Pakua App Yetu Playstore Bofya Hapa!

X
MAPISHI

MAPISHI: Visheti Vya Namba Nane Vya Maziwa Na Uji Wa Ngano | Mshindo media

MAPISHI: Visheti Vya Namba Nane Vya Maziwa Na Uji Wa Ngano | MjasiriamaliPlus.

MAHITAJI
 Visheti
1.Unga wa Ngano ¼ Kg

2.Maziwa ya maji Kikombe Kidogo 1

3.Yai 1             

4.Hamira Vijiko vya Chakula 2

5.Siagi Vijiko 2

6.Sukari Kijiko 1

7.Chumvi Kiduchu

8.Mafuta ya Kukaangia Lita 1

Shira
1.Sukari Kikombe Kidogo 1

2.Hiliki Ilotwangwa Kijiko cha Chai 1
  
3.Arki Vanilla na Ice Cream Nusu Vifuniko Vyake

4.Maji Robo Kikombe

Uji wa Ngano Nzima
1.Ngano Nzima Kikombe Kikubwa 1

2.Maji ya Kuchemshia
  
3.Hiliki nzima punje 10
  
4.Maji ya kupikia uji Lita 2
    
5.Unga wa ngano Kikombe Kikubwa 1

   6.Sukari Kikombe Kidogo 1

MAANDALIZI
Visheti
1. Chunga unga kwenye bakuli na changanya na vitu vyote vikavu yaani,sukari,chumvi
Hamira

2.Vunja yai weka kwenye mchanganyiko wako

3.Mimina maziwa taratibu mpaka unga ushikane uweze kuukanda
4. Kanda unga wako kiasi cha dakika 7

5.Weka Siagi kijiko 1 endelea kukanda kiasi cha dakika 2

6.Ukipata donge laini weka kwenye bakuli lipake kijiko cha siagi kilobakia kasha funika kwa kitambaa kisafi au plastic wrap katika sehemu ya joto na acha kiasi cha nusu saa au mpaka liumuke  vizuri.

8.Nyunyiza unga katika chombo cha kuekea visheti vyako
   
9.Likande donge lako kiasi cha dakika moja kisha kata madonge madogo madogo 16

                  MAPISHI: Visheti Vya Namba Nane Vya Maziwa Na Uji Wa Ngano | MjasiriamaliPlus.
10.Chukua donge moja ingiza vidole kati kutengeneza tobo mpaka upate umbo la duara lilitobolewa(Mfano kama Bangili)
  
        
    
11.Kisha zungusha duara lako upande wa juu peleka kushoto na upande mwengine kulia mpaka kati pakutane upate umbo la namba8

             
MAPISHI: Visheti Vya Namba Nane Vya Maziwa Na Uji Wa Ngano | MjasiriamaliPlus.
12. Rudia kuzungusha kwa madonge 15 yaliyobakia mpaka uyamalize

          
13.Vifunike sehemu ya joto acha viumuke kiasi cha dakika 20
   
Uji
1.Safisha ngano vizuri na uzioshe kasha weka kwenye sufuria na maji kiasi
  
2.Weka unga na maji kwenye bakuli na ukoroge kuondoa mabuje

JINSI YA KUPIKA
Visheti
1.Weka mafuta jikoni acha yapate moto kiasi
  
2.Weka kisheti kimoja kimoja hakikisha huvipikwi sana vikibadilika rangi tu vitoe
  
3.Weka kwenye Tray ulioiweka tissue au chujio
  
4.Acha vipoe kiasi cha dakika 10.
JIFUNZE: Jinsi ya Keki ya Vannilla na Cocoa kwa Njia rahisi.
Shira
1.Weka sukari,hiliki na maji kwenye sufuria

2.Acha ichemke kiasi dakika 1 ongeza arki
  
3.Wacha ichemke hadi ifanye mapovu na subiri dakika 3 kisha weka visheti vyako

4.Shika sufuria yako anza kuvipeta kasha rudisha jikoni acha kwa dakika 2

5.Rudia hio hatua(4) mpaka sukari igande kwenye visheti vyako ifanye rangi nyeupe

6.Acha Vipoe tayari kula na uji,kahawa au kinywaji upendacho
k  
Uji
1.Chemsha ngano mpaka ziive na zikauke maji yote
  
2.Weka maji Lita moja kwenye sufuria acha yachemke

3. Mimina mchanganyiko wa unga na maji ulio ukoroga mwanzo kwenye maji yanayo chemka kasha koroga vizuri mpaka uchanganyike

4.Acha uji uchemke kiasi cha dakika 10 kisha weka tui

5.Baada ya dakika 5 weka sukari na hiliki na ngano koroga vizuri uji wako

6.Acha kwa dakika 5 nyengine epua na uache upoe

7.Tayari kula na visheti,maandazi au mkate wowote uupendao

MAPISHI: Visheti Vya Namba Nane Vya Maziwa Na Uji Wa Ngano | MjasiriamaliPlus.
Angalizo:
1.Unaweza kukandia tui badala ya maziwa na visheti vikawa vizuri tu

2.Uji ukiwa mzito unaweza kuongeza maji ukiwa jikoni ukauzimua

3.Unaweza kuweka aina moja ya arki au hata aina tatu tofauti kwenye shira
4.Ukiona visheti vimegandana sana usishtuke endelea kuvipeta kwa nguvu kidogo kisha virudishe jikoni mpaka sukari igande 
5.Hakikisha mafuta unayopikia Visheti hayana harufu yoyote mfano (yasinukie alizeti) na masafi yasiwe yamepikiwa chochote

Furahia Uji Na Visheti Vyako.

*******************************************************

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.