Pakua App Yetu Playstore Bofya Hapa!

XKILIMO

KILIMO:JINSI YA KUANZISHA BUSTANI NDOGO YA MBOGAMBOGA I Mshindo media

https://mjasiriamaliplus.blogspot.com/
JINSI YA KUANZISHA BUSTANI NDOGO NYUMBANI.
Uanzishaji wa bustani nyumbani ni jambo ambalo huwaweza kulifanya kwa kiasi ambacho kinaweza kukuletea faida kemkem, Kwa kutumia malighafi unazo ziona nyumbani waweza fanikisha zoezi hili, iwe ni mifuko ya nailoni. Makopo, gunia, au kiji pande kidogo cha ardhi na ukaweza kukitunza.
Mboga ambazo unaweza kuzizalisha nyumbani ni kama mchicha, nyanya, kitunguu, sukuma wiki, kabichi, chinizi, majani ya maboga na pilipili (kali au hoho).
Mboga zilizo nyingi hutumia muda wa miezi mitatu hadi kufikia muda wake wa kuvunwa, Hivyo hakiwezi kukuchosha na mazao kama mchicha huchukua wiki karibuni 2 mpaka 3 na unaweza kutumia/kuvuna.
Faida za mbogamboga hizi ni nyingi ikwemo kiafya kwani husaidia kuongeza damu mwilini, kutupatia nguvu na hata kutusaidia uwezo wa kuona vizuri kama mchicha na karroti. Pamoja na hata kiuchumi kama uzalishaji wako hapo nyumbani utakidhi na ziada waweza fanya biashara.
FAIDA ZA BUSTANI HIZI ZA NYUMBANI.
- Ni rahisi sana kufanya.
- Ni chanzo kizuri cha mboga nyumbani.
- Inasaidia watoto kupenda kula mboga za majani, kwani uweza kuziona jinsi zinavyozalishwa na kupenda zaidi uzalishaji.
- Ungalizi wake ni wa karibu na hata udhibit wa magonjwa ni mkubwa.
AINA ZA BUSTANI AMBAZO NI RAHISI SANA KUANZISHA UKIWA NYUMBANI.
- Kwa kutumia makopo au makasha ya mbao.
- Kwa kutumia gunia.
- Kwa kuandaa kitalu.
BUSTANI YA MAKOPO/NDOO NA MAGUNIA
Bustani ya makopo hiutaji vitu vifuatavyo,
- Kopo/ndoo.
- Udongo.
Udongo huwezesha mmea kujishikiza pia kuupatia mmea virutubisho muhimu.
- Mbolea za samadi.
Kwaajili ya kuupatia mmea viini lishe.
- Pumba za mpunga/mchanga
Pumba husaidia kuupatia mmea kupitisha maji, pia kupitisha mizizi.
HATUA MUHIMU ZA KUFUATA.
1. Changanya udongo wako na mchanga/pumba za mpunga na mbolea kwa uwiano wa udongo 5:2:1
2. Toboa chombo utakachotumia iwe ni gunia au kopo.
3. Weka mchanganyiko wote katika chombo ulicho nacho kisha weka mche au mbegu.
BUSTANI ZA KWENYE KITALU/VITALU
Endapo hautatumia kopo au gunia tengeneza kitalu chako kwa kuchanganya udongo na mbolea pekee.
Kisha panda mbegu/miche yako kwa nafasi.
UANGALIZI.
Kila zao lina aina yake ya uangalizi japo nyingi hifanana sana kwa zao kama nyanya hutaitajika kuweka miti maalumu kwa ajili kuipatia sapoti, kuepuka kuanguka chini na hata kupelekea kufa kwa mmea.
MAMBO YA KUZINGATIA.
- Mwagilia mboga yako mala baada tu ya kupanda na kuendelea ikitegemeana ni aina gani ya mboga.
- Unapoona wadudu au dalili yeyote ya magonjwa fuata taratibu zote za utumiaji viatilifu kuzuia kusambaa kwa wadudu au magonjwa hayo.
- Mboga kama sukuma wiki, nyanya, pilipili, waweza vuna mara kwa mara, kazi yako ni kumwagilia tu.
- Usiweke bustani yako katika kivuli na bali iwekwe katika sehemu ambayo mwanga wa jua itaifkia mimea, kwa kuiweka katika kivuli itapelekea mmea kudumaa, hivyo inapaswa ikae katika mwanga.
- Endapo hutatumia makopo au gunia unatakiwa kubadilisha udongo wako kwa muda, Baada ya mavuno ya misimu ili kuakikisha mboga zako zina pata virutubisho ya kutosha.
CHANGAMOTO ZA BUSTANI HIZI ZA MBOGAMBOGA.
Kwa watu wengi hupatikanaji wa maji ya uhakika inaweza kuwa ni shida sana.
Kuna baadhi ya mbinu unaweza tumia na ukatumia maji uliyo nayo kwa ufanisi wa hali ya juu.
- Kwa kutumia makopo ya maji makubwa, weka maji na kisha toboa tundu dogo kwa chini kisha funga kifuniko chako vyema kutorusu hewa kuingia, kwa kufanya hivyo utawezesha matone madogo ya maji kuufikia mmea, nah ii itakuwezesha kutotumia maji na maji megi na bali maji yataakayo tumika yatatumika kwa ufasaha sana.
- Tumia kilimo cha matone, kwa kutengeneze mfumo mdogo tu wa mirija hata kwa wale watakao tumia kitalu. Weka kiifadhia maji kwa juu na kisha unganisha kwa kutengeneza mirija midogo/mipira midogo na itoboe kulingana na nafasi ya miche yako.
- Weka matandazo kuzunguka mmea yanaweza kuwa ya nyasi kavu au Maranda ya mbao, hii itasaidia kuhifadhi unyenyevu uliopo kuendelea kuwepo kwa kupunguza upotevu wa maji kwa jua kali.
............................................................................................................................................

About Anonymous

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.