akianza kuhatamia muweke mayai yasio na mbegu ama viza.
  3. Rudia zoezi hili mpaka itakapo fikia idadi ya kuku unao wahitaji.
  4. Baada ya kupata idadi ya kuku wawekee mayai yenye mbegu.

  N.B. kuku wote waliochaguliwa kwa ajili ya kuhatamia wawekwe wakati wa usiku kwa sababu ya utulivu uliopo.

  Kwa kupitia njia hii kuku mmoja anaweza kuhatamia hadi mayai 20 ukizingatia sifa za kuku huyo. Baada ya kutotoa hatua ya awali ya uleaji wa vifaranga. Kuku wazazi hutengwa na vifaranga ambapo vifaranga hupewa joto na mwanga kwa kutumia taa ya umeme, jiko au kandili. Maji yenye glucose kwa ajili yakuongeza nguvu, pia chakula.

  CHANGAMOTO
  • Huhitaji sehemu kubwa kwa sababu ili upate vifaranga wengi unahitaji kuku wengi wanao atamia.
  • Kuwepo kwa wadudu kama utiriri na kutopatikana kwa chakula cha kutosha husababisha kuku kutoka toka nje na kusababisha mayai kuharibika.
  • Kuku kupata magonjwa wakati wanapo atamia.
  • Kutokuwa na kipimo cha kupimia mayai yaliyo na mbegu

  Ushauri kutoka kwa mfugaji: Wakulima tubadilike na kuanza kufuga kibiashara kwa kua soko la mazao ya kuku wakienyeji lipo. Pia tuweze kuzalisha mayai bora ya kutotolesha, ni muhimu sana yatokane na kuku wako ama kwa mfugaji ambaye una uhakika na ufugaji wake.
  0

  Add a comment

 10. UFAGAJI BORA WA KUKU AINA YA KULOIREL
  UFAGAJI BORA WA KUKU AINA YA KULOIREL
  UFAGAJI BORA WA KUKU AINA YA KULOIREL: Kuloirel ni kuku chotara ambaye asili yake ni nchini india, na imetokana na mchanganyiko wa  dume la broiler na jike aina ya Rhode island red au dume la white legham na jike la Rhode island red. Kuku hawa ni moja kati ya kuku wasio na gharama kubwa katika kuwafuga lakini pia wana faida kubwa pindi ukiamua kuwafuga. Lakini pia
  kuku hawa ni moja kati ya mbegu ambayo inafanya vizuri sana katika nchi nyingi.

  SIFA ZA KULOIREL
  1. Ni aina ya kuku ambao hutumika kwa matumizi ya ani nyama pamoja na mayai
  2. Kuku mmoja anauwezo wa kutaga mayai 150 hamsini kwa mwaka ukilinganisha na kuku wengine hutoa 40- 50 kwa mwaka.
  3. Madume ya  kuloirel hua yana kilo 3.5  na jike ni kilo 2.5  ukilinganisha na kuku wengine dume hua na kilo 2.5 na jike ni kilo 1.5.
  4. Pia ni moja kati ya aina ambayo haipati magonjwa kirahisi (disease resistance)
  5. Kuku hawa hawana gharama sana katika kuwalisha kwa sababu wanauwezo pia wa kula chakula kama kuku wa kienyeji. 

  BANDA 
  Kama walivyo  kuku wengine banda lazima liwe bora ili kuweza kupata kuku bora pamoja na mayai mengi, ila pia kuku wa aina ya kuroiler sio lazima uwafungie ndani moja kwa moja unaweza kutengeneza sehemu ambayo utawafungulia ili kuweza kujipatia chakulatofauti na kuku wa kisasa.
  Lakini pia ni vyema kila wakati ukazingatia usafi ni muhimu hivyo ni vyema kuzingatia hilo 

  CHAKULA

  Chakula ni lazima kiwe bora ili kupata kuku bora pamoja na mayai ya kutosha.
  1. Kuku jike mmoja anakadiliwa kula kilo 5-8 kabla ya kuanza kutaga.
  2. muhimu sana kwa mfugaji kujifunza jinsi ya kuchanganya chakula mwenyewe.
  3. kuanzia siku 1 hadi wiki 4 unatakiwa kuwapa chakula cha kuanzia (chick starter mash)
  4. kuanzia wiki ya 4 hadi 8 unawapa chakula cha kukuzia (chick grower mash)
  5. Kuanzia wiki ya kwanza kuanza kutaga hadi mwisho unatakiwa kuwapa chakula(layersmash)
  6. Lakini pia inakadiliwa kua na drinker 15 na vyombo vya kulia chakula, wastani wa kuku 1000.
  3

  View comments


 11. MAMBO YA MSINGI YA KUZINGATIA KATIKA UJENZI WA BANDA LA KUKU
  MAMBO YA MSINGI YA KUZINGATIA KATIKA UJENZI WA BANDA LA KUKU
  MAMBO YA MSINGI YA KUZINGATIA KATIKA UJENZI WA BANDA LA KUKU: Habari ndugu mfugaji, katika ufugaji kuku kitu moja wapo cha kuzingatia banda bora. Banda bora litawafanya kuku wako wakue vizuri na kuwa Kinga na magonjwa Karibu tuwe pamoja hapa!! Ujenzi wa mabanda bora ya kuku ni miongoni mwa mambo ya msingi kabisa katika ufugaji bora wa kuku wawe ni wa asili au wale walioboreshwa. Hata hivyo si kila mtindo wa ujenzi unafaa, kwahiyo ujenzi huo ni lazima uzingatie mahitaji halisi ili ufugaji huo uweze kutoa matokeo bora yanayotarajiwa na mfugaji.

  MAMBO MUHIMU KATIKA UJENZI WA BANDA LA KUKU NI;
  1.  Liingize hewa safi wakati wote.
  2. Liwe kavu daima.
  3. Liwe nafasi ya kutosha.
  4. Liwe la gharama nafuu lakini la kudumu.
  5.  Lizuie kuingia wanyama na wadudu hatari kwa kuku.
  6. Liwe na nafasi ya kuweka vyombo vya chakula na maji. 
  7.  Lizuie upepo wakati wa baridi kali.

  HEWA NA MWANGA:
  Hewa ni muhimu kwa kila kiumbe, hivyo banda la kuku ni lazima liingize hewa safi na kutoa ile chafu na liweze kuingiza mwanga wa kutosha. _. Kwa kifupi ni kwamba madirisha ya banda ni lazima yawe makubwa na ya kutosha ili yaingize hewa safi na kutoa ile chafu. _ Ni vema madirisha haya yawe juu kiasi cha meta moja (1) kutoka chini ili hewa ipite juu ya vichwa vya kuku.
   Hewa safi siyo upepo, hivyo jaribu kuzuia upepo mkali kuingia ndani ya banda la kuku ama sivyo kuku wataugua ugonjwa wa mafua na niumonia na vifaranga vinaweza kufa kwa ugonjwa wa baridi.
  Jenga Banda lako kwa kukinga upepo unakotokea na kupanda miti kuzunguka banda hilo la kuku ili kupunguza kasi ya upepo na kuweka kivuli dhidi ya jua kali na joto.
  banda la kuku
  banda la kuku
  UKAVU NA USAFI NDANI  YA BANDA.
  Kwa vile kuku si ndege wa majini kama bata , ni jambo la busara kuhakikisha kuwa mahali anapoishi hapana unyevunyevu. Banda la kuku lijengwe mahali palipoinuka ili kuzuia maji ya mvua yasiingie. Wajengee kuku uchaga wa kulalia kwa kuweka viguzo vyenye urefu wa meta moja na kutandika miti juu yake ili usiku walale hapo, kuliko kuwalaza ardhini au sakafuni.
  Ukavu wa banda ni muhimu sana hasa kwa vifaranga na kuku wanaotaga. Ndani ya banda lenye unyevu mayai kuchafuka sana hata wakati mwingine huoza kwa urahisi na jitihada zako zitakuwa ni bure. Sakafu ya banda ni vizuri ikawa ya zege lakini kutokana na uhaba wa fedha sakafu inaweza kutengenezwa kwa mabanzi (mabanda yaliyoinuliwa) au udongo mgumu na au mchanga ambao utafunikwa kwa mabaki ya taka za mpunga na yale ya mbao. Ili kuepuka unyevunyevu ni vyema eneo/mahali pla kujenga banda pawe pameinuka na penye kupitisha hewa ya kutosha.

  PAA LA BANDA.
   Paa la banda liwe madhubuti ili kuzuia maji ya mvua kuingia hasa wakati wa masika. Sakafu ya banda iwe juu zaidi ya usawa wa nje. Paa linaweza kuezekwa kwa mabaki ya vipande vya bati , madebe na kama ikishindikana tumia nyasi zinazofaa kwa ajili ya kuezeka nyumba katika eneo hilo.

  NAFASI YA KUFANYIA KAZI.
   Banda la kuku lisiwe na nguzo au mbao nyingi sana ndani kiasi cha kumfanya mhudumiaji wa kuku ashindwe kufanya kazi zake. Hali hiyo itamfanya apoteze muda mwingi katika kuzizunguka nguzo hizo, hasa wakati wa kuokota mayai au kufanya usafi.
  Unapotaka kujenga banda la kuku kwanza kabisa tayarisha vifaa vinavyotakiwa. Vitu kama miti au nyasi, nyavu au fito, misumari au kamba ni muhimu kuviandaa mapema. Pili ni lazima uwe na plani/ramani kamili ya banda hilo. Kwa wastani kila kuku anahitaji nafasi ya Meta za eneo la 0.11 hadi 0.22 (futi 1 hadi 2 za eneo.) kutegemeana na umri wa kuku.
  Kuku wafugwao hatimaye ni lazima wafidie gharama za Ujenzi wa mabanda na chakula. Gharama zikiwa kubwa sana huenda ukaifanya shughuli ya ufugaji isiwe na faida hata kidogo hali hiyo itamfanya mfugaji aone ufugaji hauna maana yoyote kwake.
   Lakini ukijenga banda lako kwa kutumia vifaa vinavyopatikana kwa urahisi utaongeza faida zaidi kwakuwa umepunguza gharama za uendeshaji wa mradi.

  VIPIMO VYA BANDA.
  Banda la kuku linatakiwa liwe na Meta 15 hadi meta 22 za eneo yaani Meta 3 hadi 4.5 za upana kwa meta 5 za urefu. Banda hili linaweza kutunza kuku 100 wakubwa kwa wakati mmoja.

  ZINGATIA HAYA·
  Ujenzi wa mabanda unasisitizwa katika kuboresha ufugaji wa kuku wa asili iliKuongeza uzalishaji na kupunguza vifo vya vifaranga kwa majanga mbalimbali kama vicheche ,mwewe, mapaka, mbwa na wizi wa kuku wanaozurura holela. · Vile vile Inatakiwa kwamba kuku wanaozuiliwa kwenye banda na kuwekewa chakula mchanganyiko wataongeza uzalishaji kwa kiasi kikubwa.
  0

  Add a comment

 12. BATA MZINGA UJASIRIAMALI MPYA KWA WAFUGAJI
  BATA MZINGA UJASIRIAMALI MPYA KWA WAFUGAJI
  BATA MZINGA UJASIRIAMALI MPYA KWA WAFUGAJI: Unapotaja ufugaji, wengi wanakimbilia kuku, bata, ng’ombe, mbuzi, kondoo, ni wachache wanaoweza kukutajia  bata mzinga.
  Ndege huyu analipa sokoni, ila lazima niseme tangu mapema kuwa ndege hawa wanahitaji matunzo ya hali ya juu. Pia, hula chakula kingi kuliko kuku.
  Ukiondoa chakula, bata mzinga wanahitaji kuwa na uhuru wa kula majani kama sehemu ya virutubisho.
  Kabla ya kuanza ufugaji wa bata mzinga ni lazima kuhakikisha una chakula cha kutosha, kwa sababu ulishaji wa ndege hawa kadri wanavyokua huwa na gharama kubwa zaidi.
  Ni muhimu pia kujifunza kwa undani na kufahamu namna ya kutunza vifaranga wa bata mzinga kwa kuwa hufa kwa urahisi sana.
  Pia, unapaswa kujikita kutafuta soko kwa sababu wanapokua ni vigumu kuwatunza kwa muda mrefu kutokana na ukubwa wa gharama ya chakula.
  Wafugaji wachache kati ya wengi waliojaribu kuwafuga ndege hawa na kufanikiwa hata kufikia malengo yao ni kutokana na kuzingatia lishe kamili.
  Pamoja na hayo, wapo wafugaji ambao walishindwa kutokana na magonjwa pamoja na gharama ya utunzaji.

  CHAKULA
  Chakula cha bata mzinga hakina tofauti na cha kuku. Vifaranga wanahitaji kupata lishe kamili yenye protini kwa wingi ili waweze kukua vizuri.
  Vifaranga kwa siku za awali wanahitaji kiasi cha asilimia 27 ya protini mpaka wanapofikia umri wa wiki sita. Baada ya hapo mfugaji anaweza kupunguza hadi kufikia asilimia 18 na kuendelea  hadi wanapokomaa.
  Kutokana na gharama ya kununua chakula kuwa kubwa, unaweza kutumia resheni ifuatayo kwa ajili ya kutengeneza chakula cha bata mzinga wewe mwenyewe.
   Mahindi yasiyokuwa na dawa kilo 5, karanga (5), dagaa (5), mashudu (10) na chokaa (5).

  NAMNA YA KUTENGENEZA CHAKULA

  Twanga au saga pamoja kiasi cha kulainika kisha walishe vifaranga. Mchanganyiko huu hutegemeana na wingi wa bata mzinga unaowafuga.
  Hakikisha kila bata anapata chakula cha kutosha na chenye uwiano ulioelekezwa. Pia, waangalie mara kwa mara kuhakikisha wana chakula cha kutosha.

  Hifadhi chakula cha ziada kwenye mifuko au debe kisha weka sehemu isiyo na unyevu.

  Bata mzinga huanza kutaga anapofikisha umri wa mwaka mmoja. Ndege hawa wana uwezo wa kutaga kati ya mayai 15 hadi 20 kwa mara ya kwanza kisha kuatamia. Anapoendelea kukua huweza kutaga hadi mayai 30. Hii ni kulingana na lishe nzuri atakayopatiwa.
  Bata mzinga anaweza kuatamia mayai 17 hadi 20. Mayai hayo huatamiwa kwa siku 28 na huanza kuanguliwa vifaranga kwa muda wa siku tatu, kuanzia siku ya 28 hadi 31. Baada ya hapo mayai yaliyosalia bila kuanguliwa hutakiwa kutupwa kwa kuwa hayataanguliwa tena na hayafai kwa matumizi mengine.
  Baada ya vifaranga kuanguliwa, watenge na mama yao kwa kuwaweka kwenye banda safi lisilopitisha baridi. Unaweza kuwawekea taa ya kandili au ya umeme.
  Waziri Mkuu mstaafu akiangalia Bata Mzinga
  Waziri Mkuu mstaafu akiangalia Bata Mzinga, Bw, Mizengo Pinda
  BANDA
  Ni vyema banda liwe limesakafiwa au banda la asili la udongo usiotuamisha maji. Pia, unaweza kutumia banda lenye mbao au mabanzi kwa chini. Unaweza pia kutandaza maranda kwenye mabanda. Hakikisha kuta za banda zimefunikwa vizuri ili kuwakinga dhidi ya baridi.
  MAJI
  Kama ilivyo ndege wengine, bata mzinga pia wanahitaji kupatiwa maji safi na ya kutosha wakati wote. Wawekee maji katika chombo ambacho hawatamwaga na wanakifikia vizuri.
  Hakikisha maji hayamwagiki bandani kwani kwa kufanya hivyo banda litachafuka na kukaribisha magonjwa kwa urahisi. Ni vizuri kuwalisha bata mzinga vyakula vingine kama majani.
  Majani husaidia kuwapatia protini: mfano; kunde, fiwi na aina nyingine za majani jamii ya mikunde huhitajika zaidi kwa kiasi cha asilimia  25 hadi 30.

  MAGONJWA

  BATA MZINGA HUSHAMBULIWA NA MAGONJWA KAMA HOMA YA MATUMBO, MAFUA NA KUHARISHA DAMU. Wanapougua ni rahisi kuambukiza kuku, bata na ndege wengine wanaofugwa kwa haraka sana.
  Pia, ndege hawa husumbuliwa na viroboto wanaosababishwa na uchafu wa banda hasa linapokuwa na vumbi.
  CHANJO
  Bata mzinga wanatakiwa kupatiwa chanjo ya ndui (mara moja kila mwaka), kideri (kila baada ya miezi mitatu), gumboro (kwa muda wa wiki tano, ukiwapa jumatatu, basi unawapatia kila jumatatu ya wiki), na vitamini A mara baada ya kuanguliwa.
  0

  Add a comment


 13. ZIJUE SABABU ZA KUKU KUTOTAGA MAYAI
  ZIJUE SABABU ZA KUKU KUTOTAGA MAYAI
  ZIJUE SABABU ZA KUKU KUTOTAGA MAYAI: Mara nyingi wafugaji wengi wamekuwa wakilalamika ya kwamba kuku wao wamekuwa hawatagi, na wengi wao wamekuwa hawajui sababu ni hizi ndizo sababu.

  Kuku hupunguza utagaji na hata kuacha kutaga kabisa iwapo:-
  • Hawakupewa chakula bora au cha kutosha.
  • Hawapewi maji safi ya kutosha.
  • Wamebanana, yaani hawakai kwa raha.
  • Vyombo vya maji  au chakula havitoshi.
  • Mwanga hautoshi.
  • Majogoo yamezidi katika chumba(weka jogoo 1 kwa mitetea 10)
  • Kuku wanaumwa.
  • Wana vidusa vya nje na ndani (external and internal parasite).
  • Wamezeeka (umri zaidi ya miaka miwili na nusu).
  Maumbile ya kuku mwenyewe
  0

  Add a comment

 14. YAJUE MAGONJWA YA KUKU YANAYOTIBIKA KWA DAWA
  YAJUE MAGONJWA YA KUKU YANAYOTIBIKA KWA DAWA
  YAJUE MAGONJWA YA KUKU YANAYOTIBIKA KWA DAWA:

   KUHARA DAMU (coccidiosis)
   Ugonjwa huu husababishwa na virusi.
  Dalili.
  -Kuku huzubaa na kujikunyata
  -Kuku kuharisha kinyesi chenye damu au kinyesi cha kahawia
  -Kuku hudhoofika,manyoya huvurugika na kulegea mabawa na kuonekana kama wawevaa koti
  -Kuku hupungukiwa homa ya kula
  -Vifo huwa vingi kwa vifaranga
  Tiba ya ugonjwa huu.
  Wape kuku wako dawa kama Esb 3, Amprolium, au Basulfa.
  Kinga za ugonjwa huu.
  Zingatia usafi wa banda la kuku na usiruhusu unyevuunyevu katika banda la kuku.

  HOMA YA MATUMBO (Fowl typhoid)
          Husababishwa na bakteria
   Dalili za ugonjwa huu ni;
   -Kuku hupata homa kali
     -Kuku huarisha kinyesi cha kijani au njano
     -Vifo huwa vingi hasa kwa vifaranga wenye wiki 1-2
     -Kuku huzubaa,kuvimba viungo vya miguu,kuchechemea,kukosa hamu ya kula
     -Kuku wanaotaga hupunguza utagaji,hutaga mayai yenye ganda laini na hupata   vifo vya ghafla
   Tiba za ugonjwa huu.
    Dawa za oxytetracycline kama Typhoprim hutibu ugonjwa huu.
   Kinga za ugonjwa huu.
    Hakikisha usafi wa banda na vyombo vya chakula na maji kwa kuku.
    Tenganisha kuku wagonjwa na wazima

   MINYOO
  Hushambulia kuku wote wakubwa na vifaranga
   Dalili za ugonjwa huu
  -Kuku hukonda
  -Kuku huarisha
  -Kuku hukohoa
  -Kuku hupunguza utagaji
  -Kuku hudumaa katika ukuaji/hawakui vizuri
  -Kuku hupungua uzito
  Tiba za ugonjwa huu.
  Tumia dawa za minyoo kama piperazine
  Kinga za ugonjwa huu.
  Wapewe dawa za minyoo mara kwa mara kila baada ya miezi mitatu\

  VIROBOTO/CHAWA/UTITIRI
     Hushambulia sana vifaranga na hutokea vifo kwa wingi kwa vifaranga Kwa kuku wakubwa tatizo halionekani kwa sana lakini nao huathiriwa sana.
  Dalili za ugonjwa huu.
   -Kuku kutochangamka
   -Ukuaji mdogo wa kuku
   -Kuku kutotaga na kuhatamia vizuri kutokana na kusumbuliwa na chawa,utitiri au  viroboto
   -Viroboto huonekana kuganda machoni wakinyonya damu
  Tiba za ugonjwa huu
  Tumia dawa za unga kama sevin dust 5% ,Malathion ,akheri powder kwa kuku wote na mabanda yao.
  Kinga za ugonjwa huu.
   Boresha usafi wa mabanda ya kuku.
  0

  Add a comment

 15. NAMNA YA KUZUI KUKU ANAYEDONOA MAYAI YAKE
  NAMNA YA KUZUI KUKU ANAYEDONOA MAYAI YAKE
  NAMNA YA KUZUI KUKU ANAYEDONOA MAYAI YAKE: Kuku wengi wamekuwa na tabia za kudonoa mayai ambayo wameyataga wenyewe au ambayo yametagwa na kuku wengine, hivyo pindi uonapo tabia hii katika kuku wako unatakiwa kufanya yafutayo ili kukomesha tabia hii:
  1. Kuweka idadi ya kuku inayolingana na sehem ulionayo.
  2. Usizidishe mwanga.
  3. Banda liwe safi.
  4. Weka vyombo vya kutosha.
  5. Wape lishe bora.
  6. Wape kuku shughuli kwa kuwawekea bembea na sehem ya uwazi kwa ajili ya mazoezi.
  7. Kata midomo ya juu.
  8. Epuka ukoo wenye tabia hizo.
  0

  Add a comment


 16. KILIMO BORA CHA UFUTA
  KILIMO BORA CHA UFUTA
  KILIMO BORA CHA UFUTA: Ufuta ni zao linalolimwa kwa wingi katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma, Pwani, Morogoro, Dodoma, Tanga na ukanda wa chini katika mikoa ya Rukwa na Mbeya. Zao hili hulimwa kwa ajili ya chakula na biashara. Mbegu za zao hili huwa na wastani wa mafuta kiasi cha asilimia 45.

  MAMBO YA KUZINGATIA WA KATI WA KUZALISHA MBEGU 
  1. Chagua aina ya mbegu inayotoa mazao mengi na bora, inayovumilia mashambulizi  ya magonjwa na wadudu, inayokomaa mapema na kutoa mafuta mengi.

  1. Chagua mbegu inayokomaa kwa pamoja ili kurahisisha uvunaji na pia kuepuka upotevu wa zao shambani.

  1. Aina nyeupe ya mbegu ya ufuta hupendelewa zaidi kuliko aina nyeusi.

  UPANDAJI
  Panda mbegu nusu inchi chini ya udongo, inchi sita umbali wa mbegu na mbegu na futi mbili nafasi ya msitari na msitari, kabla ya kupanda hakikisha ardhi imelowana vya kutosha na upande mbegu masaa mawili au matatu baadae

  MBOLEA
  Ufuta unahitaji rutuba ya kutosha ili kutoa mazao bora. Katika kudumisha rutuba ya udongo, tumia kilimo cha mzunguko wa mazao au weka mbolea za asili pale inapobidi.

  PALIZI
  Dhibiti magugu kwa kupalilia ili kuruhusu ufuta kutumia vizuri unyevu na virutubishi. Magugu mengine huwa ni maficho ya wadudu waharibifu wa zao la ufuta.

  MAGONJWA NA WADUDU
  Ufuta hushambuliwa na magonjwa na wadudu mbalimbali ambao huweza kusababisha upungufu na ubora wa mazao. Hivyo kagua shamba mara kwa mara hasa kwenye maua na mapodo ili kuona dalili za mashambulizi. Endapo kuna dalili zamashambulizi, chukua tahadhari mapema kabla ya uharibifu mkubwa haujatokea.

  MAANDALIZI KABLA YA KUVUNA 
  1. Kagua shamba kuona kama ufuta umekomaa,  Ufuta hukomaa, kati ya miezi mitatu na   minne tangu kupanda kutegemea aina.
  2. Aina ya ufuta usiokuwa na matawi hukomaa mapema kuliko ile yenye matawi.
  3. Ni muhimu kuwahi kuvuna ili kuepuka ufuta kupukutikia shambani.

   DALILI ZA KUKOMAA UFUTA SHAMBANI
  • Kwa kawaida majani hubadilika rangi kutoka kijani na kuwa ya manjano na hatimaye kudondoka.
  • Mashina hubadilika rangi kutoka kijani na kuwa ya kahawia.

  VIFAA VYA KUVUNIA
  • Kamba
  • Siko
  • Panga

  VIFAA VYA KUKAUSHIA
  • Sehemu ya kukaushia yenye Sakafu ya saruji
  • Maturubai
  • Sakafu safi

  KUVUNA
  1. Vuna ufuta mapema kabla mapodo kukomaa sana na kuanza kupasuka na kuachia punje.Mapodo ya ufuta yaliyokomaa sana yakiguswa au kutikiswa na upepo hupasuka na kuachia mbegu, hali inayosababisha upotevu mkubwa.

  1. Mbegu za ufuta ni ndogo na zikidondoka chini ni vigumu kuziokota. Vilevile mbegu zilizodondoka ni vigumu kuzitenganisha na uchafu.

  1. Kwa aina za ufuta zenye mapodo yanayopasuka, uvunaji ufanyike wakati mimea bado ni kijani ili kuepuka upotevu wa mbegu.

  1. Aidha uvunaji ufanyike wakati hakuna upepo wala jua kali.

  1. Baada ya kukata mashina yafunge katika mizigo midogo na kuweka katika vyombo vya kusafirisha kama vile mikokoteni, matela au magari hadi sehemu ya kukaushia.

  1. Panga mizigo midogo kwa kusimamisha katika malundo madogo yasiyozidi mizigo minane kwenye sehemu safi za kukaushia.

  KUKAUSHA
  Mapodo ya ufuta hukaushwa yakiwa yamefungwa katika vitita. Vitita huwekwa kwa kuegeshwa kwenye fremu ya kukaushia kwa muda wa wiki mbili hadi tatu kutegemea hali ya hewa. Fremu hii huwekwa juu ya turubai au sakafu ili kuzuia upotevu wa punje kutokana na kupasuka kwa mapodo.

  KUPURA
  Upuraji hufanyika kwenye turubai, mkeka au kwenye sakafu safi.
  • Vitita hupigwa taratibu kwa kutumia mti au hutikiswa vikiwa vimegeuzwa vichwa chini ili kuruhusu punje za ufuta kudondoka kwenye sakafu safi au turubai.

  KUPEPETA NA KUPEMBUA
  Kupepeta na kupembua hufanywa ili kuondoa takataka kama vile mawe, vipande vya mapodo,vijiti na vumbi. Njia bora ya kupepeta na kupembua ni kwa kutumia mikono.
  Ufuta huwekwa kwenye vyombo kama vile ungo kwa kiasi cha kilo mbili hadi tatu. Ufuta hurushwa hewani kwa kasi ndogo na takataka nyepesi huchukuliwa na upepo. Zile nzito huondolewa kwa mikono.

  KUFUNGASHA
  Mbegu za ufuta zilizo safi huwekwa kwenye vifungashio kama vile magunia madogo ya aina ya juti ya ujazo wa kilo 50. Fungasha mbegu za ufuta kwenye magunia yenye uzito usiozidi kilo 50. Kabla ya kufungasha hakikisha mbegu zimekauka hadi kufikia unyevu wa asilimia 10.

    KUHIFADHI
  • Panga magunia ya ufuta juu ya chaga.
  • Panga kwa kupishanisha ili kuruhusu mzunguko wa hewa kati ya magunia.

  KUSINDIKA MBEGU ZA UFUTA
  Ufuta husindikwa kupata bidhaa ya mafuta ambayo hutumika katika mapishi mbalimbali. Mafuta hukamuliwa kwa kutumia njia za asili na kwa kutumia mashine. Njia za asili zina ufanisi mdogo ukilinganisha na zile za kukamua kwa mashine, hivyo ni vyema kutumia mashine. Kuna mashine za aina mbili zinazotumika kukamua mafuta; mashine za mkono na zile zinazoendeshwa kwa injini au mota ya umeme. Mashine za mikono zinazotumika zaidi hapa nchini ni za aina ya daraja (Bridge press) na Ram.

  MATUMIZI
  Mafuta ya ufuta hutumika katika mapishi mbalimbali ili kuongeza ladha. Pia husaidia kuleta nguvu na joto mwilini. Mbegu za ufuta huchanganywa na vyakula mbali mbali kama mikate, keki, mboga na kadhalika
  0

  Add a comment

 17. JINSI YA KUANDAA CHAKULA CHA KUKU
  JINSI YA KUANDAA CHAKULA CHA KUKU
  JINSI YA KUANDAA CHAKULA CHA KUKU : Somo hili ni  mahususi kwa ajili ya wafugaji wote wa kuku, au kwa wale wote ambao wanapenda kufuga kuku. Kwani mfumo huu ni mzuri na humsaidia mfugaji kuweza kutengeza chakula ambacho kina virubishio vyote ambavyo ni muhimu kwa kuku.

  JINSI KUANDAA CHAKULA CHA KUKU KUANZIA WIKI LA 1- HADI WIKI LA 8.
  Mahitaji.
  1. Pumba 60kg
  2. Mahind ya kuparaza 10kg
  3. Mashudu alizeti 10kg
  4. Dagaaa 15kg
  5. unga wa mifupa 5kg
  6. Chumvi ½
  7. premix ¼
  Mara baada ya kuanda mahitaji hayo changanya vyote ili kupata mchnganyiko wa chakula.

  CHAKULA CHA KUKU, KUANZIA WIKI LA NANE NA KUENDELEA.
  Mahitaji
  1. Pumba ya mahindi yenye chenga- kg 38
  2. Mashudu ya alizeti- kg 7.5
  3. Mabaki ya dagaa – kg 1.5
  4. Chokaa ya kuku – kg 0. 5
  5. Unga wa mifupa – kg 0.5
  6. Lusina – kg 2
  7. Chumvi – kg 0.25
  Mara baada ya kuanda mahitaji hayo changanya vyote ili kupata mchnganyiko wa chakula.
  0

  Add a comment

 18. KILIMO BORA CHA KAROTI
  KILIMO BORA CHA KAROTI
  KILIMO BORA CHA KAROTI : Karoti ni zao la mbogamboga ambalo ni zao mizizi, kwa kawaida hupatikana katika rangi ya machungwa,  nyekundu, njano. Karoti za sasa zimetokeza kutokana na karoti pori, Daucus carota. Karoti hutumika sana kwaajili ya kuongeza radha kama kiungo kwenye mboga au kwenye kachumbari na pia zinafaida kubwa katika mwili kwa kukupatia vitamin A na C pamoja na madini ya chuma hasa pale mtu atafunapo.

  HALI YA HEWA NA UDONGO.
  Karoti zinahitaji hali isiyokuwa na joto sana, wala baridi sana, kati ya nyuzi za degree 15 mpaka 27 za sentigredi. Kama ukanda wa pwani una joto kali, inatakiwa karoti zilimwa miezi ya majira ya baridi, karoti zinazotoka mazingira ya baridi huwa na radha nzuri pamoja na harufu nzuri. Udongo wa kichanga chepesi na tifutifu ndio unafaa katika kilimo cha karoti, udongo wa mfinyanzi na udongo mzito hudumaza mazao.


  UTAYARISHA WA SHAMBA
  Karoti zinahitaji Shamba la Karoti lilimwe kwa trekta, kwa ng’ombe ama kwa jembe la mkono kwa kina cha sentimita 30 hadi 45 kwenda chini ya ardhi. Mkulima anatakiwa kuandaa matuta yenye mwinuko wa kimo cha sentimita 28 – 40 kwenye shamba, na upana wa mita 1, pia mita 1.5 umbali wa tuta moja hadi lingine. Kwa maandalizi mazuri tengeneza mifereji midogo ya kusiha mbegu za karoti yenye umbali wa sentimita 15- 20, mifereji minne kwa tuta.

  MBEGU
  Jinsi ya kujua mbegu nzuri zenye uwezo wa kukua bila wasiwasi. Mbegu zenye uwezo wa kuota hutoa harufu kali unapozifikicha. Zilizopoteza uwezo wa kuota huwa hazitoi harufu yoyote. Ili mbegu ziote haraka ziloweke katika maji kwa muda wa saa 24. Baada ya hapo changanya mbegu hizo na mchanga, kwa kiasi kinacholingana ili kupata mtawanyiko mzuri wa mbegu wakati wa kupanda/kusia.


  UPANDAJI
  Inahitajika uoteshe kwenye kitalu ndipo uhamishie shambani.
  Weka mbegu katika chupa ya milimita 100 na toboa kidogo mfuniko, baada ya hapo Sia mbegu katika mifereji ya kupandia kwa kutikisa chupa yenye mbegu, ndipo, Funika mbegu kwa kutumia mboji au mchanga, ukimaliza Nyunyiza maji ya kutosha, Funika tuta na plastiki nyeusi, hatua nyingine Kandamiza plastiki kwa pembeni na kwa mabonge ya udongo ili isipeperushwe na upepo.
  Mbegu huota baada ya siku 3-5 kutegemea na hali ya hewa. Inakupasa kukagua shamba mara tatu kwa siku. Baadaye Ondoa plastiki mara moja pindi utakapoona mbegu moja tu iliyoota. Usicheleweshe kuondoa plastiki husababisha miche inayoota kufa kwa kuunguzwa na joto lililo katika plastiki. Hapo tayari kwa kupanda shambani.
  Upandaji wa moja kwa moja shambani katika matuta au sesa.
  Kiasi cha kilo 8 za mbegu kinatosha kupandwa kwenye Hekta moja.


  MBOLEA
  Weka mbolea aina za asili (samadi au mboji) mwanzoni, ila kama haukutumia mbolea ya samadi au mboji, weka mbolea ya S/A kilogramu 100 kwa hekta kama haukutumia mbolea za asili, kama ulitumia mbolea za asili basi weka kilogramu 50 kwa hekta. kisha tumia NPK wiki sita baada ya kupanda. Matumizi ya mbolea za maji yafanyike kila baada ya wiki mbili kutegemea na mahitaji

  UPALILIAJI & UNYEVU
  Ili kupata mavuno mengi palilia shamba mara kwa mara ili kuhakikisha shamba halina magugu na nyasi kwa kung’olea kwa mkono, jembe na mangineyo, na kwenye udongo hakikisha kuna unyevu wa kutosha kama sio kipindi cha mvua inatakiwa umwagilie shamba lako kwa wiki mara mbili.

  MAGONJWA NA WADUDU WAHARIBIFU WA ZAO HILI

  MAGONJWA ;
  1. Madoajani (Leaf Spot):
  Ugonjwa huu husababishwa na ukungu na hutokea wakati karoti zina urefu wa sentimita 13 mpaka 15. Hushambulia majani na kuyafanya yawe na madoa yenye rangi nyeusi iliyochanganyika na kijivu au kahawia. Sehemu zinazozunguka madoa haya hubadilika rangi na kuwa njano.
  Ugonjwa ukizidi majani hukauka.

  Zuia ugonjwa huu kwa kunyunyizia dawa za ukungu kama vile Dithane-M 45, Blitox, Copperhydroxide (Kocide), Copper Oxychloride, Cupric Hydroxide (Champion), Antrocol, Topsin M- 70% na Ridomil.

  1. Kuoza Mizizi (Sclerotinia Rot).
  Ugonjwa huu husababishwa na ukungu na hushambulia mizizi namajani. Dalili zake ni kuoza kwa mizizi na majani. Baadaye sehemu hizi hufunikwa na uyoga mweupe. Kwenye uyoga huu huota siklerotia kubwa zenye rangi nyeusi.


  ZUIA UGONJWA HUU KWA KUZINGATIA YAFUATAYO:-
  • – Epuka kustawisha karoti kwenye maeneo yaliyoshambuliwa na ugonjwa huu.
  • – Nyunyuzia dawa za ukungu kama vile Dithane M- 45, Blitox, Topsin – M 70% na Ridomil.


  1. Madoa Meusi (Black Leaf Spot):
  Huu pia ni ugonjwa wa ukungu unaoshambulia majani na mizizi. Majani yaliyoshambuliwa huwa na rangi ya manjano ambayo baadaye hubadilika na kuwa kahawia. Mizizi huwa na madoa meusi yaliyodidimia. Ugonjwa huu unaweza kuzuiwa kwa kutumia mbegu zilizothibitishwa kitaalamu, kubadilisha mazao na kuepuka kujeruhi karoti wakati wa kupalilia, kuvuna au kusafirisha.

  WADUDU WAHARIBIFU WA ZAO HILI
  1. Minyoo Fundo:
  Minyoo hii hushambulia mizizi na kuifanya iwe na vinundu. Hali hii husababisha mmea kudumaa na kupunguza mavuno. Minyoo fundo huweza kuzuiwa kwa kubalidilisha mazao. Baada ya kuvuna usipande mazao ya jamii ya karoti au mazao yanayoshambuliwa na wadudu hawa. Unaweza kupanda mazao ambayo hayashambuliwi na minyoo fundo kama vile mahindi. Pia hakikisha shamba ni safi wakati wote.

  1. Imi wa Karoti:
  Mashambulizi hufanywa na funza ambaye hutoboa mizizi. Ili kuzuia wadudu hawa tumia dawa kama vile Dichlorvos, Sapa Diazinon na Fenvalerate. Pia badilisha mazao na wakati wa kupalilia pandishia udongo kufunika mizizi.

  1. Karoti Kuwa na Mizizi Mingi (Folking);
  Hii hutokea kama karoti zimepandwa kwenye udongo wenye takataka nyingi na usiolainishwa vizuri. Vile vile utumiaji wa mbolea za asili zisizooza vizuri unaweza kusababisba karoti kuwa na mizizi mingi. Hali hii inaweza kuzuiwa kwa kulainisha udongo vizuri na kutumia mbolea za asili zilizooza vizuri.

  UVUNAJI
  Karoti hukomaa baada ya wiki 11 mpaka 13 kutoka mda ilipokuwa imepandwa kulingana na hali ya hewa ya eneo ilipolimwa, tani 15 hadi 25 za karoti huvuna katika hekta moja.

  SOKO
  Karoti inatumika sana na watu mbalimbali, tafuta soko pale unapoona karoti zako zimekaribia kukomaa. Ulizia wanunuzi ni bei gani wataweza kuchukua pia kiasi gani watachukua.

  Asante kwa kusoma mafundisho haya.
  0

  Add a comment

 19. KILIMO BORA CHA PILIPILI MBUZI
  KILIMO BORA CHA PILIPILI MBUZI
  KILIMO BORA CHA PILIPILI MBUZI : Pilipili mbuzi ni zao ambalo linaweza kulimwa kibiashara na kumpatia faida nzuri mkulima. Zao hili huitaji mwanga wa kutosha wa jua angalau kiasi cha masaa 6 kwa siku.
  Pilipili hustawi vizuri zaidi kwenye udongo wenye mbolea ya asili, undongo wenye unyevu nyevu ila usiwe wenye kutuamisha maji.

  Pilipili mbuzi huitaji udongo wenye pH 6.0 hadi 6.8, Ikiwa pH ni chini ya 6.0 ongezea madini chokaa kwenye udongo; Na ikiwa pH ya udongo imefika 8 onana na wataalam wa kilimo wakusahuri namna ya kuipunguza.

  Kuandaa miche.
  Mbegu za pilipili huoteshwa miche kwenye kitalu kabla ya kwenda kupandikizwa shambani. Pandikiza mbegu kwenye kitalu week 7 hadi 10 kabla ya kipindi ambacho umepanga kupandikiza miche shambani. Panda mbegu tatu tatu kwenye kila kishimo na chagua mbili zilizo chipua vizuri kwa ajili ya kuhamishia shambani.

  Kuhamishia miche shambani.
  Hamisha miche shambani ikiwa imetengeneza majani 8, ingawa kuhamisha ikiwa na majani machache au mengi zaidi haitapelekea shida yoyote.

  MUHIMU…Unashauriwa kuhamisha miche shambani kwa kuzingatia mambo yafuatayo.

  • Siku ya kwanza kwa lisaa limoja weka miche kivulini au mahali ambapo kuna kizuizi jua la moja kwa moja lisiifikie miche. Kadri siku zinavyo kwenda ruhusu miche kupata mwanga wa jua zaidi.

  • Chimba mashimo marefu kuzidi urefu wa mizizi ya miche kisha changanya vyema udongo na mbolea ya Ngo’ombe. Muda mzuri wa kuhamisha miche yako shambani ni jioni au kipindi ambacho jua limefifia kuepuka miche kukauka.

  • Changanya sulphur (Tembe 2) kwenye maji na kumwagilia na rudia mchanganyo huu kila baada ya week mbili. Sulphur husaidia kuuwa fungus, inauwa bacteria wasio faa, kuzuia magonjwa pia huasaidi mizizi kusambaa na kukua kwa haraka na kupata virutubisho.

  • Mwagilia miche maji ya kutosha baada ya kuihamishia shambani hiyo husaidia kupunguza stress za mmea unapobadilishiwa mazingira. Tumia mbolea ya Miracle Gro kila baada ya week mbili.

  Mahitaji ya mmea.
  Pilipili ni zao lenye kuhitaji zaidi unyevu unyevu shambani ila maji yasiwe yenye ktuama. Kipindi ambacho maua yametoka na vitunda vya pilipili vimeanza kujitokeza, udongo ukiwa mkavu sana hauna unyevu wa kutosha hupelekea maua kudondoka. Epuka umwagiliaji ulio zidi mahitaji au ulio chini ya mahitaji. Unaweza kutandaza nyasi kwaajili ya kusaidia kuhifadhi unyevu shambani. Mmea huanza kutoa maua mapema baada ya kutengeneza matawi, Maua ya mmea hua na set iliyo kamilika (jike na dume) hivyo kuwa na sifa ya kuweza kujichavusha yenyewe.

  Upepo, wadudu au kwakutumia mkono husaidia kuongeza uchavushaji.

  MBOLEA
  Siku 10 Baada ya kupanda sasa endelea kukuzia mbolea,wakati huu tumia Yaramila winner 5-10g kwa mche.NB:Usitupie juu..hakikisha mbolea unaifukia kuzunguka mmea na usiweke karibu sana na mmea,weka 4-6 cm kutoka kwenye mmea.

  Na kila baada ya siku 21 weka mbolea aina ya Yaramila winner au NPK Isipokuwa wakati maua yameanza weka Yaramila nitrabo au CAN 10g /plant,na baada ya hapo utaendelea na Y-winner mpaka mwisho wa mavuno.

  KUPALILIA
  Pilipili zi zao ambalo halina mizizi merefu sana, hivyo basi mkulima anapaswa kuzingatia hilo na kuongeza umakini wakati wa kupalilia kuepuka kukata mizizi.

  MAGONJWA


  1. Fusarium wilt (Mnyauko)
  Njinsi ya kuepuka. .Tandika shamba lako na majani makavu ili kupunguza joto.

  • Ng’oa mimea yote iliyougua na choma moto mabaki.
  • Epuka kusambaza ugonjwa kwa kusafisha vizur vifaa vya shamba na chini ya miguu uingiapo shambani.
  • Jitahidi mimea iwe na afya nzuri kwa kuweka mbolea na maji ya kutosha.
  • Pulizia dawa ya fangas kama vile ortiva.

  2) Southern blight ( Sclerotium wilt)
  Huu ungonjwa utaona kwenye shina china panaota fangasi weupeweupe (Whitish fungal growth on the stems of infected plant) .Majani ya chini huweza kunyauka,Huu ungonjwa hutokea muda mfupi kipindi cha joto kali.
  Kuepuka/Kuzuia.

  • Wakati wa kulima ..lima hadi chini sana ili hao fangasi waende chini sana ambapo mizizi haifiki.
  • Mimea iliyoshambuliwa…Ing’oe yote na choma moto lakini chomea nje ya eneo la shamba.
  • Pulizia Ortiva.

  3) Anthracnose.
  Huu ni ugonjwa wa kawaida kwenye pilipili mbuzi na huu ugonjwa huweza kukaa ardhini muda mrefu.Dalili zake utaona matunda kama kuna sehemu zinakuwa nyeusi na panajaa majimaji …dalili hii huenea sehemu kubwa ya tunda na baadaye tunda huoza.

  Kuepuka.
  Kuepuka ugonjwa kujirudia musimu na musimu..Baada ya kuvuna choma mabaki yote.
  • Shamba ambalo ulilima pilipili usirudie kulima pilipili mfululizo zaidi ya mara mbili…badilisha zao kwa kupanda zao ambalo sio jamii moja na pilipili mbuzi (Do crop rotation).
  • Pia huu ugonjwa huweza kupitia mbegu…kwa hiyo mkulima lazima achukue mbegu kutoka kwa wakala aliyeidhinishwa na mwaminifu…mbegu hazitakiwi kutengenezwa kutoka kwenye mimea iliyoathirika na ugonjwa.

  4) Bacteria.
  Madoamadoa ya bacteria kwenye matunda….huweza kutokea na kusambaa haraka wakati wa joto kali na unyevu kwenye udongo.Pia huu ugonjwa huweza kuenea kupitia mbegu.

  Dalili zake utaona madoamadoa ya kama brown chini ya majini na pia kwenye matunda.
  Kuepuka.
  • Usitengeneze mbegu kutoka kwa mimea iliyoathirika na huu ugonjwa.Nunua kutoka kwa wakala.
  • Pulizia dawa yoyote copper.

  5) Virusi.
  Kuna aina nyingi ya virusi ambao hushambulia pilipili mbuzi.
  Dalili zake ni majani kuwe ba njano na kujikunja .

  Kuepuka.
  • Nunua mbegu bora
  • Pulizia dawa za wadudu kuanzia kwenye kitaru na kuendelea.Wadudu wanaosababisha virus sanasana na wadudu mafuta (Aphids) kwa hiyo akikisha muda wote shambani hakuna hao wadudu kwa kupulizia Actara.
  NB:Pamoja na maelezo yote hapo juu.Usikae zaid ya siku 14 bila kupiga dawa ya wadudu na ukungu/fangasi hata kama hakuna ugonjwa.

  Wadudu.
  Pilipili mbuzi hushambuliwa na ;

  1. Wadudu mafuta ( Aphids)
  Kuwadhibiti.
  Tumia Actara 8g/20L.
  Au tumia wadudu wanaokula wadudu mafuta,mfano special beetles.

  1. Crickets
  Hawa wadudu hukaa aridhini karibu na mmea na usiku hutoka walipo jificha na kukata miche michanga.
  Kawadhibiti.

  Unapo andaa shamba andaa vizur ili nyumba zao zife na kuwaacha katka halu ya hatari ya kuliwa na ndege na wadudu wengine ,kama ni miche na iko kwenye tray…basi weka hizo tray juu ya kichanja.

  1. Beetle.
  Tuma Karate 40cm/20L.

  1. Utitiri
  Dawa:Tumia Dynamec au yoyote yenye Abamectin.

  1. Nematodes 
  Tumia solvigo.

  Mavuno.
  Pilipili huwa tayari kwa kuvunwa siku 60 hadi 95 kutegemea na aina ya mbegu uliyotumia. Chuma kwa uangalifu bila kung’oa mmea ili uendelee kuzalisha. Muvuno yanaweza kudumu kwa muda wa mwezi 1 hadi 3.

  Usalama wakati wa uvunaji.
  Pilipili huwa na kemikali iitwayo capsaicinoids ambayo inaweza
  kukuwasha kwenye ngozi au kwenye macho ikiwa utajigusa. Vaa gloves wakati wa kuvuna na kuwa mwangalifu usijiguse kwenye macho.

  SOKO
  Fursa
  Pilipili ni zao ambalo halina mbadala wake au (substitute) hivyo kufanya mahitaji yake kuwa ni ya muda wote bila kutetereka.

  Changamoto
  Muda ambao wakulima wengi wanakuwa wamezizalisha zaidi huathiri sana soko la pilipili kwa maana hata bei ikishushwa sana haiwezi kushawishi watumiaji kutumia pilipili nyingi zaidi.
  Kuepuka changamoto hiyo wakulima wanashauriwa kupunguza huduma shambani hadi pale soko litakapo tengemaa vizuri.

  Mbinu za mafanikio kwenye kilimo hiki.
  1. ZALISHA KWA WINGI
  Uzalishaji mkubwa husaidia sana kupunguza gharama ambazo haziepukiki yani (Fixed Cost). Ukizalisha kwa wingi kwa gharama ndogo utaweza pia uza bidhaa zako kwa bei ndogo na bado utapata faida nzuri na kujihakikishia soko la uhakika kwa bidhaa zako.

  1. TAFUTA MASOKO YA BIDHAA KABLA YA KUANZA UZALISHAJI
  Mkulima mwenye mafanikio ni lazima pia awe mfanya biashara mzuri ukiachilia mbali kuwa mzalishaji mzuri. Mkulima ni vyema kutengeneza channels mapema kupata wateja wa mazao yako. Ukizalisha kwa wingi kwa gharama ndogo itakusaidia sana kwenye kupata masoko utakwa na ushawishi zaidi kwa wateja. Tengeneza wateja na wateja watakutengenezea biashara.
  Mteja anataka vitu vitatu vya msingi.
  • Unafuu wa bei
  • Ubora wa zao
  • Upatikanaji wa uhakika wa bidhaa
  Ukijihakikishia hivyo vitu vitatu hapo juu hapana shaka utakuwa umejihakikishia soko la uhakika.

  1. USILIME KWA KUFUATA MSIMU
  Unapolima kwa kufuata msimu, mtajikuta wakulima wengi mmezalisha zao fulani kwa wiiingi kwa kipindi kimoja hivyo kupelekea upatikanaji wa zao hilo kuwa mkubwa kuliko inavyo hitajika kwenye masoko, jambo hili hupelekea mazao kuuzwa kwa bei ndogo na kupelekea wakulima kukosa faida ya kutosha au hata kupata hasara muda mwingine.
  Unapolima kwa kutofata msimu mkulima utaweza kuazalisha zao/mazao kipindi ambacho wengine hawazalishi hivyo mahitaji yatakuwa makubwa na upatikanaji wa zao hilo utakuwa ni mdogo hivyo mkulima ataweza kupanga bei nzuri kwa mazao yake.

  1. USIFANYE KILIMO KWA MAZOEA
  • Tumia wataalamu wa kilimo
  • Tumia njia za kisasa za kilimo
  • Fanya utafiti wa ardhi dhidi ya zao unalotaka kufanya (Tumia wataalamu)
  • Fanya kilimo cha umwagiliaji uweze kuzalisha kipindi ambacho wengine hawawezi kuzalisha ili uuze mazao yako kwa bei nzuri zaidi,


  FAIDA ZA KUTUMIA PILIPILI
  1. Pilipili inasaidia sana kusawazisha sukari kwenye damu.

  1. Ulaji wa pilipili kunaweza kunawasaidia sana watu wanene (overweight) au wanao ugua ugonjwa wa kisukari. Hii ni kwa mujibu wa timu ya watafiti katika Chuo Kikuu cha Tasmania, utafiti iliyochapishwa katika American Journal of Clinical Nutrition, mwezi Julai 2006.

  1. Utafiti huo pia umeonyesha kwamba kawaida ya kula Pilipili kunaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti na kusawazisha insulini kwa 60%. baada ya kula chakula.

  1. Pilipili husaidia kupunguza maumizi na uvimbe kwenye tezi na vilevile huwasaidia wagonjwa wa rheumatoid na arthritis kupata nafuu. Vile vile husaidia kuondoa mkusanyiko wa damu sehemu moja ya mwili.

  1. Pilipili husaidia kufungua kwa haraka na kwa ufanisi pua zilizoziba kwa mafua, kuruhusu kupumua kwa urahisi zaidi.

  1. Pilipili pia husaidia kupunguza upatikanaji wa saratani ya kwenye tumbo (Stomach Cancer).

  1. Pilipili husaidia kuongezeka kwa kiwango cha metabolic, ambayo husaidia kuchoma mafuta, ulaji wa pilipili kunaweza kuinua kiwango na metabolic yako hadi 23% ndani ya masaa 3.

  8. Kula pilipili husaidia kupunguza cholesterol, na kupunguza kiasi cha fibrin katika damu
  1

  View comments

 20. JINSI YA KUTENGENEZA CHAKULA CHA SAMAKI
  JINSI YA KUTENGENEZA CHAKULA CHA SAMAKI
  JINSI YA KUTENGENEZA CHAKULA CHA SAMAKI : Mfugaji anaweza kupunguza gaharama za kununua chakula kwa ajili ya samaki, kwa kutengeneza chakula mwenyewe kwa kutumia malighafi ulizo nazo katika eneo lako. Tumia resheni rahisi ambayo itakupatia chakula cha kutosha na kwa gharama nafuu.

  MAHITAJI
  1. Pumba ya mahindi sadolini 1.
  2. Pumba ya ngano au mpunga sadolini 1.
  3. Dagaa sadolini 1.
  4. Kilo moja ya soya.
  5. Robo kilo ya mashudu ya pamba au alizeti.

  NAMNA YA KUANDAA
  1. Changanya malighafi hizo kwa pamoja.
  2. Saga hadi zilainike.
  3. Kanda kama vile unga wa kutengenezea chapati.
  4. Weka kwenye mashine ya kusaga nyama au kutengenezea tambi.
  5. Anika kwenye jua la wastani.
  6. Baada ya kukauka, vunja vunja kwenye vipande vidogo vidogo hasa kwa kuzingatia umri wa samaki unaokusudia kuwalisha.
  7. Tumia lishe hiyo kwa samaki mara tatu kwa siku.
  0

  Add a comment

 21. NAMNA YA KUTUNZA KUMBUKUMBU KATIKA UFUGAJI WA KUKU
  NAMNA YA KUTUNZA KUMBUKUMBU KATIKA UFUGAJI WA KUKU
  NAMNA YA KUTUNZA KUMBUKUMBU KATIKA UFUGAJI WA KUKU : Kwa mfugaji yeyeote yule wa kuku ni lazima aweze kujijengea utaratibu wa kuandika na kutunza kumbukumbu wa kuku wake. Usipo kuwa na utaraitibu huo, jiandae kusikia ule usemi usemao.”mali bila daftari hupotea bila habari“. Hivyo ni vyema  ukiwa na mradi wowote wa ufugaji ni vema ukiwa unaweka kumbukumbu za kila siku au kwa kila wiki.

  KATIKA KUTUNZA KUMBUKUMBU ZA UFUGAJI KUNA MAMBO MUHIMU YA KUYAZINGATIA KAMA IFUATAVYO:-

  1. Kumbukumbu za kuku na uzalishaji
  Hii ni kuanzia unapowapokea hadi kuwatoa bandani. Hapa unapaswa kila siku uwaangalie kuku wako ili kujua wanahali gani na ni wangapi waliopo, hapo utaelewa kama kuna ugonjwa wa kutibu au tahadhari gani zichukuliwe.
  kama ni kuku wa mayai basi kujua idadi ya mayai wanyotaga kila siku, ili uweze kujua asilimia za utagaji na uweze kupima kiwango chao cha utagaji.

  1. Kumbukumbu za chanjo.
  Weka kumbukumbu za chanjo dhidi ya magonjwa mbalimbali kama vile mdondo (Newcastle), gumboro, ndui na magonjwa mengine.

  1. Kumbukumbu za afya.
  Hapa unarekodi kila aina ya ugonjwa uliotekea bandani, idadi ya walioathirika, waliotibiwa, waliopona na waliokufa. Gharama za matibabu nazo pia ziwekwe kwenye kumbukumbu.

  1. Gharama za vifaa na chakula.
  Vifaa vyote unavyonunua kwa ajili ya ufugaji ni lazima viorodheshwe na viwekwe kwenye kumbukumbu, na gharama za chakula kuanzia unapoingiza kuku hadi unapowatoa iwekwe kwenye kumbukumbu pia.

  MUHIMU: Njia rahisi ya kutunza kumbukumbu ni kununua daftari na kutengeneza majedwali yanayoonesha vipengele tajwa hapo juu
  0

  Add a comment

 22. YAFAHAMU MAGONJWA MAKUU YANAYOSHAMBULIA KAHAWA
  YAFAHAMU MAGONJWA MAKUU YANAYOSHAMBULIA KAHAWA
  YAFAHAMU MAGONJWA MAKUU YANAYOSHAMBULIA KAHAWA : Kilimo cha kahawa kimekuwa kikiwanufaisha wakulima ambao wanalima kilimo hicho kwa kiwango kikubwa , lakini licha ya kuendelea kuwanufaisha wakulima hao, lakini ipo changamoto kubwa ambayo imekuwa ikiwakabili wakulima hao, na changamoto hiyo si nyingine bali ni changamo ya mogonjwa,

   Hivyo  siku ya leo naomba tuangalie japo kwa uchache magonjwa ambayo huathiri kilimo cha kahawwa na namna ya kujikinga na magonjjwa hayo;

  Magonjwa makuu ya kahawa ni haya yafuatayo
  1. Chule buni (CBD)
  2. Kutu ya majani (Coffee leaf rust)
  3. Mnyauko fuzari (Fusarium)
  CHULE BUNI (CBD- Coffee Berry Disease)
  CHULE BUNI (CBD- Coffee Berry Disease)
  Leo nitaongelea ugonjwa wa chule buni

  CHULE BUNI (CBD- Coffee Berry Disease)
  Chule Buni (CBD) ni ugonjwa wa matunda ya kahawa ambao umeenea sehemu nyingi nchini hasa zile za miinuko ya juu. Ugonjwa huu husababishwa na fangas wajulikanao kama colletotrichum kahawae. Ushambuliaji huwa ni mkubwa zaidi wakati wa mvua za masika kwani wakati huu hali ya unyevu unyevu kwenye hewa ni mkubwa na hali ya hewa ni ya baridi.

  MFANO WA TUNDA LILISHAMBULIWA

  MADHARA
  Ugonjwa huu ni mbaya sana na huenea kwa kasi. Mbuni ulioshambuliwa haufi bali mkulima anaweza kupoteza mpaka asilimia 90 ya mavuno kwa mwaka kama hatazingatia namna bora ya kuuzuia.

  Ugonjwa huu hushambulia mibuni katika hatua tatu muhimu nazo ni:
  1. Maua yanapochanua.
  2. Punje zikiwa changa na laini.
  3. Punje zinazoiva.

  Madhara makubwa hutokea wakati punje zikiwa changa na laini.
  Mara nyingi mibuni iliyoshambuliwa na Chule Buni matunda yake huwa na vidonda vyeusi na vilivyobonyea na hudondoka na mengine hubakia kwenye mibuni. Yale matunda yanayobakia yanakauka na kuwa chanzo cha uambukizaji kwenye mavuno ya msimu unaofuata. Picha ya mbuni ulioshambuliwa na Chule Buni

  JINSI YA KUZUIA
  Ili mkulima aweze kudhibiti vizuri ugonjwa huu anashauriwa:
  • Kupunguza matawi yasiyotakiwa ili sumu iweze kupenya vizuri
  na kufikia matunda yote.
  • Kutumia sumu sahihi zilizopendekezwa kutumika kwenye kahawa.
  • Kutumia kiasi na kipimo sahihi kilichopendekezwa.
  • Kunyunyizia sumu wakati sahihi yaani:

  1. Kabla ya ugonjwa haujatokeza.
  2. Unyunyuziaji dawa uanze wiki tatu kabla ya mvua za vuli kuanza (Oktoba – Novemba)na kurudiwa tena mwezi mmoja baadae (Disemba).
  3. Unyunyiziaji unaofuata ufanyike tena wiki tatu kabla ya mvua za masika (Machi)na kurudiwa kila mwezi hadi matunda yakomae (Julai)


  Mkulima anashauriwa kunyunyizia sumu mojawapo ya hizi zifuatazo:
  1. Jamii ya mrututu – hasa zile nyekundu na za bluu zilizopendekezwa kudhibiti Chule buni. Mfano: Nordox, Cobox, Funguran-OH.
  2. Jamii isiyo ya mrututu – hizi mara nyingi ni zile za maji maji zilizopendekezwa kutumika kwenye kahawa mfano: Bravo, Daconil na Dyrene.

  FAIDA YA KUDHIBITI
  Mkulima akidhibiti vizuri Chule Buni anapata faida zifuatazo:
  1. Atakuwa amepunguza uwezekano wa kuendelea kuongeza kasi ya huu ugonjwa mwaka hadi mwaka.
  2. Atakuwa ameongeza wingi na ubora wa kahawa.
  3. Atakuwa amejiongezea kipato chake na kuwa na maisha bora zaidi.
  4. Atakuwa ameongeza pato la taifa kwa ujumla.

  MAMBO YA KUZINGATIA
  • Mwisho wa msimu hakikisha unaondoa matunda yote haswa yale yaliyoshambuliwa na chule buni.
  • Tambua wakati sahihi wa kuzuia huu ugonjwa.
  • Nunua sumu sahihi zilizopendekezwa.
  • Hakikisha matunda yote yanapata sumu vizuri.
  • Epuka ununuzi holela wa sumu kwani unaweza kununua hata zile zilizokwisha muda wake.
  • Mara upatapo tatizo onana na mtaalamu wa kilimo/afisa ugani aliyekaribu nawe.

  Asante sana kwa kuwa kusoma makala haya, nikutakie siku njema na  kazi njema
  0

  Add a comment

 23. KILIMO BORA CHA KUNDE
  KILIMO BORA CHA KUNDE
  KILIMO BORA CHA KUNDE : Kunde ni zao ambalo linaweza kulimwa kwa ajili ya chakula na biashara, pia ni zao lenye kiasi kukubwa cha protini na majani yake yanaweza kutumika kama mboga za majani. Vilevile ni zao ambalo linatoa mavuno ya Kiasi cha kilogram 500 hadi 1500 kwa ekari.

  Hali ya hewa ifaayo kwa kilimo hiki.
  Ni zao linalostahimili ukame, Kunde hukubari vizuri katika mwinuko wa mita 0 hadi 1500 kutoka usawa wa bahari. kunde huweza kulimwa katika maeneo yapatayo mvua kidogo kiasi cha milimita 500 hadi 1200 kwa mwaka. Lakini pia kunde hukuwa vizuri katika joto la nyuzi 28 had 32 C.

  Ardhi ifaayo kwa kilimo hiki.
  Huweza kulimwa katika udongo usiotuamisha maji wa aina tofauti tofauti kuanzia kichanga hadi mfinyazi. Kunde zinaweza kupandwa katika udongo usio na rutuba ya kutosha lakini hustawi vizuri katika udongo wa tifutifu kichanga au  mfinyanzi au mchanganyiko wa mfinyazi na kichanga wenye p.H kati ya 6 hadi 7.

  Maandalizi ya shamba.
  Shamba la kunde liandaliwe mapema kabla shughuli ya upandaji kuanza, Kama ni la kukata miti mikubwa miti ikatwe mapema, Kama ni la kufyeka nyasi na miti midogo shughuli hii ifanyike mapema kabla hatua ya kulimwa kwa shamba kwa kutumia trekta, Pawatilla, jembe la ng’ombe au la mikono. Shamba lisawazishwe na
  kukusanywa mabaki ya mimea au visiki na mawe madogomadogo kama yapo.

  Mbegu bora za kunde 
  Kuna aina mbalimbali za mbegu bora za kunde ambazo zimegawanyika katika makundi makubwa mawili ambazo ni;
  1.Kunde zinazosimama
  1. kunde zinazotambaa.

  BAADHI YA MBEGU BORA NA SIFA ZAKE.


  1.TUMAINI
  Hukomaa kwa muda wa siku 75 – 90. Aina hii ya kunde husambaa ina maua yenye rangi za zambarau na mbegu zake ni mviringo. Maeneo yanayoshauriwa kupanda ni yenye mwinuko wa mita 0 – 1500 toka usawa wa bahari. Inahitaji udongo mwepesi wenye rutuba na usiotuamisha maji. Kunde hizi hutoa mazao hadi tani 3 (kilogram 600 – 1500 kwa ekari)kwa hekta moja. Huvumilia virusi vya mozaiki vinavyotokana na wadudu mafuta wa kunde na bakiteria. Aina hii ya kunde ilizalishwa mwaka 1992 na Kituoa cha Utafiti cha Ilonga kwa ushirikiano na Naliendele.

  2.FAHARI
  Aina hii hukomaa kwa siku kati ya 75 – 90. Mmea husambaa na maua yana rangi ya zambarau. Mbegu zake ni za mviringo. Hustawi maeneo yenye mwinuko wa mita 0 – 1500 kutoka usawa wa bahari. Hutoa hadi tani 3 kwa hekta moja (kilogram 600 – 1500 kwa ekari ). Huvumilia magonjwa ya CABMV na mabaka. Fahari ilitolewa mwaka 1982 na Kituo cha Utafiti Ilonga kwa kushirikiana na Naliendele.

  3.VULI_1
  Inakomaa kwa siku 55 – 65. Hukua ka kunyooka na kusambaa kidogo. Mbegu zake ni nyekundu na za mviringo. Inastawi vizuri maeneo yenye mwinuko wa mita 0 – 1500 toka usawa wa bahari. Ikipataiwa matunzo mazuri huto hadi tani 2 kwa hekta moja (Kilogram 450-800 kwa ekari). Vuli – 1 inavumilia CABMV, BP na BB Vuli – 1 ilizalishwa mwaka 1987 kutoka kituo cha utafiti Ilonga.

  4.VULI_2
  Inakomaa baada ya siku 65 – 70 baada ya kupandwa inaota ikiwa imenyooka na kusambaa kidogo. Mbegu zake zina weupe uliofifia na ni mviringo. Aina hii husitawi vizuri maeneo yenye mwinuko wa mita 0 – 1500 kutoka usawa wa bahari. Katika matunzo mazuri aina hii huzalisha hadi tani 3.5 kwa hekta moja(Kilogram 800 -1200 kwa ekari) . Vuli – 2 huvumilia CABMV, BP na BB Vuli – 2 ilizalishwa mwaka 1987 kutoka kituo cha utafiti Ilonga.

  Kupanda kunde.
  Kunde hupandwa mwishoni mwa msimu wa mvua ili kuziepusha kukauka wakati mvua inaendelea kunyesha, pia unaweza kupanda wakati zao jingine linakaribia kuvunwa au katika shamba lililovunwa mpunga na lina unyevu wa kutosha. Muda mzuri wa kupanda kunde ni kuanzia mwezi Februari mwishoni hadi Machi na Aprili kwa maeneo ambayo mvua huchelewa kuisha.

  KUMBUKA mbegu zinazotambaa za kunde zipandwe miezi miwili kabla ya mvua kuisha kwani hizi huchukua siku nyingi kukomaa na Mbegu zinazosimama zipandwe mwezi mmoja kabla ya mvua kuisha.
  Kunde huitaji kiasi cha kilogram 4-12 za mbegu kwa ekari. kiasi cha mbegu kitategemea ukubwa wa mbegu,(mbegu kubwa zitahitajika kilogram nyingi) nafasi za upandaji,Ukipanda karibu karibu na mbegu itahitajika nyingi, Ubora wa mbegu katika uotaji. Zisizoota vizuri huitaji mbegu nyingi zaidi.

  Nafasi ya upandaji.
  Unaweza kutumia nafasi zifuatazo kwa kupanda kunde zako.

  KUNDE ZINASOSIMAMA
  Tumia sentimeta 45 hadi 50 mstari hadi msatari na sentimeta 15 hadi 20 shina hadi shina katika mstari / Sm ( 50 X 20 )

  KUNDE ZINAZOSAMBAA
  Tumia nafasi ya Sentimeta 70 hadi 75 mstari hadi mstari Kwa sentimeta 25 hadi 30 shina hadi shina katika mstari / Sm ( 75 X 30 ).
  Panda kwa kufikia kiasi cha sentimeta 2.5 hadi 5 ardhini na tumia mbegu tatu kwa kila shimo na baadaye punguza uache 2 kwa kila shimo kama unauhakika wa mbegu zako unaweza kupanda moja kwa moja mbili mbili kwa shimo.
  Palizi
  Palilia na Punguza mimea mapema katika shamba lako la kunde ili ikuwe ikiwa na afya bora.

  Mbolea
  Kama shamba lako halina rutuba ya kutosha unaweza kuongeza samadi kiasi cha tani tano kwa ekari moja na uhakikishe mbolea hii imemwagiwa au imenyeshewa na mvua ya kutosha kuiozesha kabla ya kupanda kunde zako na pia unaweza kupanda kwa kutumia mbolea ya TSP kiasi cha Kg 50 kwa ekari na baadaye kuzia mbolea ya SA kiasin cha Kg 50 kwa ekari.

  Wadudu na magonjwa.
  Wadudu waharibifu wa zao la Kunde wako katika makundi mawili:-
  1. Kundi la kwanza ni la wadudu wanaoshambulia mimea ikiwa shambani. Ina maana mmea hushambuliwa baada ya kuona hali inapokomaa na kutoa mbegu. Kundi la wadudu hawa lina tabia ya kufyonza (Sap = supu) ya mmea kwenye majani, matawi, mashina, maua hata mbegu hasa zikiwa changa kama vitunda.

  Njia hii ndiyo pekee kwa wadudu wa kundi hili kujipatia mlo ili waishi na kuzaliana. Katika kundi la pili kuna wadudu wenye tabia ya kukata mashina na kuangusha mimea michanga na wengine hutafuna majani na maua. Zaidi ya uharibifu katika kula mimea, wadudu wengi ni hifadhi ya viini vya magonjwa ya virusi.

  2.Kundi la pili ni la wadudu waharibifu baada ya mavuno kuwekwa ghalani. Athari ya wadudu hawa inapelekea wakulima kupoteza chakula ghalani pia kupunguza chakula ghalani pia kupunguza ubora wa mazao yanapopelekwa sokoni mfano Mahindi yanapofunguliwa soko lake ni duni.

  Uvunaji 
  Vuna kunde zako baada ya kukomaa na kuanza kukauka kwa kung’oa mashina au kuchuma kwa mikono.Kisha zisambaze kunde zako au amshina yako juani ili zikauke zaidi na uweze kuziondoa kwa urahisi kutoka katika maganda yake.Unaweza kuondoa maganda uyake kwa mkono au kuupigapiga taratibu au kwa kutwanga katika kinu taratibu bila kuzipasua kunde
  0

  Add a comment

 24. UFUGAJI BORA WA BATA BUKINI
  UFUGAJI BORA WA BATA BUKINI
  UFUGAJI BORA WA BATA BUKINI : Bata Bukini ni ndege ambao asili yao ni India na Japan. Hii ni jamii ya ndege wafugwao lakini tofauti kubwa ya bata wa kawaida wao wana asili ya usafi, hivyo hawapendi uchafu na kamwe hawali mizoga.

  Tofauti na ndege wengine au bata wengine wa kawaida, mfugaji wa bata bukini anaweza kupata kipato kikubwa kwa haraka na kwa gharama ndogo ukilinganisha na bata wengine.
  Kuna aina mbili ya bata bukini ambao ni weupe na wenye mchanganyiko wa rangi. Hali kadhalika hutofautiana katika utagaji wa mayai.

  Chakula
  Ndege hawa wanakula chakula kama wanacholishwa kuku, wanapendelea kula majani jamii ya mikunde kwa 50% na hawahitaji chakula kingi. Vifaranga ni lazima wapatiwe lishe kamili hasa protini kwa wingi ili waweze kujenga mwili, kukua vizuri na kuwa na afya nzuri.

  Kwa maana hiyo, vifaranga wanahitajika kupata walau 20% ya protini kwa wiki mbili za awali na baada ya hapo waweza kupunguza hadi 15% kulingana na kukua kwao hadi wanapokuwa wanaelekea kukomaa.

  Kama ambavyo mfugaji anaweza kutengeneza chakula kwa ajili ya mifugo wengine, pia anaweza kutengeneza cha bata bukini kama ifuatavyo:

  Mahitaji
  1. Mahindi kilo 10 ( hakikisha hayana dawa)
  2. Chokaa kilo 5 (ya kulishia mifugo)
  3. Dagaa kilo 10 (wanaotumika kulishia kuku)
  4. Mashudu kilo 20.

  Utengenezaji na Uhifadhi
  Baada ya kupima vyakula hivi kwa usahihi chukua pipa, changanya vizuri kisha walishe bata kulingana na wingi wao na uhakikishe wanapata chakula cha kutosha.Vipimo hivi hutegemea wingi wa bata unaowafuga lakini hakikisha uwiano huo unazingatiwa. Baada ya kutengeneza chakula unaweza kuhifadhi katika mifuko na kuweka katika eneo lisilokuwa na unyevu.

  Kuatamia
  Jinsi ilivyotofauti katika idadi ya utagaji wa mayai hivyo ndivyo uwezo wa kuatamia pia ulivyo. Bata Bukini weupe huatamia mayai 6 na wale wa rangi huatamia mayai 12
  Ndege hawa huatamia kwa siku 29, huangua vifaranga kwa siku 3 na mara nyingi hutotoa mayai yote, si rahisi mayai kubaki bila kutotolewa au kuharibika.

  Namna ya kutunza vifaranga
  Mara tu vifaranga wanapoanguliwa, wachukue na kuwatenga na mama yao kisha waweke katika banda safi lisilopitisha baridi. Unaweza kuwawekea taa ya umeme kama una uwezo ili kuwatengenezea joto.
  Pia, waweza kuzungushia banda lao kitu kizito kama blanketi ili kuwakinga na baridi au upepo.

  Banda
  Bata Bukini wanahitaji nafasi ya kutosha hivyo andaa banda kulingana na wingi wa bata unaotarajia kufuga.
  Hakikisha banda limesakafiwa au banda la udongo lisilotuamisha maji au unaweza kuweka mbao au mabanzi kisha unaweka maranda ili kuwakinga na baridi.

  Maji
  Ni lazima bata wapatiwe maji ya kunywa kila siku na hakikisha banda halikosi maji wakati wote. Safisha chombo cha maji na kubadilisha maji kila siku.
  Ndege hawa wanahitaji maji ya kunywa ya kutosha kama ilivyo kwa kuku. Hakikisha maji yako kwenye chombo ambacho hayatamwagika , kwani kumwagika kunaweza kusababisha kuibuka kwa magonjwa. Bata Bukini hawapendi uchafu. Hivyo maji yawe mahali ambapo hayatachafuka.

  Magonjwa
  Ni mara chache sana bata bukini kushambuliwa na magonjwa kama watawekwa katika hali ya usafi. Magonjwa yanayoweza kuwasumbua ni mafua na wakati mwingine kuharisha.

  Tiba za asili
  Unaweza kutibu bata bukini kwa njia za asili. Tumia mwarobaini, vitunguu (maji na saumu).

  1. Mwarobaini
  Unaweza kutumia dawa hii kutibu mafua kwa bata bukini wakubwa au vifaranga.

  Maandalizi
  Chukua kiasi kidogo cha mwarobaini kisha twanga vizuri kupata maji maji. Kamua maji ya mwarobaini, kisha changanya na maji uliyo andaa kuwanywesha vifaranga.

  1. Kitunguu Saumu na Kitunguu Maji:
  Dawa hii hutumika kukinga na kutibu bata bukini wanaoharisha.

  Maandalizi
  Unachukua kitunguu saumu au maji na kuondoa maganda ya nje kisha safisha na kukata vipande vidogovidogo na kuwawekea kama chakula.Unaweza kuwapatia kila siku hadi watakapopona.

  1. Majani:Bata Bukini chakula chao kikubwa ni majani. Majani yana vitamini A, hivyo hakikisha unawapatia ya kutosha. Wapatie majani jamii ya mikunde.
  Kutaga
  Bata Bukini huanza kutaga baada ya miezi saba na hutaga mara tatu kwa mwaka. Isipokuwa, utagaji wa bata bukini weupe na wa rangi hutofautiana katika idadi ya mayai, Bata Bukini weupe hutaga mayai sita tu lakini wale wa mchanganyiko wa rangi hutaga mayai kumi na mbili (mara mbili ya weupe)
  0

  Add a comment

 25. KILIMO BORA CHA NJEGERE
  KILIMO BORA CHA NJEGERE : Mara nyingi huwa  napenda kula ubwabwa na njegere, sijui kama na wewe mwenzangu unapenda kula njegere? Kama jibu  ndiyo basi nakusihi uungane nami katika makala haya ili uweze kujifunza namna  ya kulima kilimo hiki.

  Nakusihi kulima kilimo hiki kwa kwa sababu , kilimo cha njegere ni kilimo chenye tija kwa wakulima. Njegere ni mbegu za spishi za mimea katika jamii ya kunde ambayo hukuzwa sehemu mbalimbali  duniani katika maeneo ya ukanda wa juu.

  Spishi kadhaa za njegere ni:
  1. Njegere kubwa (chickpea)
  2. Njegere ya kizungu (common pea)
  3. Njegere sukari (snow pea and snap pea)

  Hapa nchini Tanzania njegere hulimwa nyanda za juu kusini, nyanda za juu kaskazini na kwenye miinuko ya Usambara na Uluguru. Katika ulimwengu njegere hulimwa kwa wingi katika Asia ya kati, Mediterania na Afrika ya kaskazini.
  Kuna aina mbalimbali za njegere zinazopatikana Tanzania kama Tanganyika yellow, Idaho white, Rondo na Mbegu za kienyeji.

  HALI YA HEWA:
  Kwa tafiti inaonesha zao la njegere hustawi vizuri maeneo yenye hali ya ubaridi wa sentigredi 17 – 21 C, na mwinuko zaidi ya mita 1200 usawa wa bahari na mvua, unyevu wa kutosha na maji yasiyotuama. Udongo uliowekwa mbolea, kulimwa kwa kina na wenye tindikali ya PH 5.5 – 6.5.

  UTAYARISHAJI WA SHAMBA:
  Maandalizi yanatakiwa yaanze kabla msimu wa mvua haanza, Shamba / bustani itayarishwe kwa trekta au pawatila au jembe la mkono au jembe la ng’ombe kwa kufuata mahitaji ya udongo kama kutotuamisha maji, kulimwa kwa kina. Changanya mbolea za asili (samadi au mboji) na udongo ili kurutubisha ardhi.

  UTAYARISHAJI WA MBEGU
  Chambua mbegu nzuri zinazoonekana hazina matatizo, zilizo na afya ili kupata mazao mengi. Unashauriwa kuandaa mbegu mapema ili kuweka maandalizi mazuri.

  UPANDAJI.
  Njegere hupandwa kipindi cha mvua ama kwa umwagiliziaji, maana udongo unatakiwa uwe na unyevu ili kufanya mmea kukua vyema, nafasi za kupanda:-

  1. i) 60 sm – 90 sm x 5.7 sentimita kwa mbegu fupi.
  2. ii) 12 sm – 15 sm x 5 – 7.5 sentimita katika safu mbili za sentimita 90 kwa mbegu inayotambaa.
  iii) Njegere hustawi vizuri zikipata sehemu za kutambalia.
  1. iv) Mbegu ya njegere huota baada ya siku 7 – 10.

  MBOLEA.
  Ukitumia mbolea za asili (samadi au Mboji) njegere hustawi vizuri. Katika kipindi cha ukuaji ni muhimu kuweka mbolea ya chumvichumvi za nitrogen kwa kipimo cha kg 40 kwa hekari.

  UPALILIAJI
  Njegere zipaliliwe zikiwa changa shamba lililotayarishwa vizuri na kuondolewa magugu ya mda mrefu (Perrenial weeds) linaweza kupalliwa mara moja, kwa sababu njegere hukua haraka, na zinaweza kushindana na magugu. Baada ya kutoa maua, njegere zisipaliliwe ili kuongeza mazao.
  Magugu hushindana na kunyanganyana na mimea kutumia virutubisho. Pia huongeza kivuli wakati wa utoaji maua na kusababisha upungufu mkubwa wa mazao. Palizi hufanyika kwa mkono au kutumia dawa za kuua magugu.

  MAGONJWA & WADUDU

  MAGONJWA.


  Ascochyta.
  Kutokea kwa mabaka makubwa ya kahawia kwenye majani na matunda. Pia hutokea hata kwenye shina. Katikati ya baka huwa rangi ya kijivu, kingo nyekundu / nyeupe husababishwa na fangasi aina ya Ascochyta pisi.

  Root Rot na Blight disease.(kuoza kwa mizizi na Blingt)
  Husababishwa na fangasiA. pinodella na mycosphaerella pinodes.
  Dalili: – madoa madogomadogo yenye rangi ya zambarau / rangi ya kahawia iliyokaza au madoa meusi ambayo huungana na kusababisha jani na maua kuwa yenye rangi nyeusi .

  Kuzuia.
  1. Kutumia mbegu zisizo na magonjwa.
  2. Kuzika mabaki ya mazao yaliyoadhirika kwa miaka 3 – 4.

  Downy mildew.
   Husababishwa na fangasi Erysiphe polygoni.
  Dalili: Majani kuonekana kama yamemwagiwa unga na baadae na
  kufa. Ugonjwa unaathiri zaidi mimea kipindi cha uhaba wa
  unyevunyevu.

  Kuzuia: – Kutumia sulphur ya unga kama inavyoshauriwa.

  Fusarium wilt:– Husababishwa na fangasi / ukungu Fusarium oxysporum.
  Dalili:
  1. Majani kubadilika rangi kuwa manjano.
  2. Mimea kudumaa.
  3. Ugonjwa ukitokea kwenye mimea michanga huua mmea wote.
  Kuzuia: – Tumia mbegu yenye uvumilivu kwa ugonjwa huu.

  Virusi – Mmea huonekana kuwa na uvimbeuvimbe kuzunguka jani. Mmea hudumaa.
  Kuzuia: – Kutumia mbegu zisizo na maradhi.

  WADUDU
  Wapo wadudu wengi ambao hushambulia zao la njegere. Baadhi ni kama American bollworm, Bean flies, Bean Aphids, Pea Aphids huambukiza virusi na Green peach aphids.
  Inashauriwa kumwona mtaalam wa kilimo aliye karibu yako kwa ufafanuzi wa kuwazuia wadudu waharibifu.

  UVUNAJI
  Kwa njegere teke / mbichi hukomaa siku 60 – 90 na kwa njegere kavu huchukua siku 80 -150 kukomaa . Njegere teke huvunwa punje zikiwa bado mbichi, Uvunaji hufanyika mara 2 – 3 kwa wiki wakati wa kipindi cha ukuaji. Zaidi ya kilo 3000 kwa hekta za njegere teke huvunwa, Njegere kavu huvunwa wakati punje zimekauka na kuwa ngumu na ni muhimu kuwahi kuvuna njegere kavu ili kutopoteza mavuno zikipasuka. Mavuno ya punje kavu na kilo 1500 kwa hekta.
  asante sana kwa kusoma makala haya


 26. MBINU BORA ZA KULEA VIFARANGA VYA KUKU
  MBINU BORA ZA KULEA VIFARANGA VYA KUKU
  MBINU BORA ZA KULEA VIFARANGA VYA KUKU : Ufagaji wa vifaranga vya kuku una changomoto nyingi, wafugaji wengi wamekuwa hawajui mbinu ambazo zitawasadia kuweza kufuga vifaranga katika mbinu ambazo zitawafanya vifaranga wasife. kama nawe ni miongoni mwa wafugaji hoa, H siku ya leo nitakupa mbinu bora za kutunza vifaranga.

  Utunzaji wa vifaranga upo wa aina mbili, ambao ni kama ifutavyo;

  (1) UTUNZAJI WA ASILI
  Njia hii hutumika kwa vifaranga wachache ambao kuku jike (tetea) huachiwa kulea vifaranga wake. Wakati tetea anapo walea utagaji hukoma, hivyo huchukua muda mwingi huyo kuku kurudia kutaga.

  (2) KUWATUNZA VIFARANGA KWA KUTUMIA CHANZO CHA JOTO:
  Mfumo huu wengi wanauona kuwa ni mgumu kutokana na kushindwa kuutumia na hatimaye vifaranga kufa. lakini mfumo huo ni mzuri kwa vifaranga hukuwa vizuri endapo mfugaji ataamua kufuga kwa kufuata mbinu bora.

  Hivyo kama kweli unataka kufuga vizuri vifaranga unatakiwa kufanya mambo yafutayo;

  BANDA BORA
  Vifaranga hawahitaji eneo kubwa sana katika majuma manne ya kwanza. Nafasi inayohitajika kwa kukadiria ni meta 1 ya mraba kwa vifaranga 16. Kwa mfano nyumba yenye meta 10 za mraba inatosha kutunzia vifaranga 160 hadi wanapofikisha umri wa majuma manne. Vipimo vya nyumba yenye eneo kama hili inaweza kuwa na hatua 5 kwa 4. Utajenga banda kutegemea na eneo ulio nalo.
  BANDA BORA LA VIFARANGA
  BANDA BORA LA VIFARANGA
  VYOMBO KATIKA NYUMBA YA KULELEA VIFARANGA

  (1) KITALU/BROODER/BRUDA:


  Bruda ya kukuzia vifaranga inatakiwa iwe ya mduara isiyopinda mahali popote, ni vizuri kutumia silingboard au mbao. Kwanini inatakiwa iwe ya mduara; tunafanya hivo kwa ajili ya kuzuia wasilundikane kwenye kona ndio maana mzunguko wa bruda unatakiwa kuwa ni mduara. Kwa maeneo ya kijijini bruda inaweza kutengenezwa kwa kutumia viroba vya magunia. Ndani ya bruda hiyo ndio kuna kuwa na chanzo cha joto, unaweza tumia jiko la mkaa, balbu, au chemli.
  Katika banda la vifaranga ni muhimu kuwa na joto lisio kithiri hasa pale kwenye siku za mwanzo na nyakati za usiku. Mwanga na mzunguko wa hewa ndani ya bruda ni muhimu kwani huvutia na kuvishawishi vifaranga kuanza kula.
  Weka madirisha makubwa yenye kuingiza hewa safi na kutoa ile chafu. Banda lisilo na hewa ya kutosha huchochea kuenea kwa magonjwa ya mfumo wa hewa. Andaa nafasi ya kutosha ili kuepuka vifaranga kurundikana.

  UTATAMBUAJE KUWA JOTO LIMEZIDI AU LIMEPUNGUA.
  (1) Kama joto linatosheleza utaona yafuatayo.
  •Vifaranga vitalia kwa furaha.
  •Vitakimbia kimbia.
  •Vitakunywa maji.
  •Vita chagua chagua na kuonesha shughuli nyingi.
  Zote ni dalili zuri za kuonesha kuwa joto linatosheleza.

  (2) Kama joto halitoshelezi utaona yafuatayo;
  •Vifaranga wakiona baridi hujikusanya kalibu sana na chanzo cha joto.
  •Au hujikusanya wenyewe kwa pamoja na kulia kwa sauti.
  Dalili hizi huonesha kuwa joto ni pungufu hivyo kuna ulazima wa kuongeza joto.

  (3) Kama joto limezidi utaona yafuatayo
  •Vifaranga hukaa mbali na chanzo cha joto.
  •Husinzia na kuzubaa
  • Kama ni kwenye chumba vifaranga hukimbilia mlango ili vipate upepo.
  Katika hali hii ni dalili za kuonesha kuwa joto limezidi hivyo unatakiwa kupandisha taa juu, kupunguza vyanzo vya joto na kuwapa vifaranga maji mengi.

  VYOMBO VYA KUWEKEA MAJI

  Vifaranga wanahitaji maji na katika kuwapa maji hakikisha kuwa hayo maji ni safi. Unaweza ukayachemsha kisha ukayachuja kama utakuwa na wasi wasi nayo.
  Tukumbuke kuwa kuna magonjwa yanayo ambukiza kupitia yale maji wanayokunywa vifaranga wako hivyo kwa kuhakikisha usalama wa maji utakuwa umewanusuru vifaranga wako dhidi ya magonjwa hayo.
  Unaweza kununua vyombo vya kuwekea maji (drinkers), lakini kwa vifaranga ni vema katika hayo maji yaliyomo kwenye drinkers ile sehemu ya kunywea uweke kokoto safi ndogo ndogo ili kuwafanya vifaranga wasilowe wakati watakapo kuwa wanakunywa maji. Kama hauna uwezo wakununua drinker basi unaweza ukatumia njia yeyote ya kutengeneza chombo cha kuwekea maji ila hakikisha kuwa hakivuji.
  Hakikisha kuwa banda ni safi na kavu wakati wote ili kuzuia maladhi kwani chanzo cha maambukizi hutokana na unyevunyevu pia.

  VYOMBO VYA KUWEKEA CHAKULA
  Wafugaji wengi hutumia feeders kuwalishia vifaranga wao chakula. Na wengine hutengeneza vyombo mfano wa feeders kwa kulishia vifaranga wao. Yote sawa ila cha muhimu ni kuzingatia usafi wa hivyo vyombo.
  Kuna wengine huamua kuwamwagia vifaranga chini chakula mle mle wanapo lala. Hii ni hatari kubwa kwa vifaranga hao kuambukizana magonjwa kiurahisi. Kwani kinyesi cha kifaranga kinacho umwa kikichanganyika kwenye hiko chakula kisha akaja kifaranga mzima akala chakula hiko kuna uwezekano wa kuambukizwa ugonjwa kiurahisi sana.
  VYOMBO VYA CHAKULA
  Hapo ndio utakuta mtu vifaranga wake wanaumwa kuhara damu (coccidiosis), amewapa dawa hawaponi. Atajiuliza kwanini hakuna cha kwanini hapo hiyo ni kwasababu banda lako, matunzo yako ni mabaya. Banda lako limekuwa banda la maambukizi wala sio uponyaji tena.

  Sifa za banda bora kwa ajili ya vifaranga.
  1. Banda lenye kuingiza hewa safi na ya kutosha
  3. Banda lenye kuingiza mwanga wa kutosha
  4. Banda lenye kuzuia upepo mkali
  5. Banda lisio ruhusu maji kusimama na kuingia ndani na kwamba liwe imara.
  6. Banda liwe rahisi kusafisha
  7. anda liwe na eneo la kutosha kulingana na idadi ya kuku.
  8. Banda liwe sehemu salama, kwa wezi na wadudu


 27. KILIMO BORA CHA NANASI

  KILIMO BORA CHA NANASI
  KILIMO BORA CHA NANASI : Nanasi ni tunda la kitropiki, linalopendwa na walaji wengi kwa sababu ya ladha yake tamu na harufu yake nzuri. Tunda hili laweza liwa mara tu baada ya kuvunwa, baada ya kulipika, au kama juisi. Nanasi ni chanzo kizuri cha vitamin A na B, pia inakiwango kingi tu cha vitamin C pamoja na madini kama vile: patasiam, magnesiam, kalsiam, na madini chuma.

  Asili ya nanasi inaaminika kuwa ni Brazil na Paraguay huko Amerika ya Kusini. Hapa Tanzania, nanasi hulimwa zaidi maeneo ya Bagamoyo, Kibaha (Pwani), Tanga, Mtwara, Lindi, Geita na Mwanza. Lakini pia maeneo yote ya pwani ya Tanzania yanafaa kwa kilimo cha nanasi.

  Hali ya hewa inayofaa kwa ukuaji wa nanasi
  Kilimo cha nanasi kinapendelea hali ya hewa ya joto na husitawi vema katika mwinuko kati ya mita 0-1750 kutoka usawa wa bahari. Mwinuko wa mita 1300 hadi 1750. Mahitaji ya joto ni kati ya nyuzi joto 18°C hadi 35°C.

  Udongo unaofaa kwa kilimo cha nanasi
  Kwa kilimo cha nanasi chachu (pH) ya udongo inayofaa ni 5.5 hadi 6.0, na hustawi vizuri zaidi katika udongo tifutifu na udongo wenye kichanga usiotuamisha maji. Ingawa nanasi huweza kustawi katika udongo wa aina yoyote ile, udongo wa mfinyanzi haufai kwa kilimo cha nanasi.

  Maandalizi ya shamba
  Lima shamba kwa trekta, kwa ng’ombe ama kwa jembe la mkono kwa kina cha sentimita 30 hadi 45. Shamba la nanasi unaweza kulilima kwa sesa (flat-bed) au kwa matuta (furrows).

  Kwa sesa: chimba mashimo kwa nafasi ya sm.60 kati ya mistari, sm. 30 kati ya miche na sm. 80 kati ya kila mistari miwili. Weka mbolea kianzio katika kila shimo na upande, hakikisha shamba lina unyevu wa kutosha kabla ya kupanda. Weka tani 10 hadi 15 za mbolea ya kuku, weka pia viganja 2 vya mbolea ya zizi katika kila shimo.

  Upandaji wa mananasi
  Zipo aina mbali mbali za ‘mbegu’ (machipukizi/maotea) lakini yale yanayochipua kutoka ardhini hufaa zaidi na hukomaa mapema. Chagua machipukizi mazuri yenye umri mdogo na yenye kulingana kwa ukubwa. Iweke miche kwenye kivuli kwa siku 3 kabla ya kuipandikiza iweze kutoa mizizi haraka. Pandikiza mwanzoni mwa mvua za masika. Nafasi iwe sm.60 kati ya mistari, sm. 30 kati ya miche na sm. 80 kati ya mistari miwili. Pandikiza miche 50,000 katika hekta moja. Chovya miche kwenye dawa ya Diazinon au Fention kwa muda wa dakika 25 kabla ya kuipandikiza ili kuzuia mashambulizi ya wadudu.

  Palizi
  Palilia shamba mara kwa mara ili kuhakikisha shamba halina magugu. Katika kilimo cha nanasi magugu hudhibitiwa kwa palizi ya jembe, kung’oa kwa mkono ama matumizi ya viuagugu. Matumizi ya viuagugu hurahisisha zaidi palizi ya nanasi ukizingatia kuwa nanasi huwa na miiba katika ncha za majani yake ambazo huchubua ngozi endapo palizi za jembe zitatumika. Njia nyingine ni matumizi ya matandazo (mulch) ya majani au plastiki (plastic mulch) maalum kuzuia magugu.


  Mahitaji ya mbolea ya mananasi

  Weka mbolea ya NPK gramu 50 hadi 70 kwa kila mche wakati wa kupanda. Weka tena gramu 85 kwa kila mche baada ya miezi 3 na pia miezi 3 baadae.

  Wadudu na Magonjwa yanayosumbua minanasi
  Nanasi ni zao lisilosumbuliwa na wadudu ama magonjwa mara nyingi. Hii ni faida kubwa sna kwa wakulima wa nanasi! Hivyo endapo patatokea mashambulizi ya wadudu na magonjwa, ushauri zaidi wa kitaalam utafutwe kukabiliana na tatizo husika. Hakikisha unakagua shamba ili kuzuia wadudu kama wataonekana.

  Uvunaji wa mananasi
  Nanasi huanza kutoa maua miezi 12 hadi 15 baada ya kupanda kutegemeana na aina ya nanasi au maotea ya mbegu yaliyotumika, muda wa kupanda na joto la mahali husika. Kwa kawaida nanasi hukomaa miezi 5 baada ya kutoa maua, hivyo nanasi huchukua miezi 18 hadi 24 kukomaa/kuiva. Katika kilimo cha nanasi, mimea ikitoa maua kwa nyakati tofauti tofauti itasababisha kuvuna kidogo kidogo na kwa muda mrefu. Kwa sababu hiyo ndio maana ni muhimu kupanda kwa wakati mmoja mbegu zenye umri na ukubwa sawa.

  Kwa wanaofanya kilimo cha nanasi kibiashara (commercial pinapples production) hutumia kemikali aina ya Ethrel (@ 100 ppm) mwezi mmoja kabla ya kuanza kutoa maua ili mimea mingi iweze kutoa maua kwa wakaii mmoja, angalau 80% ya mimea yote.

  Vuna wakati kikonyo cha nanasi kimebadilika rangi kuwa njano ya dhahabu. Kata kikonyo cha nanasi chenye urefu wa sm. 30 kikiwa kimeshikana na nanasi na upunguzie majani ya kichungi chake.

  Utunzaji wa mananasi
  Hifadhi nanasi katika eneo lenye ubaridi huku kikonyo chake kikielekea juu. Hakikisha unauza nanasi mara tu au siku 2 hadi 3 baada ya kuvuna ili kutunza ubora wake


 28. KILIMO BORA CHA MAKAKARA (PASSION FRUITS)
  KILIMO BORA CHA MAKAKARA (PASSION FRUITS) : Ni mimea inyotambaa na kuhimili hali nyingi za hewa (sio ukame). Mmea huu hustawi zaidi ukanda usio na baridi wastani wa 20c – 30c na kiasi cha mvua 1500mm za ujazo kwa Mwaka, tunda huwa na ukubwa wa sentimeta 10 kwa kipenyo na uzito gramu 90.

  kuna aina kadhaa za matunda haya lakini yale ya kijani/manjano hustawi zaidi ukanda wa pwani na yale yenye wekundu fulani hustawi zaidi maeneo ya misitu, hupendelea udongo wa kichanga wenye mbolea na usiotuamisha maji, pia udongo usiwe na chumvi nyingi na pia kusiwe na mwamba chini kasi cha mita moja tu.

  Upandaji.
  Mbegu zipandwe kwanza kwenye mifuko ya plastiki yenye udongo wenye rutuba ya kutosha , kiasi cha Mbegu 3 kwa kila mfuko na mara zinapoota mimea ikingwe na jua kali na ikifikia urefu wa sentimeta 30, huweza kuhamishiwa shambani
  Kwenye shamba lako hakikisha kuna nguzo zenye waya mmoja kwa ajili ya mimea kutambaa juu yake, sehemu ya juu baada ya nguzo kuzikwa chini ibakie kama mita mbili na kati ya msatari na mstari iwe ni mita 2 (ukanda wa pwani ) na mita 3 ukanda wa juu kiasi, na umbali kati ya nguzo na nguzo kwenye mstari ni mita 6, na mimea ipandwe umbali wa mita 3 kati ya nguzo na nguzo kufuata mstari.
  UPANDAJI WA KITAALAM
  Mbolea
  Mbolea za viwandani ziwekwe kutokana na hali ya udongo, muone afisa ugani kilimo ili afanye vipimo kujua mahitaji na upungufu wa udongo,

  Magonjwa na madudu.
  Wadudu kama chawa wa mimea na mchwa wekundu ndio adui wa makakara, pia fangasi husshambulia sana maua ya makakara. Dawa za jamii ya kopa zitumike mara dalili za magonjwa au wadudu kuonekana, kiasi cha kilo 2.8 – 3 hutosha kwa hekta moja au gramu 225 kwa ajili ya dumu moja la lita 20

  Magugu.
  Makakara yanatakiwa yawe kwenye shamba safi lisilo na majani na magugu, jembe la Mkono au madawa kama ROUND-UP na GRAMOXONE ynaweza kutumika mimea ikishaefuka na kuwa juu kwenye waya

  Kufundisha matawi ya mimea.
  Ni lazima kuyafundisha matawi mawili ya kwanza kwa kuyaelekeza kutambaa kwenye waya kila moja likielekea upande wake na matawi yatakayoota kutokana na matawi makuu nayo yaelekezwe juu kwenye waya yakifikia ukubwa wa sentimeta 30 – 40.
  KUPUNGUZA MATAWI
  Kupunguza matawi.
  Silazima kupunguza matawi kwa sababu mmea mkubwa zaidi ndio hutoa matunda mengi zaidi, labda kama kuna matatizo katika uchumaji ndio unaweza kupunguza baadhi ya matawi kiasi.


  Uvunaji.
  Uvunaji huanza baada ya miezi 8 – 9 baada yam mea kupandwa na matunda hukusanywa baada ya kudondoka yenyewe chini baada ya kuiva kila baada ya wiki moja, matunda yahifadhiwe sehemu kavu na isiyo na joto , kiasi cha tani 5 – 10 huweza kupatikana katika hakta moja kwa msimu


 29. KILIMO BORA CHA MIWA
  KILIMO BORA CHA MIWA : Kilimo cha miwa ni kilimo chenye tija kwa mkulima, kilimo hiki kinaweza kufanywa na mtu yeyote yule aidha awe ameajieiwa au laaa! Jambo la msingi ni kuhakikisha anajitoa kikamilifu katika kuhakikisha  unawekeza akili yake katika kulima kilimo hiki.
  Kuna aina kuu 2 za miwa katika mbegu za miwa zilizo shamili sana ambazo ni:
  1. Bungala
  2. Miwa myekundu.
  Unachotakiwa kufanya katika kulima kilimo hiki ni, Kwanza kabisa tafuta ekari moja ya shamba kisha anza maandalizi lakini zingatia kupuguza matumizi makubwa ya pesa kadri iwezakanavyo yaani kwa shughuli nyinginezo ambazo unaweza kuzifanya mwenyewe ni vyema ukazifanya ili kupunguza matumizi makubwa ya pesa mfano kulima, kupiga dawa, kupalia n.k
  Tafuta mbegu ya miwa ya Bungala miwa hii ni laini sana na ni rahisi kuichana kwa kutumia meno, baada ya kupata miwa hii kata vipande vipande vya pingili tatu tatu .Kumbuka kwamba miwa ni rahisi sana kushambuliwa na mchwa pale tu inapokuwa imepandwa.

  Ili kuzuia isiliwe na mchwa nenda katika maduka ya kilimo na ununue moja wapo ya madawa yafuatayo:-
  1. TAP 4% GR Tumia gram 100 za dawa kwa lita takribani 20 za maji kisha nyunyizia katika mashina ya miwa.
  2. Taniprid 25 WG. Tumia gram 100 za dawa kwa lita takribani 20 za maji au pia unaweza kuweka kijiko kimoja cha chai katika kila shina.
  3. Imida Gold Mls 20 kwa lita 20 za maji na unyunyizie shinani.
  4. Gammalin 20. Tumia gram 100 kwa lita takribani 20 za maji. Na unyunyizie katika vipande vya miwa au chovya vipande vya miwa katika maji hayo yaliyo na Gammalin 20 na ndipo uende ukavipande shambani kwako.
  5. Gladiator FT.
  6. Stom

  Mambo yakufanya:
  Zingatia kama utatumia aidha Gladiator au Gammalin au Stom, chukua ndoo ya maji ya lita 20 kisha uichanganye na dawa uliyoinunua kisha chukua kipande cha muwa na kukizamisha ndani ya maji hayo na baadae uende kuipanda shambani kwako, hivyo uewezekano wa miwa yako yote kuote utakuwa ni mkubwa sana maana shida kubwa ni mchwa na hapo tayari utakuwa umeidhibiti.

  UPANDAJI WA MIWA
  Hakikisha unapokuwa unapande miwa yako acha nafasi ya mita moja (1m) kati ya mche na mche pia hakikisha una acha nafasi ya mita moja (1m) kati ya mstari na mstari. Kumbuka awali tulisema katakata muwa wako kupata vipande vilivyo na vipingili vitatu vitatu, hivyo sasa unapokuwa unapande miwa hii hakikisha hizo pingili zote 3 zimezama ndani ya ardhi na kipande kidogo tu ndio kibakie juu ya uso wa ardhi na mche wako huo unapoutumbukiza kwenye ardhi uwe umelala wastani wa nyuzi 30.

  Zile pingili katika muwa wako kumbuka ndipo sehemu hasa miwa inamokuwa inachipuka na kuota. Mantiki ya kuacha nafasi kubwa kati ya mche na mche ni kwa sababu hilo shina lako moja ulilolipanda linaweza likachipua vijimiwa vingine zaidi hata ya ishirini kama ukiliacha shina liendelee kuzaa tu kwa kadri linavyotaka na hatimaye shamba lako litakuwa msitu hata usiopitika.

  Lakini kibaya zaidi ni kwamba miwa yako itakosa afya njema na mwisho wa siku miwa yako haitakuwa bora hata bei haitakuwa nzuri pindi utakapoamua au wakati wa kuuza utakapofika. Hivyo unashauriwa kuacha miwa kati ya tano mpaka kumi lakini mfano ukiacha miwa mitano katika shina moja ni dhairi hewa na mwanga vitakuwa vya kutosha shambani lakini hata chakula na virutubisho vingine kwa miwa hiyo vitakuwa lukuki na sio vya kung’ang’aniana hivyo mwisho wa siku utapata miwa mirefu na minene ambayo sokoni itakuwa na mvuto mkubwa kwa wateja.

  Mfano chukulia kwamba umelima ploti ndogo tu ya upana mita 50 kwa urefu mita 70, kumbukumbu namna ya upandaji miwa kama tulivyozungumza hapo awali umbali wa mita moja moja kwa kila shina. Hivyo kwa ploti ya shamba hili utakuwa na miche au mashina uliyopanda kiasi cha 70×50=3500 (mashina elfu tatu na mia tano) sasa chukulia kwa hesabu rahisi kwamba kila shina umeruhusu miwa mitano tu ndio ikuwe pale maana yake kwa mashina 3500 utazidisha mara 5 ambapo itakuwa 3500×5= 17,500 hiyo ndio itakuwa jumla ya miwa itakayovunwa shambani.

  Kwa tafiti zilizofanywa zinaonesha kama hautaki shida na unahitaji pesa ya haraka haraka sana huko huko shamba, basi unaweza ukajumlisha miwa yako kwa bei ya chini sana yaani tukadilie vile kwamba tunahitaji pesa ya haraka so tuuze muwa mmoja kwa bei ya jumla ya 300 hivyo jumla ya pesa utakayoipata itakuwa 17,500 × 300 = 5,250,000 (milioni tano laki mbili na nusu). Hiyo ni pesa ya haraka haraka huko huko shambani .

  Ila kama ukiweza kusogea zaidi na kuuza kwa faida maana kama umeweza kupigana mpaka kuweza kuikuza ni dhairi kwamba unastahili kupata faida iliyo njema kwako hivyo ni muhimu kuangalia masoko yamekaaje pande zote za miji, ila kama utaweza kuifikisha Dar es Salaam ambako kiuhalisia soko lake ni kubwa sana .

  Kama ukienda Kariakoo bei ya rejareja kwa muwa aina ya bungala wenye wastani wa urefu mita moja na robo bei yake ni 5,000 lakini ukienda mtaani kwa muwa huo huo aina ya bungala mfupi kidogo bei yake inakwenda mpaka 3,500 hivyo chukulia kwamba umeweza kufikisha Dar es Salaam huo mzigo wako wa miwa, hivyo mapato yako kama utaamua uuze kwa bei ya jumla ya 1,500 kwa kila muwa hivyo kiasi cha fedha utakachokipata kitakuwa ni sawa na idadi ya miwa yako zidisha bei ya kujumlishia yaani ingekuwa 17,500 × 1,500= 26,250,000 hii ni pesa utayoipata kwa halali kabisa wala haujamzulumu mtu.

  Hapo umelima ploti ndogo tu, sasa chukua pengine umelima ekari moja na kwa shamba la miwa ekari moja kiwango cha chini kabisa cha wewe kuvuma miwa yako ni jumla ya miwa 24,500. Sasa chukulia kama umeweza kuipeleka Dar es Salaam maana yake utapata jumla ya 24,500 × 1,500= 36,750,000. Sasa mfano ndo ukalima ekari 4 hadi 5 hapo ni hakika unatoka katika kundi la uchumi wa chini na kuingia katika uchumi wa kati. Jamani bado hatujachelewa kungali bado fursa ziko kinachohitajika hapa ni kuthubutu tu, Mungu akubariki unapoyatafari haya lakini pia pindi ukifanikiwa usimsahau Mungu maana yeye ndiye nguzo ya mafanikio yako yote. 30. FAIDIKA KWA KULIMA KILIMO BORA CHA FIGIRI
  FAIDIKA KWA KULIMA KILIMO BORA CHA FIGIRI : Ulimaji wa mbogamboga hususani figiri  ni shughuli nzuri ambayo hufanywa na baadhi ya watu wanao jikita katika kujipatia kipato. sasa leo nami nimependa kukupa somo mpendwa wangu kuhusu hiki kilimo.

  Naam kilimo cha mboga mboga kinawatoa watu katika hali ya ukata na kuwapa maisha ya kati na hata wakati mwingine kuwapeleka katika ukwasi. Namaanisha shughuli hii itakupatia kipato cha kukidhi haja za kimaisha yako endapo utaamua kulima.

  Tuangalie mambo muhimu katika kilimo hiki.

  KUANDA SHAMBA / BUSTANI
  Huwezi kulima pasipo kuanda shamba au bustani yako.

  Namna ya kuanda shamba.
  Lima shamba lako vizuri na kuondoa nyasi/ magugu yote yaliyoootea katika shamba. Kisha katua vizuri shamba lako kwa lengo la kuulainisha udongo wa shamba lako.

  Baada ya hapo mwagia mbolea ya kutosha katika shamba lako kisha mwagilia maji ya kutosha kutengeneza unyevunyevu wa kutosha.

  KUMWAGA MBEGU
  Mbegu humwagwa katika bustani kwa kurusha. Lakini mbegu hizi kabla hazija mwagwa kwenye bustani lazima uchanganye na mchanga kwa lengo la kupatia nafasi pindi utakapo mwaga mbegu na kupelekea figiri kuota kwa mpangilio. Lakini pia ikumbukwe mbegu huota ndani ya siku 3. Tangu kumwagwa.

  Utaendelea kumwagilia bustani yako kila baada ya siku 2. Kwa udongo wa tifutifu. Na kila siku kwa udongo wenye aina ya kichanga kwani aina hii ya udongo hu pitisha maji kwa urahisi na kukauka haraka.

  Mboga hii huchukua siku 30. Kuwa tayari kwa kuuzwa na wateja kwenda kula.
  Mpaka kufikia hapo hatuna la ziada, endelea kutembelea blog ya kilimo bora. 31. KILIMO BORA CHA CHOROKO
  KILIMO BORA CHA CHOROKO : Choroko ni zao la chakula na biashara lenye kiasi kikubwa cha protini na madini ya phosphorus na calicium. Zao hili likilimwa vizuri hutoa mavuno kati ya Kg 400 hadi 900 kwa ekari moja. Hivyo kwa yeyote yule mwenye nia ya dhati ni vyema akajikita katika kuhakikisha analima kilimo hiki.

  UDONGO NA HALI YA HEWA IFAAYO.
  Choroko hustawi katika udongo wa aina tofauti tofauti usiotuamisha maji.Hulimwa kutoka mita 0 hadi 1500 kutoka usawa wa bahari japokuwa kuna mbegu nyingine zinaweza kukubali zaidi ya ukanda huu.Hili ni zao linalostahimili ukame.

  AINA ZA CHOROKO
  Kuna aina kuu mbili za choroko ambazo pia zimegawanyika katika makundi mawili,choroko nyeusi na choroko za kijani.

  1. CHOROKO ZINAZOTAMBAA-hizi ni choroko ambazo zinarefuka sana na hutambaa sehemu mbalimbali.

  1. CHOROKO ZINAZOSIMAA-Hizi ni choroko ambazo zinakuwa kwa kusima kwenda juu.Hizi huchukua muda mfupi kukomaa wastani wa siku 60-70.


  KIPINDI KIZURI CHA UPANDAJI WA CHOROKO
  Choroko hazihitaji maji mengi hivyo ni budi zipandwe mwishoni mwa msimu wa mvua,Pia zinaweza kupandwa katika shamba lililolimwa mpunga.

  NAFASI ZA UPANDAJI WA CHOROKO NA KIASI CHA MBEGU
  Choroko huitaji mbegu kiasi cha kilogram 8 hadi kumi kwa ekari moja.
  Panda choroko zako kwa nafasi ya sentimeta 30 mastari na mstari na sentimeta 10 shina hadi shina (30 x10 )sentimeta au (40 x 8 )sentimeta.

  SAMADI NA MBOLEA ZA VIWANDANI
  Kama shmba lako halina rutuba ya kutosha unaweza kuongeza samadi kiasi cha tani tano kwa ekari na pia unaweza kupanda kwa kutumia mbolea ya NPK kg 50 kwa ekari.weka mbolea zote kabla ya kupanda.

  UMWAGILIAJI
  Kama umepanda kipindi cha ukame sana au unalima kilimo cha umwagiliaji basi mwagilia shamba lako upate unyevu wa kuotesha mbegu, kisha baada ya mbegu kuota kaa siku 6 hadi 10 na umawgilie tena. Mara tatu za kumwagilia zinatosha kwa choroko.

  PALIZI
  Palilia shamba lako mapema kuzuia magugu.Palizi moja inaweza kutosha.

  MAGONJWA YA CHOROKO
  1. Yellow mosaic virus ( Ugonjwa wa manjano)
  Dalili: mmea unakuwa wa njano na madoa ya njano katika majani.
  Kinga na tiba-Panda mbegu zinazostahimili magonjwa.

  1. Powdery Mildew (Ukungu)
  Dalili-Majani yanakuwa na vidoti vya njano ambavyo vinabadilika kuwa vya kahawia au kijivu haraka na ambapo kunakuwa na unga unga katika majani.
  Kinga na tiba-Panda mbegu zinazostahimili ukungu,Pulizia dawa za ukungu (Fungicide).
  anza kupuliza wiki tatu baada ya mimea kuota na kuendelea kulingana na hali halisi.

  1. LEAF SPOT (Vidoti katika majani)
  Dalili-majani yanakuwa na vidoti vya mviringo na visivyo na umbo maalum ambapo katikati  yanakuwa na rangi rangi ya kijivu na weupe na mistari ya rangi ya wekundu-kahawia au nyeusi-kahawia.ugonjwa huu husababisha hasara hadi ya asilimia 58 ya mapato.

  Kinga na Tiba-Panda mbegu inayostahimili ugonjwa huu,Choma mabaki ya mimea hii na ile ya jamii moja baada ya kuvuna.Pulizia dawa za ukungu (Fungicide) Katika nafasi ya wiki mbili mbili kama eneo hilom linashambuliwa mara kwa mara na ukungu.

  WADUDU.
  Kuna wadudu mbalimbali wanaoshambulia choroko kama vile aphidi,funza wa vitumba,nzi wa maharage.Wazui wadudu hawa kwa kupuliza dawa za wadudu mara tu baada ya mimea kuota,dawa kama karate,twigathoate,dimethote na nyinginezo zinaweza kutumika.

  UVUNAJI
  Mara tuu choroko zinapofikia asilimia 85 ya ukaukaji zinabidi zivunwe ukichelewa zitapukutikia shambani 32. KILIMO BORA CHA MBAAZI
  KILIMO BORA CHA MBAAZI


  KILIMO BORA CHA MBAAZI : Mbaazi ni zao la chakula ambalo pia linaweza kulimwa kama zao la biashara kutokana na kuwa na soko zuri. Mbaazi ina kiasi kikubwa cha protini. Mbaazi inaweza kutoa mavuno ya tani 6 hadi 8 kwa hekta
  MAHITAJI MUHIMU YA MBAAZI.
  • Mbaazi zinafaa kulimwa katika maeneo ya ukanda wa chini kutoka usawa wa bahari na pia hata sehemu za nyanda za juu nazo zinafaa kulimwa zao hili. 

  • Ni zao linalostahimili ukame na hili linalifanya kulimwa hata katika maeneo yanayopata mvua za wastani na yale yanayopata mvua kwa kiasi kidogo.

  • Mbaazi hukua vizuri katika maeneo yenye wastani wa mua wa mm 400-1000 kwa mwaka,katika maeneo yenye mvua zaidi ya mm 1000 kwa waka hustawi ila ni rahisi kupta ugonjwa wa mnyauko.

  • Mbaazi hustawi vizuri katika hali ya joto ya nyuzi 18-30 C. Pia kama hali ya udongo na unyevu ni nzuri  zinaweza kukua vizuri katika hata katika 35 C.

  UDONGO UNAOFAA KWA KILIMO CHA MBAAZI
  Mbaazi zinastawi katika udongo wowote ambao hautuamishi maji.Hivyo zao hili linaweza kulimwa katika maeneo yoyote na pia linaweza kulimwa katika udongo wenye asili ya mfinyanzi katika maeneo yanayopata mvua kwa kiasi kidogo. Hustawi vizuri katika udongo wenye pH 5-7, Pia pH 4.5 – 8 zinaweza kulimwa

  AINA KUU ZA MIMEA YA  MBAAZI
  KUNA AINA KUU TATU ZA MIMEA YA MBAAZI
  • Mbaazi za muda mrefu: Hii ni mbaazi ambazo zinawezwa kuvunwa katika misimu zaidi ya miwili.Huchukua muda mrefu kukua hadi kuvunwa kwa mbaazi zake.Baada ya mbaazi kuvunwa Mbaazi hukatwa nusu yake na kuruhusu Machipukizi yake kukua na kuvunwa tena msimu unaofuata na zoezi hili hufanyika ziadi ya msimu mmoja.Huchukua Siku 180 hadi 270 kupandwa hadi kuvunwa.

  • Mbaazi za Muda wa kati; Hizi hulimwa kwa msimu mmoja ila huchukua mda wa kati katika kukomaa kwake.huchukua siku 140 hadi 180.

  • Mbaazi za muda MfupiHizi hulimwa kwa msimu mmoja na baada ya kuvunwa mimea yake hukatwa na kung’olewa na kupandwa mbegu mpya msimu unaofuata.mbegu hizi huchukua siku 120 hadi 140.

  MAANDALIZI YA SHAMBA
  Andaa shamba lako mapema kadri utakavyoweza kulima kulinga na aina ya kilimo unachotumia, hakikisha umeondoa magugu shambani na uchafu mwingine ambao unaweza kuinyima mimea ya mibaazi kukua vizuri.

  UPANDAJI.
  Mbaazi za Muda Mirefu
  ; Panda kwa mistari kwa umbali/ nafasi ya sentimeta 150 kwa 100.(Sentimeta 150 Mstari na mstari na sentimeta 100 Shina hadi shina katika mstari)
  Mbaazi za Muda wa Kati; Mbaazi.Panda kwa mstari nafasi ya sentimeta 100  kwa 60
  Mbaazi za Muda  Mifupi; Panda kwa mstari  kwa umbali/ nafasi ya sentimeta 90 kwa sentimeta 60

  ANGALIZO:
  Maaneo ya Pwani ambayo yanarutuba kwa wingi na joto la kutosha mimea inakuwa kwa kasi na ili upate mavuno bora lazima uhakikishe mimea yako unaipa nafasi ya kutosha,Hivyo uwe makini na nafasi za mimea yako uanapopanda shambani.

  MATUMIZI YA MBOLEA.
  Mara nyingi zao la mbaazi halihitaji matumizi ya mbolea na samadi. Ijapokuwa Hustawi zaidi katika shamba lenye rutuba ya kutosha.

  PALIZI
  Mimea ya mibaazi huitaji kupaliliwa mapema ili kufanya ikue katika hali ya afya bora na kusaidia kuongeza mavuno yako.

  WADUDU WANAOSHAMBULIA MIBAAZI NA MBAAZI
  Mbaazi ni mojawapo ya mazao ambayo hayashambuliwi sana na wadudu japokuwa wapo wadudu ambao kuna maeneo mengine hushambulia kwa kiasi kikubwa mbaazi nao ni funza wa tumba na wadudu wapekechaji wa mbaazi. Zuia wadudu hawa kwa dawa za wadudu kama ATTAKAN-C,Karate au dawa nyingine za wadudu.

  MAGONJWA YA MBAAZI
  Ugonjwa mkuu unaoshambulia mbaazi ni mnyauko wa fusaria ( fusarium wilt).Ambao husababisha shina la mbaazi kuwa na rangi nyeusi,ugoro au kahawia.ugonjwa huu huzuia mfumo wa usafirishaji wa mmea.
  Zuia ugonjwa huu kwa kuzungusha mazao shambani kila baada ya msimu kuisha.usipande kila msimu mbaazi tuu.Kila msimu badilisha zao.

  UVUNAJI WA MBAAZI
  Mbaazi zikishakomaa na kuanza kukauka zivunwe mapema kwa kukatwa matawi yenye mbaazi na kukaushwa zaidi kisha Mbaazi zitenganishwe kwa mikono au kwa kupigwa hayo matawi  taratibu  baada ya kukaushwa sana.
 33. JINSI YA KUSINDIKA MBOGA ZA MAJANI KWA NJIA YA UKAUSHAJI : Ukashauji wa mboga za majani ni njia ambayo inatumika sana maeneo ya vijijini lakini si vibaya ikianza pia kutumika maeneo ya mijini kwani ni njia nzuri sana. Kwa maneno mengine njia hii ni usindikaji wa mboga za majani. Na moja kati faida kubwa ambayo utaipata mara baada ya kukausha mboga hizi ni kwamba mboga hizi zinaweza kukaa kwa muda mrefu hivyo kusaidia wakati wa mboga zinapokuwa hadimu.


  MAMBO YA MSINGI YA KUZINGATIA WAKATI WA KUKAUSHA MBOGA ZA MAJANI NI IFUATAVYO:
  1. Chuma mboga nyingi katika bustani yako. Hajalishi ni mboga za aina gani.

  • Hatua inayofuata ikatekate vipande vidogo vidogo.

  • Baada ya hapo chemsha katika maji ya moto. Lakini jambo la kuzingatia ni kwamba chemsha mpaka ibadili rangi yake, isiwe katika hali ya ukijani.

  • Mara baada ya kuchemka na kujiridhisha kwamba imeiva vizuri. Epuka kisha subiri kwa muda fulani mpaka ipoe vizuri.

  • Ikisha poa vizuri  chukua kitu ambacho kitakusaidia kuianika mboga hiyo mpaka ikauke vizuri.

  • Mara baada ya kukauka vizuri ni kwamba unaweza ukaiifadhi sehemu safi ili ije kuliwa hapo baadae.
   

 34. KANUNI 5 MUHIMU ZA KUFANYA KILIMO BORA CHA MAHINDI  KANUNI 5 MUHIMU ZA KUFANYA KILIMO BORA CHA MAHINDI
  KANUNI 5 MUHIMU ZA KUFANYA KILIMO BORA CHA MAHINDI : Moja kati mbinu ambazo zitakufanya uweze kulima kilimo chenye tija kujua kanuni ambazo zitakuzaidia kuweza kulima kilimo hicho, na kanunia hizo nitazieleze katika Makala haya. Mahindi ni zao muhimu linalo limwa katika maeneo ya kitropiki. Pia zao hili hulimwa katika udongo wenye uchachu pH 6-6.5. lakini pia hustawi zaidi kwenye maeneo yenye mwinuko wa 2500.

  KANUNI YA KWANZA; Kutayarisha shamba mapema.
  • Tayarisha shamba la mahindi mara tu baada ya kuvuna mazao ya msimu uliopita.
  • Mahindi hustawi sehemu yenye udongo wenye rutuba na usiosimamisha maji.
  • Moto usitumike wakati wa kuandaa shamba.

  Faida ya kuandaa shamba mapema
  1. Baada ya kuvuna,udongo bado ni mlaini hivyo hulimika kwa urahisi kwa kutumia jembe lolote.
  2. Masalia yatakayofunikwa udongoni huoza mapema.
  3. Hupunguza magugu.
  4. Hupunguza wadudu waharibifu.

  KANUNI YA PILI ; kujua wakati wa kupanda mbegu sahambani.
  Wakati wa kupanda hutatanisha kwani mvua haitabiriki, Kama mvua hunyesha nyakati na majira yale yale ya mwaka basi kalenda ifuatayo inaonyesha tahere za kupanda zao la mahindi katika eneo lako.
  1. Mbeya na maeneo ya jirani, mwanzoni mwa mwezi Novemba hadi Desemba mwishoni.
  1. Morogoro na maeneo ya jirani, Mwezi Januari katikati hadi Februari katikati
  1. Iringa na maeneo ya jirani, katikati ya mwezi Novemba hadi Desemba mwishoni
  1. Songea na maeneo ya jirani, katikati ya mwezi Novemba hadi Januari mwanzoni.

  Kupanda mahindi mapema ni muhimu kwani uwezekano wa kuvuna mazao mengi ni mkubwa. Kwa mashamba makubwa makubwa sana wakati wa kupanda uwe wiki moja kabla ya mvua kuanza kunyesha na isizidi wiki mbili kabla ya mvua.
  Isiwe mapema zaidi kwani mbegu zitaharibiwa na joto kati ya udongoni wadudu, panya, ndege na wanyama wengineo.

  FAIDA ZA KUPANDA MAPEMA
  1.  Mahindi yanapata mvua ya kutosha hadi kukomaa.
  2.  Magonjwa kama yale ya ya majani (streak ugonjwa wa milia) hayatatokea au yatakuwa kidogo.
  3. c) Mbolea uliyoweka itayeyuka pamoja na mahindi yastawi vizuri.

  KANUNI YA TATU KUCHAGUA MBEGU BORA
  Mbegu bora ni zile zilizo zalishwa kitaalamu.
  1. a) Ni safi hazijabunguliwa na wadudu.
  2. b) Huzaa mazao mengi.
  3. c) Hustahimili magonjwa.

  AINA ZA MBEGU
  1.  Mbegu aina ya chotara (hybrid)
  2.  Aina ya ndugu moja (synthetic)
  3.  Mbegu aina ya composite
  Mbegu za kisasa zikitumiwa vizuri katika vizuri katika misingi ya kilimo zina uwezo wa kuzaa magunia 50-80 au tani 5.5 – 7.5 kwa hekta moja au umi kwa hekari.

  MAPENDEKEZO YA MBEGU ZA KUPANDA
  Kuna mbegu nyingi za kisasa zilizoko kwenye soko mfano wa
  SIDCO ,PANNAR, CHOTARA, kutoka KENYA n.k Ni vyema
  kufuata ushauriwa wataalamu wa kilimo

  KANUNI YA NNE KUPANDA
  Idadi ya mimea katika eneo ni muhimu kwani ikazidi
  1. Mazao hupungua.
  2. Mmea huangushwa na upepo
  3. Mabua mengi hayazai.
  Idadi ya mimea nayo ikipungua kwenya eneo husababishwa mavuno kupungua jambo la kufanya ni kupanda mbegu katika nafasi sahihi zilizoshauriwa na wataalamu.

  KIASI CHA KUPANDA
  1. Mbegu za mahindi huhifadhiwa kwa dawa kali(sumu
  2. Kiasi cha kilo 20(ishirini) za mbegu kinatosha kupanda hekari moja., (Hii hutegemea na aina ya mbegu)

  Nafasi za kupanda.
  75cm x 30cm
  75cm x 60cm
  90cm x 25cm
  90cm x 50cm

  KANUNI YA TANO; KUTUMIA MBOLEA
  Mahindi hustawi na kuzaa vizuri iwapo yatapatiwambolea pamoja na matunzo mengine ya kilimo bora. Ukipanda mbegu bora bila kutumia mbolea ni kazi bure.

  KUNA AINA MBILI KUU ZA MBOLEA
  1. Mbolea za asili mfano; samadi,mboji na majani mabichi,mbolea hizi hua na virutubisho vya kutosh ambavyo havijulikani vipo kwa kipimo kiasi gani
   KANUNI 5 MUHIMU ZA KUFANYA KILIMO BORA CHA MAHINDI
  1. Mbolea za viwandani, hizi hua na virutubisho vya kutosha na vipimo hujulikana, hii inasaidia kujua ni kiasi gani kitumike kwa kipindi gani.

About Anonymous

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.