Pakua App Yetu Playstore Bofya Hapa!

X
MAPISHI

MAPISHI: Jinsi ya Kupika Keki Rahisi Ya Vanilla Na Cocoa | Mshindo media

MAPISHI: Jinsi ya Kupika Keki Rahisi Ya Vanilla Na Cocoa | MjasiriamaliPlus

MAHITAJI/INGREDIENTS
1.Siagi Robo kilo(1/4 Kg)

2.Sukari Robo kilo(1/4 Kg)

3.Unga Robo kilo(1/4 Kg)

4.Mayai 6

5.Arki Vanilla Kijiko cha chai 1

6.Cocoa Vijiko vya Chakula 3

7.Baking Powder Kijiko Cha Chakula 1

8.Chungwa 1

7.Maganda ya Chungwa Kijiko Cha Chakula 1

8.Chumvi Kiduchu

9.Fruit Cake Kikombe Cha Chai Nusu(Sio Lazima)

10.Juisi ya Chungwa Vijiko 3
 
MAANDALIZI/PREPARATIONS
1.Chekecha unga kwenye bakuli kisha weka chumvi na baking powder na uchanganye vizuri kwa mwiko

2.Osha chungwa vizuri kasha lipare kwa kipario ili upate maganda yake kijiko kimoja

3.Weka maganda ya chungwa na Fruit Cake kwenye ungana uchanganye tena vizuri

4.Weka sukari na siagi kwenye bakuli jengine

5.Saga mchanganyiko wako kiasi cha dakika 3

6.Weka Vanilla endelea kusaga kiasi cha dakika 2

7.Weka mayai yako moja moja mpaka yamalize huku ukiendelea kusaga

8.Weka juice ya chungwa kisha saga tena kidogo

9.Malizia kuweka unga kidogo kidogo mpaka umalize wotehuku ukisaga

10.Chukua bakuli chota mchanganyiko wako weka miko 3

11.Kisha weka cocoa kwenye kibakuli uloweka mchanganyiko wako changanya vizuri kwa kijiko kikubwa

12.Washa Jiko la Umeme moto wa nyuzi joto 160

13.Chukua trei weka karatasi ya kupikia

14.Kisha Anza kuweka mchanganyiko mweupe na kati weka wa cocoa kasha malizia mweupe

JINSI YA KUPIKA/HOW TO COOK
1.Weka trei jikoni kwa muda wa dakika 50 ndio fungua jiko na tizama keki yako

2.Ingiza kijiti kisafi kwenye sehemu mbali mbali za keki yako kuangalia kama imeiva

3.Ikiwa kijiti kitatoka na umaji maji basi keki yako bado rudisha jikoni

4.Kijiti kikitoka kikavu zima jiko toa keki wacha ipoe
5.Ikipoa toa kwenye trei na ikate vipande tayari kuliwa na kinywaji upendacho

MAPISHI: Jinsi ya Kupika Keki Rahisi Ya Vanilla Na Cocoa | MjasiriamaliPlus
Angalizo:Note;
1.Hakikisha unafata vipimo sahihi vya unga,siagi,sukari,baking powder na mayai ili upate keki nzuri

2.Ukikosea vipimo vya keki hupelekea kutoiva au kuwa ngumu

3.Kuwa makini na jiko lako kama lina moto mkali tumia nyuzi joto ambazo hazitounguza keki yako

4.Tumia Chombo ambacho mchanganyiko wa keki hautojaa mpaka juu ili ipate nafasi ya kuiva vizuri kwani ikipata joto hufura na huweza kupelekea mchanganyiko ukamwagika kabla ya kuiva

5.Unaweza kupika kwa kutumia mkaa pia

6.Hakikisha hukati keki yako mpaka ipoe inaweza kupelekea kukatika katika

7.Keki inaweza kukaa mpaka siku 3 mpaka 4 kwenye mazingira ya joto na siku 6 mpaka 7 kwenye mazingira ya baridi bila kuharibika

Furahia Keki Yako.

********************************************************

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.